Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,869
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity stage iliwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012 mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Band nyingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover.

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?

Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?

China wa China...?
Shaibu Mapajero....?

Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?


Note of Appreciation.
wakati naandika huu uzi sikufikiria kama ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.
 
Huyo Abdul Mteketa alikuwa Mbunge wa Kilombero, Mkoani Morogoro na Sasa ni marehemu baada ya kuugua sana na mwisho wake aliishiwa mpaka alikosa pesa ya matibabu pale Muhimbili na kuomba msaada kwa mh.hayati JPM.

Huyo Charles Mtawali ni tajiri mmoja hivi aliwika na mpaka sasa nafikiri yuko na pesa maana alikuwa anaishi Kinondoni Stereo aliwahi kununua mtaa mzima pale,na mle ndani kwake parking ukiingia ilikuwa Kama yard magari ya kifahari akirudi ama mkewe akirudi ilikuwa hatumii gari ile ambayo amerudi nayo anatoka na nyingine.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna huyu wanamwita too much money NI Nani?ndo Fred vunjabei ama?
Huyo ni wa kizazi cha sasa cha machawa.

ni aina ya vijana ambao majina yao yamefahamika kwa msaada mkubwa wa social media hususani instagram.

bila mitandao ya kijamii, hakuna ambaye angewafahamu.

Wakati akina Msofe wanasumbua mjini, yeye alikuwa primary may be.
 
Wakati Mustahiki Meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama anatuchezesha Dar es salaam kibinda nkoyi ndani ya Silent in Mwenge ulikuwa darasa la ngapi?

Unamjuwa Joseph Rwegasira?

Hao wote nawajua kaka, wengine nimeacha kuwataja ili nitoe nafasi kwa wana JF kufunguka.

Mzee Rwegasira namkumbuka sana, alikuwa mmiliki wa club ya silent inn, baadae akaokoka na kuachana na biashara za masuala ya burudani.
 
awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. itabidi msome kimya kimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

kwa uchache tu, band zilizotamba ni fm academia, akudo impact, twanga pepeta na diamond musica. zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

umuarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.
kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa john young millionaire muzee ya range rover.

haya twende kazi:
Pedeshee Mychoisi na Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko mbeya, watu wa mbeya mtatusaidia.

Braza K na Tunduma:
watu wa tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya mikocheni barabara ya rose garden. back on those days she was very pretty. kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnana:
bika shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV. baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana.sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. fm academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
alikuwa mmiliki wa band ya daimond musica kwa kuwezeshwa na mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages. watu wa zamani wanaelewa. juddy alikuwa mrembo si kitoto. kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
sina haja ya kumuelezea , ni mtu maarufu wa nyakati zote. wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Billgate Muzamil Katunzi:
Christian bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la muzamir katunzi. i don't know him personally, but it's told he was financially very successful.

Papaa Msope Chuma cha Reli.
sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa papaa msofe. itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana. halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
ni marehemu kwa sasa. huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya Fm Academia. nilikuwa namfahamu personally.licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer ktk Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi mpya za gari mtaa wa agrey kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiriwa kwa jina la general supply. ktk biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

pedeshee David Kabunga:
sifahamu alikuwa ni nani. jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Ali Kileo:
he was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe Big Boss:
anafahamika vizuri. jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Amos Makalla mzee wa Mvomero:
kwa sasa ni RC wa dar. jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: anafahamika vizuri, wajanja wa wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk mkoa wa morogoro. sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za lumumba.

Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
?/
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy nyamalonda mzee wa pamba...
?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Hahahaha umenikumbusha enzi za best yangu Amos Makalla enzi hizo mweka hazina wa CCM!!

Makalla ana bahati ya kuzaliwa niishie hapo!!
 
Back
Top Bottom