Tuweke ushabiki pembeni: Hatua ya Robo Fainali ni ngumu kuliko tunavyopiga hesabu za vidole na kujifariji

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,361
12,901
Nimepita kwenye vijiwe nongwa vya mtaani nakusikiliza mashabiki wa kariakoo (sunche na kapeto) wanavyopiga hesabu za kutoboa robo mpaka fainali Tena hesabu nyepesi kabisa utadhani robo Kuna Namungo, Azam au Mashujaa.

Twende kwenye matazamio ya kiuchambuzi tuchambue timu zitakazokutana na mapacha wa kariakoo (sunche na kapeto)

Hizi ndiyo zinazoweza kukutana nazo baada ya draw ya Robo kufunguliwa.

Simba

1. Al Ahly
2. Mamelody Sundowns
3. Petro Atletico de Luanda

Yanga
1. Asec Mimosas
2. Mamelody Sundown
3. Petro Atletico de Luanda

Al ahly na Mamelody Hawa wanafahamika uwezo wao tuwaweke pembeni kwanza.

Tumuongelee Petro de Luanda na Asec Mimosa Hawa nao new comer baada ya wydad na Raja Casablanca kukaa NJEE.

*Petro de Luanda hii timu ilitinga Robo kwa kishindo kikubwa na ndiyo timu ambayo haijafungwa/haijaruhusu bao katika mechi 6 Petro de Luanda ametoka na clean sheets 6.
Tunapowaongelea Hawa Petro de Luanda ni timu iliyo Moto kabisa katika msimu huu kwa hiyo Hawa mapacha wa kariakoo (sunche na kapeto)
Mashabiki wasibeze na kuzani wanaenda kukutana na mteremko (kitonga)

*Asec Mimosa niliwatazama Asec Mimosa kocha wao anacheza kimkakati hii timu ndiyo inaweza kuwa neema endapo wataheshimiwa na Kama Yanga watakutana nao lolote linaweza kutokea maana hata Asec siyo wanyonge kabisa.

Imeandikwa na NALIA NGWENA
Tuendelee kuziombea timu zetu zipige hatua na taifa letu liheshimike katika nyanja za michezo.
 
Petro Atletico de Luanda ni giant wa soka la vilabu Afrika. Wamekuwa wakiingia robo fainali mpaka just fainali CAF champions League. Sasa unaposema ni new comer means hujui mpira
UNATAKA KUSEMA YANGA HII HATUA YA ROBO HAWAJAFIKA TOKA WAANZE ??

HAO PERO DE LUANDA USIIONGELEE KAMA WALIVYOKUA HAPO MWANZO MZEE SAFARI HII NI BALAA WAMEJIPANGA.
 
Petro Atletico de Luanda ni giant wa soka la vilabu Afrika. Wamekuwa wakiingia robo fainali mpaka just fainali CAF champions League. Sasa unaposema ni new comer means hujui mpira
UNAPOONGELEA KUFIKA FAINALI HATA SIMBA SC NAO WALISHAWAHI KUCHEZA FAINALI DHIDI YA ABJANI YA HUKO IVORY COAST KAMA WENYEWE WANAVYODAI.
 
Mkuu tuongee ukweli, hakuna mtu mwepesi ktk hii hatua kama Simba na Asec.

Yeyote atakayepangwa dhidi ya Simba au Asec, nje ya Mamelod na Al Ahly, ni wazi kwamba amepewa mteremko kwenda Nusu.

Wale Asec wakirudi kucheza tena na timu za Tanzania hatua ya robo, hawezi kuchukua ushindi kwa Mkapa wala kule kwao, hasa hasa iwe dhidi ya Yanga.
 
Na ndiyo maana nilisema kuwa kidogo Asec tunaweza kukomaa nae lakini hao wengine tunajipa matumaini tu.
 
Mpira wetu unahitaji serious uwekezaji sio hao wapumbavu akina Mo??????

Mo ni chupli sana
Juzi qmeropoka kuwa ameinunua simba.

Kwa wawekezaji kama hao timu zetu mwisho wake ni Robo tu.
 
UNAFIKILI PETRO DE LUANDA NI JWANENG GALAXY
Anadhani ni zile timu famba famba zilizokuwa kwenye kundi lao, siku zote timu yenye ulinzi imara itakupa makombe na timu yenye washambuliaji imara watakufanya ushinde mechi, Petro atretico wako vizuri sana kwenye backline yao wakikupigia kimoja ndio bye bye imeisha iyo!
 
UNATAKA KUSEMA YANGA HII HATUA YA ROBO HAWAJAFIKA TOKA WAANZE ??

HAO PERO DE LUANDA USIIONGELEE KAMA WALIVYOKUA HAPO MWANZO MZEE SAFARI HII NI BALAA WAMEJIPANGA.
Ndiyo
 
Attachments

  • Screenshot_2024-03-03-21-13-05-923~2.jpeg
    Screenshot_2024-03-03-21-13-05-923~2.jpeg
    173.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom