Tutumie akili zetu vizuri katika kumiliki mali kwa faida

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,482
40,496
Tumiliki vitu tunavyoweza kuvitumia

Kumiliki vitu vingi halafu huvitumii; huo ni mpango mbovu katika utumiaji wa akili.

Chochote unachomiliki, unatakiwa ukitumie, iwe; mashamba, majengo, vyombo vya moto n.k

Nakuvitumia huko, ni kuhakikisha, vyote vinatumika kwa kufanya kazi; chombo cha moto kiwe barabarani, majengo yawe yanakaliwa, mashamba yawe yanalimwa n.k

Utakuta mtu anamiliki ekari 500, 1000, 3000 n.k lakini analitelekeza na kuwa pori, kuwapatia wengine walitumie, hataki; Lakini atasimama mbele na kusema namiliki shamba, hii sio sahihi tutumie akili zetu vizuri

Mwingine anaweza kumiliki labda magari 10 n.k, lakini lililopo barabarani ni mawili tu, atasema akiyaruhusu yote yatembee yatakula mafuta; sasa kwa nini uliyanunua yote; tutumie akili zetu vizuri.

Mwingine anaweza kuwa na majengo mengi, lakini yanayotumika ni machache; lakini yeye anaona fahari kuwa na majengo mengi, hii sio sahihi, tutumie akili zetu vizuri.

Tutumie akili zetu vizuri
 
Ili wafe kwa stress au?
siku itokee magari
Yote alowapa watu yakipata ajali je,
Kisa tu yakae barabarani?
 
Mimi nina shamba fulani ila mtu mwenye mtoto mchanga hatakiwi kulilima kamwe so jiongoze
Mapori ni mengi sana, kama wameshindwa kuendeleza, wapewe wanaoweza kuendeleza; kuliko kumiliki shamba kubwa huku kukiwa hakuna uzalishaji.
 
Unakuta jitu kwenye .Bufee linapakua chakula cha kila namna, halafu likikaa kula linakula nyama tu vingine hata haligusi au linachukua bia,maji linakunywa nusu. Ukiliuliza kwa nini, linakwambia nafidia mchango.
 
Back
Top Bottom