Tuwache kula ugali

Jamani ugali iwe wa mahindi au wowote mwengine ni mtamu,lakini kwa kweli ugali wa mahindi ambao wengine huuita sembe au sima ni vyema kujizoesha kuwachana nao.Kabla kusikia hoja zangu nyinyi mwasemaje?.


Another thread from one of the great thinkers of this forum. Kweli JF imefulia!!!!
 
masoud,hivi umewaza nini mpaka kutoa hii hoja? labda kidogo wahaya wanaweza wakakuelewa ila sio wasukuma,wakiacha ugali watakula nini kama chakula cha asili?

Vyakula maarufu vya Wachina ni mchele, ngano, shairi, uwele, mtama, na jamii ya viazi.Kwa upande wa vitoweo wanakula vitu kama vile mapezi ya papa, mwani, vyura,nyoka,nguruwe na hata nyama za mbwa na paka.
Katika upishi wa vyakula vyao; Wachina huongozwa na mafunzo ya kiroho kwa kuleta uwiyano kati ya Yin (ubaridi) na Yang (ujoto).Kwa upande mwengine upishi huambatana na kuleta uwiyano wa rangi na msokotano(texture) wa chakula chenyewe.
Wahindi wao hupendelea kula mchele,ngano,shairi na aina nyenginezo za nafaka kama vile dengu.Kwa ujumla vyakula vya wahindi hutawaliwa na viungo mfano ukwaju ,mabilingani,pilipili na vitango.Ni nadra sana vyakula vya kihindi kukosa tangawizi na manjano.Harufu ya chakula ni kitu muhimu katika vyakula vyao.
Tukiwachana na vitoweo vya wachina ambavyo kwa imani ya kundi mojawapo la watanzania vina utata,na ambavyo kutokana na wingi wa mifugo iliyopo havina ulazima kuvitumia, ni kuwa kwa wachina na wahindi, mahindi ambayo hutengeneza ugali si zao muhimu la chakula kwao.
 
napata picha ya hii mada mada imetulia tusitegemee ugali pekee

Mpaka hapa tumeona kuwa nchi zenye watu wengi zaidi duniani sizo zenye njaa.Vile vile nchi hizo hazili ugali utokanao na mahindi.
Sasa basi tuone kilimo cha mahindi kulinganisha na ukulima wa mazao mengine.
 
Kwa uzoefu nimegundua ya kuwa kile chakula mtu anachokula wakati wa utoto wake kuelekea ukubwa katika hali ya raha,yaani katika hali ya kupata na kuridhika kimazingira alipo ,hicho ndicho chakula atakachokiona ni kitamu kuliko vyote duniani.Hata ukimpeleka nchi gani basi bado atakitamani chakula hicho.
Watu huweza kuzoea vyakula kama viwili hivi kimoja zaidi na kingine chini yake.Wale waliozoea wali na kuku wataendelea hivyo mpaka uzeeni.Wa ndizi na muhogo nao ni hivyo hivyo,na kadhalika.Wazungu hakuna chakula bora kama viazi mbatata.Waarabu ni jamii ya mikate na nyama.
Wengi wetu katika Afrika tunapenda ugali hasa wa mahindi,wengine huita ugali wa sembe na majina mengineyo.Hata wakiwa maraisi na mawaziri wakifika ugenini huuweweseka ugali.
Mimi ndio wale wa wali kwa kuku kama chakula kikuu cha siku.Inapokuwa si wakati wa njaa na ukame, huna cha kuniambia mbele ya chakula hiki.Upishi wake huweza kutofautiana.Kwa bahati niko karibu na mafundi wa upishi wake.Ningependa watu wote wajizoeshe chakula changu cha wali,hata ikiwa ni kwa samaki.
Vyakula vyengine ninavyopendelea kula kwa ajili ya kifungua kinywa na chai ya usiku, ni jamii ya mikate na mboga mboga za majani zilizotiwa viungo mbali mbali.Nikijiweza zaidi ni supu ya mbuzi inayonukia viungo vya kiasili vya kiEshia.
Ufanisi wa sera ya KILIMO KWANZA ni wa mashaka iwapo hatutobadili vipaumbele vya vyakula tunavyokula.Bahati mbaya sera hiyo katika nguzo yake ya 4 ya mpango wa utekelezaji, bado inataja mahindi ambayo hutoa ugali, kama zao la mwanzo katika mazao muhimu ya chakula.
Sasa wewe Masoud unachotaka kutuambia ni nini hasa? Mi naona unahangaika tu badala ya kutoa hoja ya kwa nini watu wasile ugali. Halafu unatushauri tule wali kama wewe! Sasa nini hii? Ulichotakiwa kutuambia labda ingekuwa ni kwamba tujifunze kuji-adapt na mazingira mageni pale tunapokuwa mbali na kwetu au pale tunapokuwe hatuwezi kupata vyakula tulivyovizoea. Na kwa hili sidhani kama kuna mtu ameshindwa. Lakini kusema categorically kabisa kwamba watu wasile ugali unashangaza sana Masoud.
 
