Tutengeneze mazingira ya kuondoana madarakani kistaarabu

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Mtake msitake, binadamu ni tofauti na mnyama, ambaye hutamkandamiza akubali siku zote.

Tulichokikataa kwa wazungu wachache wa Afrika ya kusini zamani;

hatutakifanya leo kikubalike popote!

Ubabe, maguvu siyo suruhu katika ulimwengu uliostaarabika!

Si-mnaona mataifa yenye nguvu yanavyoaibika pale wanapojaribu kuvitiisha vitaifa vidogo!

Kimsingi sisi kama taifa tulipaswa kutengeneza utaratibu wa kuondoana madarakani kistaarabu.

Nani hajui kama kudharauliana kwa kuibiana kura ndiko kutalipeleka taifa hili kubaya?

Kwa nini sisi waafrika mpaka leo tuishi kama mang'ombe?

Kulikoni tusiheshimiane na kutengeneza utaratibu unaoaminiwa na wote; wa kuondoana madarakani kwa amani?

CCM, Chadema, ADC, CUF na kadharika, vyote ni vyama vyetu sote.

Kwa hakika tunajua kuna njia mbili za kuheshimiana baina ya ndugu.

Mosi, ni ile ya kupigana mpaka mnachoka na kurejea mezani kukubaliana. ambayo tulio wengi hatuitaki.

Pili ni kwenda mezani moja kwa moja, ambayo baadhi hawaitaki, na hasa wanaonufaika.

Watanzania lazima tuchague kati ya njia hizi.

Kenya wao walichagua njia ya kupigana mpaka wakaheshimiana! Na kurudi mezani wakaandaa utaratibu unaviweka na kuviondoa vyama vya siasa madarakani kwa amani.

Hongera yao maana walikata mzizi wa fitina.

Mbona sisi hatukujifunza ili tuindee njia salama bila machungu?

Siku zote mwenye hekima hujifunza kwa makosa ya wenzake, bali mpumbavu hujifunza kwa makosa yake akiwa na makovu!

Mungu tupatie kiongozi atakayekuja kuliona hili tatizo linalotusibu akalishughurikia.
 
Back
Top Bottom