Tuwache kula ugali

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,152
10,862
Jamani ugali iwe wa mahindi au wowote mwengine ni mtamu,lakini kwa kweli ugali wa mahindi ambao wengine huuita sembe au sima ni vyema kujizoesha kuwachana nao.Kabla kusikia hoja zangu nyinyi mwasemaje?.
 
Tuambie basi kwann tuache wengine ni chakula kikuu kwetu!
 
Hatuna usemi!.....!
Ugali ni mzuri sana...Kabla sijaweka hoja zangu, nyinyi mnasemaje?
 
Jamani ugali iwe wa mahindi au wowote mwengine ni mtamu,lakini kwa kweli ugali wa mahindi ambao wengine huuita sembe au sima ni vyema kujizoesha kuwachana nao.Kabla kusikia hoja zangu nyinyi mwasemaje?.

kwa sababu gani tuache kula ugali?
 
Aagh achaneni na NGUNA (UGALI) nyieeeee. Ukiwa Morogoro songa Ugali halafu lumangia na kipande cha NGURUKA, mkuu waweza jng'ata. Ukiwa A-town (Arusha) vile vile pika UGALI wako halafu nunua wale samaki wanaokaangwa na akina mama kwenye magenge, wale samaki wanatoka bwawa la nyumba ya Mungu ni balaa tupu. Ukiwa Dar kula ugali na Kipande cha Papa, Kibua au changu wallahi utasahau km kuna kitu chaitwa NYAMA. Ukiwa Nyumbi hii bombi hii (SONGEA) kula Ugali na Dagaa nyasa au samaki wa ziwa nyasa wanaitwa Mbelele au MBASA mamaaaaaaaaaaaaaaaaa usisahau na lidelele (mlenda). Hahaha Ukiwa Sumbawanga kula Ugali kwa NSWA (kumbikumbi) hahahaha mambo hayoo wadau UGALI MTAMU BANA, uwe sembe au dona whatever MAN!!!!!!!!!!!.
 
Ahhahahaaah mkuu umegusa penyewe, halafu huyu jamaa eti anasema tuachane nao! tule nini sasa wakati ugali ndio chakula chetu kikuu.
 
Sijui aliyeanzisha mada hii alikusudia nini? lakini mimi namuunga mkono kwasababu mhimu za kisanyansi kama nitakavyozieleza hapa. kwanza, vyakula vyote vya nafaka vina kiasi kikubwa cha omega-6 ambayo kitaalamu ikizidi mwilini inasababisha madhara kiafya kama vile magonjwa ya moyo (coronary heart diseases). pili vyakula vya nafaka vilivyokobolewa vina ufungufu wa virutubisho mhimu (km protein, vitamin na madini). Pia kwa watu wenye matatizo ya kisukari, vyakula vya nafaka zilizokobolewa vina ongeza sukari mara dufu mwilini (High glycemic index). kwahiyo naunga mkono ila ni vigumu kuacha kula ugali kwani licha ya kuwa asili yetu bali pia ndio chakula kinachopatikana kwa urahisi. cha msingi ni kula dona, tusione haya maana tunajimaliza wenyewe.
 
masoud,hivi umewaza nini mpaka kutoa hii hoja? labda kidogo wahaya wanaweza wakakuelewa ila sio wasukuma,wakiacha ugali watakula nini kama chakula cha asili?
 
Aagh achaneni na NGUNA (UGALI) nyieeeee. Ukiwa Morogoro songa Ugali halafu lumangia na kipande cha NGURUKA, mkuu waweza jng'ata. Ukiwa A-town (Arusha) vile vile pika UGALI wako halafu nunua wale samaki wanaokaangwa na akina mama kwenye magenge, wale samaki wanatoka bwawa la nyumba ya Mungu ni balaa tupu. Ukiwa Dar kula ugali na Kipande cha Papa, Kibua au changu wallahi utasahau km kuna kitu chaitwa NYAMA. Ukiwa Nyumbi hii bombi hii (SONGEA) kula Ugali na Dagaa nyasa au samaki wa ziwa nyasa wanaitwa Mbelele au MBASA mamaaaaaaaaaaaaaaaaa usisahau na lidelele (mlenda). Hahaha Ukiwa Sumbawanga kula Ugali kwa NSWA (kumbikumbi) hahahaha mambo hayoo wadau UGALI MTAMU BANA, uwe sembe au dona whatever MAN!!!!!!!!!!!.

NGURUKA WEEEH ACHA TU, samaki huyu kajaa mawese na chumvi, natilia shaka kama kweli huyu samaki anavitamini zaidi ya calisium itokanayo na mifupa yake.
 