Aagh achaneni na NGUNA (UGALI) nyieeeee. Ukiwa Morogoro songa Ugali halafu lumangia na kipande cha NGURUKA, mkuu waweza jng'ata. Ukiwa A-town (Arusha) vile vile pika UGALI wako halafu nunua wale samaki wanaokaangwa na akina mama kwenye magenge, wale samaki wanatoka bwawa la nyumba ya Mungu ni balaa tupu. Ukiwa Dar kula ugali na Kipande cha Papa, Kibua au changu wallahi utasahau km kuna kitu chaitwa NYAMA. Ukiwa Nyumbi hii bombi hii (SONGEA) kula Ugali na Dagaa nyasa au samaki wa ziwa nyasa wanaitwa Mbelele au MBASA mamaaaaaaaaaaaaaaaaa usisahau na lidelele (mlenda). Hahaha Ukiwa Sumbawanga kula Ugali kwa NSWA (kumbikumbi) hahahaha mambo hayoo wadau UGALI MTAMU BANA, uwe sembe au dona whatever MAN!!!!!!!!!!!.

Nyongeza:
Ukiwa kanda ya ziwa pata ugali wako kwa Sangara (mbuta), Sato, Mumi (kambale), furu (hasa Ukerewe), Kamogo (Kwa Wajaluo), na Bukoba ongezea senene,
we acha kabisa
 
Semina nyingi na makongamano kuanzia ngazi za kijiji,kitaifa na kimataifa yamefanyika kulalamikia tatizo la kuenea kwa jangwa,ukataji miti na kupunguka kwa misitu.Ukweli ni kuwa suluhisho hawana.
Mashirika ya kimataifa na NGO’s yametumia fursa hiyo kuingiza ajenda zao, mfano wengine wamesema ni lazima programu za kupunguza uzazi zilazimishwe kwa serikali,kubadili aina za umilikaji ardhi na wengine wamesema itolewe mikopo “for Nature”.
Andiko la Yvonne Agyei linasema: Utafiti wa FAO umegundua kuwa kati ya mwaka 1980-1990 misitu katika nchi za tropiki ilipungua kwa hekta 15.4mil ,yaani kasi ya 0.8% ya ardhi yote kwa kila mwaka Ardhi hiyo ni zaidi ya mara 3 ya ukubwa wa Ufaransa .
Hili ni tatizo la dunia kutokana na sababu mbali mbali.Kwa nchi zilizoendelea ni kutokana na biashara ya magogo na ufugaji wa ranchi.Kwa Afrika,zaidi ni kutokana na kilimo na matumizi ya kuni.Asilimia 90 ya watu wa Afrika katika ripoti hii wametajwa kuwa hutumia kuni kwa kupikia.
Ukataji miti na misitu kwa ajili ya kilimo na kwa ajili ya kuni ni karibu sawa kwa sawa.Na kwa kweli sababu hizi zinachangia 60% ya ukataji miti kote duniani.
Mwishoni mwa mwaka 1990 Afrika kwa jumla ilikuwa na hekta milioni 528 za misitu ambazo ni 30% ya misitu yote duniani.Ukataji wake wa misitu ilikuwa ni zaidi ya 0.8%.
Sababu nyingi zimetajwa katika utafiti huo.Ukiangalia na majumuisho ya makongamano mengine,sababu kuu imetajwa kuwa ni ujinga wa watu wa Afrika kuhusiana na miti na misitu. Nimegundua sababu hizo sizo.Tatizo ni aina ya chakula kikuu wanachokula watu wake,yaani Ugali.
 
Mpaka hapo tumeona kuwa nchi za Afrika zinaongoza kwa ukataji miti,sababu kuu ni kwa ajili ya kilimo na kuni.Kila sababu ina mchango karibu sawa na mwenzake.
Kwa Afrika nchi za kusini ya jangwa la sahara zinakata miti kwa zaidi ya 0.8% ambayo ni kasi ya dunia.Maana yake ni kuwa kilimo cha nchi hizi ndicho kinachosababisha ukataji huo wa miti.
Tukiangalia kwamba kilimo kikubwa ni mahindi,hivyo kilimo cha mahindi kinachotupatia ugali ndicho kinacholeta athari hii.
Kwa kila njaa moja inayoondoshwa kwa kula ugali husababisha njaa nyengine kadhaa kwa watu,wanyama na ndege kutokana na ukataji wa miti.
 
Mahindi ni moja ya zao ambalo uotaji wake unahitaji rutuba ya kutosha ili yastawi na hayana uvumilivu na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kutokana na sababu hii wakulima hulazimika kufyeka vichaka vilivyonawiri na kuchoma moto ili wapande mahindi.Hali huwa ya kuridhisha pindi mvua za kutosha zikinyesha.Hata hivyo hali hiyo haidumu kwa muda mrefu,ardhi huchoka na kumlazimu mkulima kufyeka vichaka vyengine.
Angalia hali ya njaa kwa Tanzania.Mara nyingi wale ambao wanatumia ugali zaidi ndio wanaokuwa wa mwanzo kukumbwa na njaa pindi mabadiliko ya hali ya hewa yakiwa ni ukame.Handeni ni mfano mmojawapo.Wanaongoza kwa uchomaji misitu na kwa kukumbwa na njaa mwanzo.
Hii ina maana mpango mzima wa KILIMO KWANZA unaohimiza kilimo cha mahindi hautoondoa njaa kwa watanzani kinyume na kuweka mazingira ya kuiendeleza.
 
nyinyi wanafalsafa mnaongelea ugali au kuna kitu kipo ndani ya ugali

Ndugu yangu Godwine mimi si mwanafalsafa.Hii mada ni msaada wa bure kwa watanzania ili kuondokana na njaa.
Ngoja tuangalie zaidi kilimo cha mahindi yanayotoa ugali tulinganishe na mpunga.
 
