sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Wamasai wameishi Ngorongoro maelfu ya miaka, wameondoshwa ili wapishe wageni, Mwaka 2100 Mmasai akirudi Ngorongoro wageni wana haki ya kumuita mmassai ni mvamizi?

ndivyo ilivyo nao waisrael walivamiwa wakahamishiwa ulaya kimabavu, Ardhi ya Israel wakahamia wapalestina lakini baada ya miaka kupita waisrael wakarudi nyumbani kwao ila cha ajabu wapalestina wakawa wabishi kwamba Israel ni nchi yao, wanatoa wapi jeuri hii?

Huwa naona Wapalestina wengine wanatumia hati za viwanja walivyouziwa kipindi waisrael wamehamishwa kimabavu kwenda ulaya,

Ni sawa na wamasai wakirudi Ngorngoro mwaka 2100 kisha wageni hawa waliopewa Ngorongoro waanze kupinga kwa kuonyesha hati walizopewa na serikali iliyowatoa wamasai kinguvu Ngorongoro.
 
Una hoja usikilizwe..
Tuchukulie scenario nyingine

Ingekuwa vipi Dubai ingevamiwa hapo zamani na waarabu wahamishwe kinguvu kwenda ulaya kisha hapo Dubai wangehamia waisrael.

Baada ya miaka kwenda Waarabu wanataka kurudi kwao Dubai wanakuta kuna waisrael waliohamia na wengine wana hati za ardhi walizouziwa na wavamizi walioteka Dubai hapo zamani, Je waisrael wangewaambia waarabu Dubai ni yao Pangetosha kweli?
 
Soma historia wacha kuleta majibu rahisi kwa maswali magumu.Soma kitabu kinachoitwa The Palestine /Israel Conflict ili uelewe kiini cha mgogoro huu wa Mashariki ya Kati.
 
ni propaganda tu, ukweli ni kwamba waisrael wana kwao na kwao ni Israel
 
Wamasai wameiishi Ngorongoro maelfu ya miaka, wameondoshwa ili wapishe wageni, Mwaka 2100 Mmasai akirudi Ngorongoro wageni wana haki ya kumuita mmassai ni mvamizi??

ndivyo ilivyo nao waisrael walivamiwa wakahamishiwa ulaya kimabavu, Ardhi ya Israel wakahamia wapalestina lakini baada ya miaka kupita waisrael wakarudi nyumbani kwao ila cha ajabu wapalestina wakawa wabishi kwamba Israel ni nchi yao, wanatoa wapi jeuri hii ?

Huwa naona wapalesrina wengine wanatumia hati za viwanja walivyouziwa kipindi waisrael wamehamishwa kimabavu kwenda ulaya, Ni sawa na wamasai wakirudi Ngorngoro mwaka 2100 kisha wageni hawa waliopewa Ngorongoro waanze kupinga kwa kuonyesha hati walizopewa na serikali iliyowatoa wamasai kinguvu Ngorongoro.
Hapana itakubidi uende tena darasani ukapitie uzuri historia.

Eneo la Gaza lilikuwa chini ya waingereza na ni wao mwaka 1947 walikuja na mpango wa kuligawa ili upande mwingine wapewe Waisraeli, mpango uloitwa UN partition Plan for British Palestine.

Gaza ilikuwa chini ya uangalizi wa Waingereza kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na uangalizi huo ulipoisha mwaka 1948 ndo wakaanza kugawa eneo hilo kwa pande mbili, wa kiyahudi "Jewish State" na wa kiarabu "Arab State".

Leo ni miaka 75 tangia taifa la Israeli litengenezwe mwaka 1948.

Waisraeli walokuwa nje nao wakapelekwa pale Palestrina na wakatafutiwa eneo ambapo wenyeji wenyewe Wapalestina wakaondolewa na wengine kupotezwa.

Wapalestina wakaja na vita ya kwanza kubwa ya mwaka 1967 (miaka 55 imepita) iloitwa Six Day War ambapo waisraeli walinogewa na ardhi walopewa ya Ukanda wa Gaza na kuanza kuchukua sehemu ya ardhi upande wa Ukanda wa Magharibi au West Bank.

Mwaka 2006 kulikuwa na vita ingine kati ya Waisraeli na Wapalestina ambapo Unada wa Gaza ulifungwa na wapalestina wengi kuuawa kwa mabomu na kushambuliwa kwa ndege za kivita.

Sasa hii yalingana kidogo na mfano wako wa wageni kupewa ardhi ya Ngorongoro na wamasai kuhamishwa kinguvu (hatufahamu kama wengi wameuawa kama wapalestina au la).

