Tuzungumze mapenzi

hassan yahaya

Member
Aug 27, 2022
32
34
Mwandishi: Hassan yahaya ( B.Sc )
Contact: hassanmatola508@gmail.com

habari ndugu zangu, awali ya yote napenda nitoe maana ya mapenzi. Mapenzi ni ukaribu unajijenga baina wa watu, wanyama, mtu na kundi la watu, kiumbe kimoja na kingine au kiumbe na kitu au hali fulani ambayo hufanya vitu hivyo kujihisi ni sehemu ya kitu kingine. Kimsingi mapenzi hujengwa katika namna tofauti tofauti kama vile kiasili, kitabia, vichochezi, au ukaribu.

Kwa mtazamo wa kiasili, mapenzi hutokea tu bila kisababishi fulani mfano mtu ukaenda ugenini na ukakutana na watu mbalimbali lakini kati yao ukampenda mtu mmoja na si wengine na mtu huyo ndio ukawa karibu nae sana kuliko wengine.

Kwa mtazamo wa kitabia, mapenzi hutokana na mtu kuvutiwa na kushawishiwa na tabia ya mtu fulani. Mfano kutokana na mtu kijiweka nadhifu mda wote wapo watu watampenda kutokana na tabua yake hiyo. Pia tabia kama ucheshi, upole n.k husababisha mtu kuwa na maoenzi na mtu mwingine.

Kwa mtazamo wa vichochezi, mapenzi husababishwa na vichochezi fulani ambavyo humfanya mtu akavutiwa na mtu mwingine. Mfano wa vichochezi hivi ni kama vile pesa, utajiri, au uwezo wa kufanya mambo fulani. Mfano hivi sana mapenzi baina ya watu wengi huchochewa na pesa.

Kwa mtazamo wa ukaribu, mapenzi hujengwa na watu fulani kuwa karibu kwa mda mwingi. Yaani katika siku masaa mengi wanakaa pamoja pamoja. Kwa mfano watu wanafanya kazi katika ofisi moja kama vile walimu. Mapenzi yao husababishwa saba na kuwa karibu katika mazingira yao ya kazi. Hii hutokea kwasababu watu hao huchunguzana sana mfano wakati wa kuongea, kutembea au mda mwingine vile wanavyoongozana wanaporudi nyumbani.

Leo hii suala la mapenzi linawasumbua watu wengi sana, pia watu wengi akili zao zimetekea sana katika mapenzi na mwisho wa siku wanaishia kuumizwa na kujiona hawana thamani na kufikia hatua ya kujiua au kusababisha ugomvi.
Yote haya hutokea bila kujua nini chanzo ya yote.

Kulitatua hili kwanza ifahamike mapenzi mahala pake ni moyoni, hivyo hakuna upendo kama moyo haujapenda. Mapenzi ya dhati kabisa ni yake ambayo watu wamependana kutoka moyoni na sio kwa pesa, ukaribu au kwa vichocheo kwasababu kama mlipendana kwaajili ya pesa siku zikiisha mapenzi hayatakuwepo tena, kama mlipendana kwasababu ya ukaribu siku mkiwa mbalimbali mfano mmoja wenu akahamishiwa kituo cha kazi mapenzi yataanza kushuka na mwishowe kukatika kabisa na kama mlipendana kutokana na tabia mapenzi yeno hayapo hatarini sana kwasababu tabia ni mwenendo wa mtu hivyo ni ngumu kubalika haraka. Lakini tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa mtu anavyozidi kukua tabia nazi hubadilika taratibu, hivyo mapenzi hayo yanaweza kupungua ila kwa kiwango kidogo.

Ushauri wangu kwenu ndugu zangu ni kwamba katika suala hili la mapenzi kwanza elekea kwenye hisia zako, pia kama hisia zako zinaenda kwa mtu ambaye hayupo na hisia na wewe usikate tamaa kwani huwezi kuvutiwa na mtu mmoja. Hivyo katika kuchagua mpenzi ni vizuri kuchagua kigezo cha kupenda kutoka moyoni au kuoenda kutokana na tabia.

Shukran
0cb26d466f0112dafeff03b745fb0ecd.jpg
 

Attachments

  • 155a7daba71c3485.jpg
    155a7daba71c3485.jpg
    40.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom