Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,502
113,610
Wanabodi,

Hii ni Makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa Jumapili ya leo, Tarehe 19 Mwezi Machi, ambapo leo ndio miaka miwili kamili ya Rais Samia madarakani, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania siku kama ya leo, miaka miwili iliyopita.

Screen Shot 2023-03-19 at 1.21.15 PM.png
Screen Shot 2023-03-19 at 1.21.37 PM.png

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "mgema akisifiwa, tembo hulitia maji".

Kuanzia leo na mpaka mwisho wa mwezi huu, vyombo vyetu vya habari, Radio, TV na Magazeti vitashehenezwa na makala za kusifu na kumpongeza Rais Samia kwa miaka yake miwili madarakani, haswa kwa kuangazia mambo mengi, makubwa na mazuri aliyoyafanya ndani ya hii miaka yake miwili madarakani, hivyo kama wote tutapongeza tuu kwa yaliyofanyika, hatutakuwa tunamsaidia Rais Samia, unless kama na Rais Samia ni Rais mpenda sifa kwa kufanya mambo kwa masifa ili watu waone wampongeze!.

Samia ninayemuona mimi hafanyi mambo kwa masifa ili watu waone au kufurahisha watu, anafanya mambo kwa ukweli ili mambo yaende.

Mtu wa namna hii anahitaji kuungwa mkono na watu wote ambao ni Wazalendo wa kweli wa taifa lao na wenye mapenzi mema na nchi yao, hivyo mimi nami, na Safu yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa, yenye Fikra Mbadala, najiunga na Watanzania wengine wote kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka miwili madarakani.

Ila mimi badala ya kusifu tuu, kwa kuchelea mgema huyu tembo asije kulitia maji, mimi namsaidia mgema wetu kwa kumuangazia jambo moja kubwa muhimu kuliko yote ambalo lilipaswa kufanyika toka mwanzo, lakini bado halijafanyika.

Lengo la kuliangazia hili sio ili kumpangia kazi Rais wetu Samia, afanye hiki au kile, no!. Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT, Rais wa JMT hapangiwi!. Anaweza tuu kushauriwa lakini kwenye kufikia maamuzi, Rais wa JMT anafikia maamuzi yeye kama yeye kwa kufanya kile anaona kinafaa na halazimiki kufuata ushauri wowote wa yeyote, anafikia maamuzi yeye kama yeye hivyo hakuna ubaya wowote kumshauri jambo lolote rais wa JMT, na hiki ndicho ninachokifanya leo kwenye makala hii. Kwa vile wote sio wasomaji wa vitu deep, wale wa short and clear tuishie hapa na ku jump mwisho, wale wazama deep, tuzameni.
Mwezi huu wa March pia ni mwezi wa kihistoria, wa kumbukumbu nzuri na tamu kwa Tanzania kupata rais wa kwanza Mwanamke, Dr. Samia Suluhu Hassan, ambaye leo atimiza miaka 2 madarakani. Hivyo ni mwaka wa ukombozi wa Mwanamke na kwa vile Rais Samia ameupata urais kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, akashauri uchaguzi wa 2025 Watanzania sasa twende tukachague rais Mwanamke.

Katika miaka hii miwili ya Rais Samia, amefanya mengi, makubwa mazuri kwenye nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Lengo la makala hii sio kuzungumzia mafanikio ya Rais Samia na mambo makubwa mazuri aliyoyafanya bali kumsaidia tuu Rais wetu Samia kuwa kuna jambo moja kubwa kuliko na muhimu kuliko jambo lolote au mambo mengine yote kwa taifa lolote ambalo Rais Samia anapaswa kulifanya kabla ya kuhitimisha awamu yake ya kwanza October 2025.

Kilio kikubwa cha kisiasa kwa sasa ni kilio cha katiba mpya, ila kwa huu muda wa miaka miwili uliobakia kwa Rais Samia kukamilisha awamu yake ya kwanza, hautoshi kwa mchakato wa kutupatia katiba mpya bora, vinginevyo tutake bora katiba, ila muda huu wa miaka 2, unatosha kabisa kufanya mabadiliko ya katiba, kwa spirit ya "Linalowezekana leo, lisingoje kesho!".