Lakini wageni hao hawajapewa ardhi ya Ngorongoro ili kuigeuza ni kamji kadogo ka Ngorongoro ingawa kwa dunia hii ya leo twaweza kuja shangaa siku moja tukaiona Ngorongoro imekuwa mji kamili wenye kila kitu na ni wale wenye pesa tu ndo wapaswa kuingia hapo.

Haya yote hufanywa na serikali dhalimu ambazo hazajali haki za binadamu na misingi yake.
 
ni propaganda tu, ukweli ni kwamba waisrael wana kwao na kwao ni Israel
Hivyo vitabu vinavyoandikwa na waarabu Koko ku justfy uhuni wanaomfanyia Taifa teule la Izrael? Kitabu Cha rejea ni biblia hakuna kingine labda tora ya wayahudi zaidi ya hapo ni propaganda za kijinga
 
Kwanza mimi siamini wale Israeli taifa teule la Mungu ndio hawa wa mashariki ya kati.
wanawezaje kuruhusu ushoga wakati wao ni taifa la Mungu!
Biblia inaonyesha hata enzi za manabii Kuna wakati walikuwa wanaabudu miungu ya kigeni. Unajua kisa cha nabii Eliya na manabii wa Baali? Kama waliweza kufanya hayo enzi hizo, watashindwa la ushoga leo?

Halafu Mkuu, hivi yanayoendelea pale kwenye kitovu cha dini yako Saudi Arabia, unaona ni sawa? Mbona Kuna haram nyingi sana zinafanyika pale kwenye nchi palipo na Kaaba?
 
Soma historia wacha kuleta majibu rahisi kwa maswali magumu.Soma kitabu kinachoitwa The Palestine /Israel Conflict ili uelewe kiini cha mgogoro huu wa Mashariki ya Kati.
Huwezi japo kukisummerize hicho kitabu hapa na sisi wavivu wa kufunua kurasa tukaambulia chochote kitu?
 
Wamasai wameishi Ngorongoro maelfu ya miaka, wameondoshwa ili wapishe wageni, Mwaka 2100 Mmasai akirudi Ngorongoro wageni wana haki ya kumuita mmassai ni mvamizi?

ndivyo ilivyo nao waisrael walivamiwa wakahamishiwa ulaya kimabavu, Ardhi ya Israel wakahamia wapalestina lakini baada ya miaka kupita waisrael wakarudi nyumbani kwao ila cha ajabu wapalestina wakawa wabishi kwamba Israel ni nchi yao, wanatoa wapi jeuri hii?

Huwa naona Wapalestina wengine wanatumia hati za viwanja walivyouziwa kipindi waisrael wamehamishwa kimabavu kwenda ulaya,

Ni sawa na wamasai wakirudi Ngorngoro mwaka 2100 kisha wageni hawa waliopewa Ngorongoro waanze kupinga kwa kuonyesha hati walizopewa na serikali iliyowatoa wamasai kinguvu Ngorongoro.
First of all unapaswa kurudi nyuma kabisa kwenye biblia, kitabu kilichoelezea vizuri zaidi kuhusu historia hii. Abraham/Ibrahim anatambulika kama ndie baba wa taifa la Israel maana yeye ndie baba wa Ishmael na Isaka ambaye kupitia yeye walizaliwa watoto kumi na wawili na hayo ndio makabila kumi na mawili ya Israel, sasa huyu Mzee Abrahamu hakuzaliwa Israel ila alizaliwa Iraq (middle east) na baada ya kuishi kwao kwa kipindi fulani Mungu alimwambia aondoke nchi hiyo aende kwenye nchi atakayo muonesha, mzee akafunga virago vyake hadi kwenye eneo la Israel huo ya sasa na pale aliwakuta watu wakiishi manaake n wenyeji wa pale mzee akaendelea na maisha.

Baada ya kipindi kirefu kupita, Israel walikuja wakawa watumwa Misri huko kwa mafarao kina Mohamed salah na waliishi huko kwa miaka 430, sasa muda anavokuja kuwakomboa na kuwarudisha nyumbani walikuta eneo lile linamilikiwa na makabila mengine na ndipo Mungu alimteua joshua kuwaongoza Israel kuconqure maeneo.

Sasa unatakiwa kujua wale waliokutwa kwenye eneo lile hawakuwa wanajua linamilikiwa na watu gani na pia eneo lile limekaliwa na kutumika na mataifa na makabila mbalimbali sasa shida n kuwa wapalestina wanaona lile n eneo lao na wanahaki ya kuishi pale na waisraeli pia wanatumia historia kuwa lile eneo ni lao na mtafaruku ni mkubwa sana juu ya ardhi ile na ndio maana British aliamua kutenganisha ardhi ile itumike na wote mwaka 1948. Ila mtafaruku bado ni mkubwa sana, na hakuna mwanaintelijensia yeyote atakaeweza kusolve issue ile.
 