Nakiri tumeishiwa thread za kuanzisha

Wakati watanzania kibao hawana option ya kula au kutokula ( wao ni njaa kwa kwenda mbele) sisi tunadiscuss kula au kutokula ugali. This is unfair Nguli nakubaliana na wewe kama great thinkers tungefikiria jinsi gani au chakula gani watu wasio na chakula wale.
 
Tuambie basi kwann tuache wengine ni chakula kikuu kwetu!

Kwa uzoefu nimegundua ya kuwa kile chakula mtu anachokula wakati wa utoto wake kuelekea ukubwa katika hali ya raha,yaani katika hali ya kupata na kuridhika kimazingira alipo ,hicho ndicho chakula atakachokiona ni kitamu kuliko vyote duniani.Hata ukimpeleka nchi gani basi bado atakitamani chakula hicho.
Watu huweza kuzoea vyakula kama viwili hivi kimoja zaidi na kingine chini yake.Wale waliozoea wali na kuku wataendelea hivyo mpaka uzeeni.Wa ndizi na muhogo nao ni hivyo hivyo,na kadhalika.Wazungu hakuna chakula bora kama viazi mbatata.Waarabu ni jamii ya mikate na nyama.
Wengi wetu katika Afrika tunapenda ugali hasa wa mahindi,wengine huita ugali wa sembe na majina mengineyo.Hata wakiwa maraisi na mawaziri wakifika ugenini huuweweseka ugali.
Mimi ndio wale wa wali kwa kuku kama chakula kikuu cha siku.Inapokuwa si wakati wa njaa na ukame, huna cha kuniambia mbele ya chakula hiki.Upishi wake huweza kutofautiana.Kwa bahati niko karibu na mafundi wa upishi wake.Ningependa watu wote wajizoeshe chakula changu cha wali,hata ikiwa ni kwa samaki.
Vyakula vyengine ninavyopendelea kula kwa ajili ya kifungua kinywa na chai ya usiku, ni jamii ya mikate na mboga mboga za majani zilizotiwa viungo mbali mbali.Nikijiweza zaidi ni supu ya mbuzi inayonukia viungo vya kiasili vya kiEshia.
Ufanisi wa sera ya KILIMO KWANZA ni wa mashaka iwapo hatutobadili vipaumbele vya vyakula tunavyokula.Bahati mbaya sera hiyo katika nguzo yake ya 4 ya mpango wa utekelezaji, bado inataja mahindi ambayo hutoa ugali, kama zao la mwanzo katika mazao muhimu ya chakula.
 
Ni ushauri wa bure tu! Ugali wa mahindi yaliyokobolewa si mzuri kwani hauna virutubisho. Bora tule dona. Altenatively, tule ugali wa muhogo (kwa wavivu wa kutafuna), au ugali wa mtama (kwa wachumi) huu ukiula mchana utapiga 'lampard' hadi kesho asubuhi....!
 
ugali ndo umetukuza wenzio hadi leo. hata kama kuna vyakula vingine, tusipokula ugali tunaona kama tumelala na njaa. kwanini tuache ugali?
 
ugali ndo umetukuza wenzio hadi leo. hata kama kuna vyakula vingine, tusipokula ugali tunaona kama tumelala na njaa. kwanini tuache ugali?

Mpaka saa 1.32 asubuhi tarehe 14.03.2010 China ilikuwa na watu 1,336,350,000 na India walikuwa 1,178,508,099. Dunia nzima ilikuwa wako 6,895,066,487. Wachina ni 19.63% na India ni 17.31% ya watu wote duniani.Kumbuka nchi hizi ndizo mbili za juu kwa idadi ya watu duniani.Hivi tunavyosoma tarakimu zimebadilika lakini kwa kiwango kidogo sana.
Tanzania kwa makadirio ya UN mpaka siku hiyo ilikuwa ni watu 43,739,000 sawa na
0.64% ya watu wote,na ni ya 30 kati ya nchi zote duniani ki idadi ya watu.
Muhimu ni kuwa ukifuatilia habari za njaa duniani, wanasema eti Korea Kaskazini ndio ya mwanzo.Tanzania sijui ni ya ngapi, lakini hakuna shaka Tanzania iko mbele mbele kinjaa kuzipita hata nchi za majangwa.Tatizo nini?.Kwa njaa hatuzisikii China wala India ambazo inaonesha ingekuwa hivyo kutokana na idadi ya watu wake.
Iwapo mipango mizuri kama KILIMO KWANZA tunayo, inabidi tujifunze mengi kutoka kwa nchi hizi mbili.Kwa kuanzia tuone aina ya mazao yanayolimwa na nchi hizo pamoja na vyakula wanavyokula.
 
Dah,naona ni viroja kwa kwenda mbele...Mjadala mwema jamani!!
 
Back
Top Bottom