Nizungumzie kidogo ushauri kwa rais wa JMT. Rais anapewa ushauri kwa njia Kuu mbili. Ushauri rasmi na ushauri usio rasmi

Ushauri rasmi ni ule ushauri unaotolewa na washauri rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, wasaidizi wake, wakuu wa taasisi na vyombo vyake, usually ushauri huu huwa unakuwa kwa maandishi, formally.

Ushauri usio rasmi ni ushauri mwingine wowote ambao rais wetu anaweza kushauri na yeyote kwa njia yoyote, tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wasanii, wanamuziki au wananchi wowote wa kawaida, enzi za JPM wananchi walitumia mabango, wasanii wakitumia sanaa, wanamuziki wakitumia nyimbo na sisi waandishi tukitumia kalamu zetu.

Kuna wengi wanadhani kwa vile Rais wa nchi ana washauri rasmi, basi washauri hao ndio wanaomshauri ushauri mzuri au ushauri sahihi, bila kujua kuwa kuna uwezekano, ushauri usio rasmi kwa rais wetu ukawa na manufaa kwa taifa letu kuliko hata ushauri rasmi.

Mfano mzuri ni kwa vile nchi yetu inaongozwa na katiba, wasaidizi wa rais walipaswa kuijua katiba na kumshauri rais wetu ushauri stahiki.

Lakini kama washauri waliopaswa kuijua katiba, hawaijui katiba kikamilifu, ikitokea rais wetu akakiuka katiba bila ya yeye kujua, na wanaopaswa kuijua katiba ili kumshauri rais wetu, ama hawajui, ama wanajua lakini wanamuogopa sana kumwambia rais katiba hairuhusu jambo fulani, watu pekee wa kumshauri rais ni sisi wananchi wa kawaida, na hiki ndicho ninachokifanya hapa.

Katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote ikipingana na katiba, sheria hiyo inakwenda kinyume cha katiba inakuwa ni sheria batili.

Mamlaka ya kuibatilisha hiyo sheria inayokinzana na katiba ni katiba yenyewe na sio Mahakama Kuu!. Kazi ya Mahakama Kuu ni kutamka tuu kuwa sheria fulani ni kinyume cha katiba, na tangu baada ya tamko hilo la Mahakama Kuu, ubatili huo unakuwa ni tayari umeisha batilika kazi ya serikali na Bunge ni kuufuta tuu ubatili huo toka kwenye vitabu vya sheria!.

Nimesema wasaidizi wa rais na washauri wa rais walipaswa kuijua katiba lakini hawaijui ndio maana baadhi ya wanasheria wetu, na serikali yetu (sio awamu hii ya Rais Samia), walitunga sheria fulani yenye kipengele batili, kinachokwenda kinyume na katiba ya JMT. Bunge letu likaitunga sheria hiyo batili na rais akaisaini sheria hiyo batili ambayo inaendelea kutumika mpaka leo ninapoandika hapa.

Mchungaji Mtikila, (Mungu amuweke roho yake mahala pema peponi) akafungua shauri kupinga kipengele hicho, akashinda, mahakama ikakitamka kipengele hicho ni batili.

Serikali ikakata rufaa kupinga hukumu hiyo na wakati huo huo kufanya mabadiliko ya ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 na kukichomekea kipengele hicho ndani ya katiba yetu.

Kwenye ile rufaa serikali ilishindwa, Mchungaji Mtikila akafungua shauri jingine kupiga mabadiliko hayo ya katiba, na akashinda tena kwa Mahakama Kuu kutangaza mabadiliko hayo ni batili kwasababu yameingiza ubatili ndani ya katiba yetu!.

Serikali ikakata rufaa kupinga hukumu hiyo na Mahakama ya Rufani ikatamka kwa lugha ya Kiingereza "The Court is not the custodians of the will of the people", the will of the people ni katiba, kumaanisha Mhimili wa Mahakama sio mlinzi wa katiba, hilo ni jukumu la Mhimili wa Bunge. Hivyo suala hilo likarudishwa Bungeni kitu ambacho sio sahihi. Hivyo mpaka leo ninapoandika makala hii, ubatili ule bado uko kwenye sheria zetu na ndani ya katiba yetu!.