Hakukusa na israel kbla ya 1940's...hilo ni taifa lililoanzishwa na likapewa Jina ili kuleta mgogoro ili watu wapate faida ya mgogoro huo...
Kama weww ulivyodanganywa kipindi kile kuwa Iddi amini kachokoza Tanzania 😀😀
 
Hakuna wala haijwahi kuwepo nchi inayoitwa israel kabla ya mwaka 1948.

Tusidanganyane.
 
Wamasai wameishi Ngorongoro maelfu ya miaka, wameondoshwa ili wapishe wageni, Mwaka 2100 Mmasai akirudi Ngorongoro wageni wana haki ya kumuita mmassai ni mvamizi?

ndivyo ilivyo nao waisrael walivamiwa wakahamishiwa ulaya kimabavu, Ardhi ya Israel wakahamia wapalestina lakini baada ya miaka kupita waisrael wakarudi nyumbani kwao ila cha ajabu wapalestina wakawa wabishi kwamba Israel ni nchi yao, wanatoa wapi jeuri hii?

Huwa naona Wapalestina wengine wanatumia hati za viwanja walivyouziwa kipindi waisrael wamehamishwa kimabavu kwenda ulaya,

Ni sawa na wamasai wakirudi Ngorngoro mwaka 2100 kisha wageni hawa waliopewa Ngorongoro waanze kupinga kwa kuonyesha hati walizopewa na serikali iliyowatoa wamasai kinguvu Ngorongoro.
Ipo siku wamasai watarudi tu msidhani yeisha
 
Soma historia wacha kuleta majibu rahisi kwa maswali magumu.Soma kitabu kinachoitwa The Palestine /Israel Conflict ili uelewe kiini cha mgogoro huu wa Mashariki ya Kati.
Kwann tukiamini hicho kitabu?
 
Wamasai wameishi Ngorongoro maelfu ya miaka, wameondoshwa ili wapishe wageni, Mwaka 2100 Mmasai akirudi Ngorongoro wageni wana haki ya kumuita mmassai ni mvamizi?

ndivyo ilivyo nao waisrael walivamiwa wakahamishiwa ulaya kimabavu, Ardhi ya Israel wakahamia wapalestina lakini baada ya miaka kupita waisrael wakarudi nyumbani kwao ila cha ajabu wapalestina wakawa wabishi kwamba Israel ni nchi yao, wanatoa wapi jeuri hii?

Huwa naona Wapalestina wengine wanatumia hati za viwanja walivyouziwa kipindi waisrael wamehamishwa kimabavu kwenda ulaya,

Ni sawa na wamasai wakirudi Ngorngoro mwaka 2100 kisha wageni hawa waliopewa Ngorongoro waanze kupinga kwa kuonyesha hati walizopewa na serikali iliyowatoa wamasai kinguvu Ngorongoro.
Mfano sahihi kabisa na mweoesi kuuelewa ni kama uji kwa mwenye mapengo.
 
Hivyo vitabu vinavyoandikwa na waarabu Koko ku justfy uhuni wanaomfanyia Taifa teule la Izrael? Kitabu Cha rejea ni biblia hakuna kingine labda tora ya wayahudi zaidi ya hapo ni propaganda za kijinga
Kwani ushoga ulianza lini?
Sodoma na Gomora ziliadhibiwa kwasababu gani?
 
Tuchukulie scenario nyingine

Ingekuwa vipi Dubai ingevamiwa hapo zamani na waarabu wahamishwe kinguvu kwenda ulaya kisha hapo Dubai wangehamia waisrael.

Baada ya miaka kwenda Waarabu wanataka kurudi kwao Dubai wanakuta kuna waisrael waliohamia na wengine wana hati za ardhi walizouziwa na wavamizi walioteka Dubai hapo zamani, Je waisrael wangewaambia waarabu Dubai ni yao Pangetosha kweli?
Wajua Saudia Arabia nayo ilikuwa ya Israel kichumi Mudy mullister aliua wote na akapiga marufuku non Muslim kukanyaga Madina.. hata kisa cha Waislam Ijumaa kuwa siku ya lazima kuswali sababu ni Wayahudi walikuwa wanafunga maduka yao Ijumaa jioni Sabato inapoingia. So siku ya Ijumaa kwa Muslim wakawa wanafurika madukani kwa wayahudi ili jumamosi wasije kufa kwa njaa maana hakuna kunachouzwa wala kununuliwa... aya ya lazima ikaja kuswali ijumaa so wanaenda madukani kishwa kuswali then madukani..
 
