Vyombo vingi vya habari vimekuwa vikipokea pongezi za wananchi kutoka kila pembe ya Tanzania wakiunga mkono hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati akizindua Bunge la 11 Ijumaa iliyopita.
Walio wengi wameguswa na hotuba hiyo, wakisema inatoa matumaini makubwa kwa Watanzania na inathibitisha kwamba Rais Magufuli, kama alivyosema mwenyewe, hakutoa ahadi zilizolenga kujipatia kura tu wakati wa kampeni, bali kuhakikisha anazitekeleza kwa vitendo kwa faida ya Watanzania.
Hata hivyo, tunaona katika mitandao ya kijamii na hata kwenye vyombo vya habari baadhi ya Watanzania wachache wakionekana kutomuunga mkono Rais, na wengine wakionekana wazi kuwaunga mkono wabunge waliofanya kitendo cha aibu Ijumaa iliyopita cha kupiga kelele, kuzomea na kususa hotuba ya Rais Magufuli.
Baadhi ya vitabu vya dini vinafundisha kwamba binadamu ana njia mbili; ama ile anayoitaka Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyemuumba au ya shetani. Ni kwa muktadha huo, tunaungana na kauli ya Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyekaririwa na vyombo vya habari likiwemo gazeti hili jana, akisema kwamba mtu yeyote anayempinga Rais Magufuli, maana yake ni kwamba atakuwa unaunga mkono mafisadi, wala rushwa na wabadhirifu.
Katika maoni yake, Zitto alisema mtu anayepinga ufisadi, uzembe, ubadhirifu, uvivu na rushwa hawezi kumzomea Rais Magufuli au kumpinga kwa namna moja au nyingine badala ya kumuunga mkono. Zitto alifafanua kwamba mtu wa aina hiyo kwa hali yoyote atakuwa ana maslahi binafsi na mafisadi na hataki mabadiliko chanya.
Zitto akaenda mbali kwa kusema kwamba huu ndio wakati ambao Watanzania watawajua watu ambao wapo upande wa mafisadi au upande wa wananchi. Hata sisi tunajiuliza kwamba wanaompinga Magufuli wanataka nini hasa?
Je, wanataka tuendelee kuwa taifa ambalo matajiri hawalipi kodi isipokuwa wanaokamuliwa zaidi ni watu masikini, wenye kipato cha chini na wafanyakazi? Je, wanataka watu waliouziwa viwanda na mashamba waendelee kuyahodhi hata kama wameshindwa kuyaendeleza kwa mujibu wa mikataba?
Yaani wanachukia dhana nzima ya kufufua viwanda vya zamani na kuanzisha vipaya? Je, wanataka tuendelee na watendaji serikalini wasiowajibika ipasavyo ambao wamegeuza sekta ya umma kuwa sehemu ya kuchuma badala ya kuitumikia kwa faida ya wananchi wote?
Wanakataa asipambane na wala rushwa, wanataka alee wazembe katika utumishi wa umma na pia wanataka asizibe mianya ya uchakachuaji wa fedha za umma? Zitto, licha ya kuwa kiongozi wa chama cha upinzani, alisema uzalendo unamtaka kumuunga mkono Rais katika vita dhidi ya ufisadi na kusimamia ustawi wa watanzania, hususan wanyonge. Na sisi swali letu kwa wanaoonekana kutokuwa upande wa rais ni hili. Je, uzalendo wao ni kuunga mkono kitu gani?
Baadhi ya watu hawa, kwa miaka nenda rudi wamekuwa wakijinadi kwamba wanachukia ufisadi. Je, sasa wanaposhindwa kuunga mkono rais anayeahidi kupambana na ufisadi tuwaeleweje?
SOURCE: Habari leo online