Kwa mambo makubwa mazuri Rais Samia anayoyafanya, naamini kabisa ndani ya moyo wake kwa kauli na matendo, amekubali mchakato wa katiba mpya kujadiliwa lakini kipindi cha miaka miwili kufikia uchaguzi wa 2025 ni kifupi kupata katiba mpya, hivyo mchakato wa katiba mpya utawekwa kiporo na kuingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025 -2030.

Kwa vile ubatili kwenye katiba yetu ulichomekewa kiubatili kwa hati ya dharura, ikimpendeza Rais Samia, anaweza kabisa kukicholopoa kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu kwa kutumia hati ya dharura kama walivyo kichomekea, kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025. Hili linawezekana kabisa. Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!.
Hili la katiba na kumshauri rais Samia aliharakishe kwa utaratibu wa Linalowezekana leo lisingoje kesho ni kwasababu hata aliyelianzisha JK alilianzisha kiungwana tuu, halikuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2010- 2015. Likawekwa ndani ya Ilani ya 2015-2020, lakini Mwamba akasema sio kipaumbele chake!. Kuna akina sisi wa kizazi cha kuhoji, hili tulilihoji Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Mimi niliamini kabisa Rais Magufuli angetuachia katiba mpya ki JK JK kwenye hili awamu yake ya pili licha ya katiba mpya kutokuwepo ndani ya Ilani ya CCM 2020 - 2025 na nikaandika humu JF vision yangu on JPM na katiba mpya Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza kama sauti HII hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Nampongeza Rais Samia kutimiza miaka miwili madarakani.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Sita mumunya. Mpeni pongezi zake anazostahili. Zangu mie na mimi zitakuja baada ya Uchaguzi 2025
Nuff said

Amani iwatawale
 
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa Jumapili ya leo, Tarehe 19 Mwezi Machi, ambapo leo ndio miaka miwili kamili ya Rais Samia madarakani, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania siku kama ya leo, miaka miwili iliyopita....
"Katiba haitakuletea menu mezani, hiyo ni kwa ajili ya wanasiasa' mwisho wa kunukuu.
 
Wanabodi,

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Paskali
maoni na mtazamo wangu BINAFSI juu ya uwepo wa haja kubwa ya Marekebisho ya haraka ya Katiba yetu ya JMT kulingana na mahitaji ya sasa. Marekebisho haya yafanyike haraka na mapema kabla ya Uchaguzi wa 2025
Mkuu Mkandara , hili ni ombi langu kama ombi lako kwa Mama, ajitahidi la katiba mpya amalizane nalo kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025.
P
 
Mkuu Mkandara , hili ni ombi langu kama ombi lako kwa Mama, ajitahidi la katiba mpya amalizane nalo kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025.
P
Katiba Mpya ni mchakato mrefu sana na nakuhakikishia haiwezi kupatikana kwa sababu hoja nyingi ni za Kisiasa kuliko haki za Wananchi.
1. Hawatakubaliana kwenye Serikali ngapi?
2. Hawata kubaliana kwenye kupunguza madaraka ya rais
3. Hawata kubaliana Ubunge wa.awamu mbili.
4.. Hawata kubaliana muundo wa uteuzi wa viongozi wa tume huru ya Uchaguzi.
Hawata kubaliana serikali ya Majimbo n.k

Nasema leo na kesho kuwa Sheria mama haiwezi kutokana na maoni ama mapendekezo ya WATU. Just imagine hata Biblia tumeshindwa kuwa na moja kwa sababu tumeruhusumaoni ya watu hivyo kila dhehebu limepingana na dhehebu jingine mahala itakuwa Katiba?. Rasimu ya Warioba haitapita ngazi yoyote ya maridhiano.. Mark my word..
 