Kilimo kama cha mpunga mara nyingi huota sehemu za mabondeni ambako watu na wanyama hawana matumizi nako sana zaidi hicho kilimo.Mahindi lazima yaote kwenye uwanda kwa kukata miti na kuchoma moto.
Ndizi unaweza kulima upenuni ukavuna na kushiba kwa miaka kadhaa.Mahindi ukilima upenuni utakufa njaa.

Baada ya hapa tuone uzuri wa mazao mengine wanayopendelea kulima na kula wenzetu ambako hakuna njaa.
 
ugali,mchele blaah blaaah blaaaaaaaaaaaaaaaaaah blaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah,mpaka njaa inauma,ngoja nikale kiporo changu cha ugali mie.
 
ugali,mchele blaah blaaah blaaaaaaaaaaaaaaaaaah blaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah,mpaka njaa inauma,ngoja nikale kiporo changu cha ugali mie.
Kwa kufupisha hii mada ili imalizike kwa vile wasioelewa wameanza kuchoka;ni kuwa vyakula wanavyokula wachina,wahindi na wengine wasiokumbwa na njaa mara kwa mara baadhi huoteshwa kwenye vieneo vidogo hata kwenye hali ngumu ya hali ya hewa,na kutoa mazao mengi. Jambo hili kwa mahindi ni nadra kutokea.Mazao mengine huota kwenye vivuli vya miti na kwa kutambaa miti wenzao ambayo nayo hutoa mazao yake yenyewe.
Kama takwimu zilivyoonesha hapo kabla,upishi wa ugali unahitaji kuni nyingi kabisa na hauivi vizuri bila kutumia mkaa.Si mara nyingi ugali kupikwa kwenye jiko la gesi.Hii ndiyo sababu kuu ya matumizi makubwa ya makaa Tanzania.
Upishi wa ugali unahitaji mtu awe na afya ndipo aweze kupika.Hii ni kasoro nyengine wakati mtu huhitaji kutayarisha chakula haraka ili aondoe njaa.Hali zote hizi ni tofauti na vyakula vingi viliwavyo na wasiokumbwa na njaa ovyo ovyo.

HIVYO ILI TANZANIA NA AFRIKA ZIONDOKANE NA NJAA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI LAZIMA SERIKALI ZAKE ZIWACHE KUTOA MSISITIZO WA KILIMO CHA MAHINDI,NA ZIWAHIMIZE WATU WAKE KUANZA KULA VYAKULA TOFAUTI TOFAUTI AMBAVYO KILIMO CHAKE NI CHEPESI,VYENYE BARAKA KATIKA MAZAO YAKE NA AMBAVYO UPISHI WAKE NA ULAJI WAKE HAUHITAJI MATUMIZI YA NGUVU NYENGINE ZA ZIADA.
 
Wanao haribu ladha ya JAMII FORUMS ni wana forum wenyewe.
Kisha tukiambiwa kuwa JF imevamiwa tunakuwa wakali.

Unayosema ni kweli kabisa.Watu wasiojua lipi lenye faida na jamii na kujadiliwa wanaharibu ladha ya JF sana.Wamezoea kujadili mambo ya udaku na vitu vya kubuni wakati vitu vya maana na vya kweli kujadiliwa vipo.
Wakati huo huo nimegundua kuwa humu JF great thinkers ni wachache sana.Wengi wao ni washabiki tu.
 
Nafiiri alikuwa na maana kuwa kula ugali wa mahindi uliokobolewa hauna virutumisho mwilini, na kadri tunavyokula huo ugali ndio na uwezo wetu wa kufikiri unavyozidi kupungua matokea yake watu wengi wanakuwa vilaza hivyo kupelekea kuwa na vyeti feki kwa wingi ila mbadala wa kula ugali wa mahindi yaliyokobolewa ni kula dona tena ya mahindi ya njano, ngano isiyokobolewa, ugali wa ulezi, mtama na nyinginezo nafaka ambazo hazijakobolea na kuondolewa virutubisho.

Tukiweza hayo uwezo wetu wa kufikiri na kusahausahau utapungua na hatimaye kutoweka kabisa hivyo mwanafunzi hata akifundishwa darasani atakuwa na kumbukumbu nzuri na mambo ya Tuition, wizi wa paper na mengineyo yafananayo yatatoweka na pengine kwa vizazi vijavyo vinaweza kuwa Taifa bora lisilo na vyeti vya kughushi.
 
Back
Top Bottom