First of all unapaswa kurudi nyuma kabisa kwenye biblia, kitabu kilichoelezea vizuri zaidi kuhusu historia hii. Abraham/Ibrahim anatambulika kama ndie baba wa taifa la Israel maana yeye ndie baba wa Ishmael na Isaka ambaye kupitia yeye walizaliwa watoto kumi na wawili na hayo ndio makabila kumi na mawili ya Israel, sasa huyu Mzee Abrahamu hakuzaliwa Israel ila alizaliwa Iraq (middle east) na baada ya kuishi kwao kwa kipindi fulani Mungu alimwambia aondoke nchi hiyo aende kwenye nchi atakayo muonesha, mzee akafunga virago vyake hadi kwenye eneo la Israel huo ya sasa na pale aliwakuta watu wakiishi manaake n wenyeji wa pale mzee akaendelea na maisha.

Baada ya kipindi kirefu kupita, Israel walikuja wakawa watumwa Misri huko kwa mafarao kina Mohamed salah na waliishi huko kwa miaka 430, sasa muda anavokuja kuwakomboa na kuwarudisha nyumbani walikuta eneo lile linamilikiwa na makabila mengine na ndipo Mungu alimteua joshua kuwaongoza Israel kuconqure maeneo.

Sasa unatakiwa kujua wale waliokutwa kwenye eneo lile hawakuwa wanajua linamilikiwa na watu gani na pia eneo lile limekaliwa na kutumika na mataifa na makabila mbalimbali sasa shida n kuwa wapalestina wanaona lile n eneo lao na wanahaki ya kuishi pale na waisraeli pia wanatumia historia kuwa lile eneo ni lao na mtafaruku ni mkubwa sana juu ya ardhi ile na ndio maana British aliamua kutenganisha ardhi ile itumike na wote mwaka 1948. Ila mtafaruku bado ni mkubwa sana, na hakuna mwanaintelijensia yeyote atakaeweza kusolve issue ile.
Acha stories za uongo, hao waisrael wa sasa sio hao mnaowasoma ktk biblia.

Nikisema uthibitishe utashindwa.

Ibrahimu hakuishi iraq wala middle east, nikisema uthibitishe pia utashindwa

Tatu: katika kila tukio lazima liwe na ushahidi wa uwepo wake kupitia mabaki, nakala+makala za kihistoria zinazoelezea jambo hilo, sayansi ya kupima uwepo wa jambo hilo/kiumbe huyo kupitia vipimo vya vinasaba na muda wa kuishi kwa kiumbe hicho(carbon 14).

Sasa kwa kutumia shahidi hizi hakuna Proof yoyote inayoonesha huyo ibrahimu aliwahi kuwepo zaid ya stories za biblia, na hapa ndipo hao wayahudi wenu wa uongo walishindwa kujitetea kuwa hiyo ardhi ni urithi kutoka kwa ibrahimu, maana kihistoria hakuna ushahid kuwa kuna mtu dunian aliwai kuitwa ibrahimu au mwenye hayo matukio yafananayo na ibrahimu kuishi iyo ardhi ya palestina.

Pia hao wayahudi wa uongo hawana ushahidi wa kuwepo ardhi hiyo maana hawana vinasaba vinavyoshahabiana na jamii ya eneo hilo, ni sawa na kusema umchukue msukuma leo hii umpeleke ulaya nchi ya sweeden alafu useme ni ardhi yake, wakati tukimpima msukuma huyo kimila+kiutamaduni hafananii na wenyeji wa maeneo hayo wala vinasaba vyake havimatch na majiran wa eneo hilo,lkn ukimchukua mtu wa norway anaweza kufanana kimila na tamaduni na watu wa sweeden why? Sababu ndio asili yake mpaka vinasaba watafanana, so why hao waisrael wenu hawana ushahidi wowote unaowasapoti wao kuwa wamiliki wa hiyo ardhi.

Mkisingizia sjui wayahudi hao hawafanani na jamii za hapo uarabuni sababu ya kukaa nje ya ardhi hiyo kwa muda mrefu basi tutawaletea ushahidi wenye mfano wa ''black Americans" ambao walichukuliwa utumwa kutokea afrika imepita mamia ya miaka lkn leo hii ukiwapima Vinasaba vyao vinafanana na jamii za watu wa maeneo ya afrika kuonesha kuwa huku ndiko asili yao, ila hao wayahudi wenu wa uongo wanakosa sifa ya umiliki ardhi kwa njia ya (1)kisayansi, (2)kihistoria mpka (3)kijamii zaidi tu ya udicteta wa nduguzo wazungu kuwaweka hapo kinguvu.

Amkeni enyi wapumbavu, mtaamini ujinga mpaka lini.
 
Back
Top Bottom