Katiba Mpya ni mchakato mrefu sana na nakuhakikishia haiwezi kupatikana kwa sababu hoja nyingi ni za Kisiasa kuliko haki za Wananchi.
Ni kweli kupata katiba bora ni mchakato mrefu, ndio maana kwenye andiko hili nimeshauri tufanye lile linalowezekana leo, lisingoje kesho.
1. Hawatakubaliana kwenye Serikali ngapi?
Hili halihitaji kukubaliana, serikali 3 ndio suluhisho la kudumu la changamoto za muungano japo mimi ni Nyerererist maoni yangu ni serikali moja Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
2. Hawata kubaliana kwenye kupunguza madaraka ya rais
Halihitaji kukubaliana, madaraka ya rais lazima yapunguzwe na kukasimiwa na Bunge na Mahakama kwa ajili ya kuongeza ufanisi. Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
3. Hawata kubaliana Ubunge wa.awamu mbili.
Hili halihitaji mjadala wala kukubaliana, kama kwenye urais limekubalika na kwenye ubunge litakubalika.
4.. Hawata kubaliana muundo wa uteuzi wa viongozi wa tume huru ya Uchaguzi.
Hili watakubaliana tuu kuunda tume huru Shirikishi.
Hawata kubaliana serikali ya Majimbo n.k
Tukiishakuwa serikali 3, hiyo ni federation tayari hivyo majimbo hayakwepeki!. Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani
Nasema leo na kesho kuwa Sheria mama haiwezi kutokana na maoni ama mapendekezo ya WATU. Just imagine hata Biblia tumeshindwa kuwa na moja kwa sababu tumeruhusumaoni ya watu hivyo kila dhehebu limepingana na dhehebu jingine mahala itakuwa Katiba?. Rasimu ya Warioba haitapita ngazi yoyote ya maridhiano.. Mark my word..
Let's be positive
P
 
Hili la katiba na kumshauri rais Samia aliharakishe kwa utaratibu wa Linalowezekana leo lisingoje kesho

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Paskali
Ndugu yangu, baadhi ya vitu vinavyolalamikiwa ni pamoja na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Je, kasi ya kushughulikia jambo hili anayoifanya SSH wewe inakuridhisha?
Natumaini jibu langu nimeliona.
P
 
Wanabodi,

Hili la katiba na kumshauri rais Samia aliharakishe kwa utaratibu wa Linalowezekana leo lisingoje kesho ni kwasababu hata aliyelianzisha JK alilianzisha kiungwana tuu, halikuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2010- 2015. Likawekwa ndani ya Ilani ya 2015-2020, lakini Mwamba akasema sio kipaumbele chake!. Kuna akina sisi wa kizazi cha kuhoji, hili tulilihoji Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Mimi niliamini kabisa Rais Magufuli angetuachia katiba mpya ki JK JK kwenye hili awamu yake ya pili licha ya katiba mpya kutokuwepo ndani ya Ilani ya CCM 2020 - 2025 na nikaandika humu JF vision yangu on JPM na katiba mpya Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Nampongeza Rais Samia kutimiza miaka miwili madarakani.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Hakuna mwana CCM hata mmoja anayethubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi.
Wewe Paskali huwezi kuthubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi, hususan kwenye 'forum' za CCM.
Duh...!, Mkuu fundimchundo , karibu bandiko hili, jee hilo linalowezekana leo, lisingoje kesho ni nini hapa ninachodai?.
P
 
Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza kama sauti HII hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Nampongeza Rais Samia kutimiza miaka miwili madarakani.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa
Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Wanabodi,

Hili la katiba na kumshauri rais Samia aliharakishe kwa utaratibu wa Linalowezekana leo lisingoje kesho ni kwasababu hata aliyelianzisha JK alilianzisha kiungwana tuu, halikuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2010- 2015. Likawekwa ndani ya Ilani ya 2015-2020, lakini Mwamba akasema sio kipaumbele chake!. Kuna akina sisi wa kizazi cha kuhoji, hili tulilihoji Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Mimi niliamini kabisa Rais Magufuli angetuachia katiba mpya ki JK JK kwenye hili awamu yake ya pili licha ya katiba mpya kutokuwepo ndani ya Ilani ya CCM 2020 - 2025 na nikaandika humu JF vision yangu on JPM na katiba mpya Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza kama sauti HII hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Nampongeza Rais Samia kutimiza miaka mitatu madarakani.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Pongezi Raisi Ssmia kwa miaka 3 madarakani.
P
 
Back
Top Bottom