Tuwaite watoto wetu majina ya asili

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Siku hizi imekuwa kawaida watoto kuitwa majina kigeni kama Joyce, Jocktan, Mary,John,Abdallah,Mohammed, Yusuphu huku tukiacha majina yetu ya asili yaliyotumiwa na wazazi wetu, haiwezekani nimetembelea shule nyingi unakuta mtoto anatumia majina yote ya kigeni mfano Michael John, Joseph tunaacha majina ya asili yetu yanapotea huku tukiendelea kutukuza majina ya kizungu.

Hakikisha mtoto anatumia jina la asili la ukoo wako kwa kufanya hivyo tutazidi kudumisha majina ya kiafrika yanayopotea kwa kasi vile vile tuhakikishe watoto wetu wanafahamu lugha za asili kama Kikurya, Kisukuma, Kinyakyusa, Kinyamwezi sio mtoto anakuwa mpaka anafika mkubwa hata hajui lugha yake ya asili pelekeni watoto wakakae na bibi zao hasa nyakati za likizo wakajifunze lugha na ni vizuri kuwapeleka wakiwa wadogo zaidi maana itakuwa rahisi kushika lugha.
 
Ungeanza kutaja wako wana majina gani au ukipata mtoto utamuita nani?
 
Hakuna cha asili wala nini cha muhimu ni jina lenye maana nzuri basi.
 
Haya majina ya Asili ni Nuksi.
Kiranga ni jina lenye asili ya Kizaramo na Maana yake ni NYEGE!

Sasa vipi Mtu amuite mwanae "Nyege"?
Inaskitisha sana.

Kama hayo majina ya asili ni nuksi na wewe ukazaliwa na wazazi wenye nuksi maana walikuwa na majina ya asili basi utakuwa na nuksi pia.
 
Kama hayo majina ya asili ni nuksi na wewe ukazaliwa na wazazi wenye nuksi maana walikuwa na majina ya asili basi utakuwa na nuksi pia.

Molembe kwa Watu wa Ujiji kigoma maana yake Jivi la mwisho.
Sasa mkuu nikikuita Jivi la Mwisho mtaani si utaanza kirusha ngumi au?

Chunguzeni majina yenu kabla ya kuyatumia. Hata yule Matola hajajua mpaka leo kuwa Matola kwa Kihehe ni Vinyweleo vya chini ya Makende!
Ni hatari sana haya majina.
 
Last edited by a moderator:
Kama hayo majina ya asili ni nuksi na wewe ukazaliwa na wazazi wenye nuksi maana walikuwa na majina ya asili basi utakuwa na nuksi pia.

suala ni kutokurudia kosa. Mzazi alikupa jina lenye maana mbaya sasa wewe usirudie hayo makosa,tupa mbali asili kama imekosa majina mazuri bora nimpe ya kizungu.
 
Majina ya asili kiukweli sio matamu kuyatamka ukilinganisha na ya kigeni hasa kutoka ulaya
 
Na hizi tamthilia za Kilatino na Kizungu ndio zinazidi kuzalisha majina mapya ya watoto, hatari. Kuna binamu yangu ana watoto wawili mmoja anamwita Bianca; itokee bahati mbaya jina la baba aitwe Brian hapo ndio utachoka pale mtoto anaitwa Bianca Brian!

Rafiki yangu mmoja nikisoma naye Chuo alikuwa anaitwa Fred Angels. Baada ya kuhitimu alipata kazi na akapata trip kikazi kwenda Afrika Kusini. Anasema akamkuta mwenyeji aliyekuja kumpokea ana bango limeandikwa jina la mgeni 'Fred Angles'; bahati mbaya yule Mwenyekiti aliyetumwa kumpokea alikuwa Mzungu, jamaa anasema ilikuwa kazi kubwa kumshawishi mwenyeji wake kuwa yeye (Mtanzania mweusi) ndiye Fred Angles!

Jamaa aliporudi akaamua kuliondoa jina Angles na kuweka la ukoo wao la Kinyakyusa!

Vv
 
Back
Top Bottom