minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 65
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini zimeahidi kukinyima kura Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyia mwezi Oktoba mwaka huu kwa lengo la kukishikisha adabu kwa madai kwamba kimewadharau baada ya kushindwa kutekeleza mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.
Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam na kiongozi wa Jumuiya hizo, Ally Basaleh alipozungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtoro.
Alisema CCM kimewadharau Waislamu kwa kushindwa kutekeleza Ilani yake ya mwaka 2005 ambapo kiliahidi kuanzisha mahakama ya Kadhi kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali ya Kiislamu.
Aidha alisema Waislamu hawapo tayari kuona serikali inaanzisha Mahakama hiyo kupitia mgongo wa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (Bakwata).
Alipinga kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwamba jukumu la kuunda Mahakama hiyo waachiwe Waislamu wenyewe kwa kuwa serikali inataka kujitoa katika suala hilo.
Aliongeza kuwa Waislamu wanataka suala hilo liingizwe katika Katiba ya nchi pamoja serikali kutoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wake ikiwemo kulipa mishara ya watumishi wake.
"Tunataka serikali iunde mahakama hiyo pamoja na kuigharamia kwa kuwa CCM mwaka 2005 katika ilani yake ya uchagzui iliahidi kutekeleza mpango huo," alisema
Aliongeza kuwa matatizo ya Waislamu yakiwemo ya kudai mirathi na talaka yanatakiwa kushughulikiwa na wao wenyewe kwani wao wanayajua kwa undani kuliko watu wengine.
Waislamu jijini Dar es Salaam wameandaa maandamano kwa ajili kudai mahakama hiyo huku Jeshi la Polisi likiwataka kuachana na mpango huo.
Wamedai kwamba hata kama polisi watawazuia kuandamana wao hawatajali lakini lazima watimize azma hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Charles Kenyela alisema waislamu wanaotaka kuandamana bila kibali wanakurupuka na kwamba mazungumzo kati ya jeshi hilo na viongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania, yanaendelea vizuri.
Kamanda Kenyela alisema viongozi hao waliwasilisha barua ya kuomba maandamano kufanyika Julai 9, mwaka huu, ambapo bado haijajibiwa na ipo kwenye hatua ya majadiliano.
"Nashangaa nimesoma kwenye vyombo vya habari viongozi hao wakitamka kwamba wataandamana kwa nguvu hata kama jeshi limekataa... Naona wanakurupuka tu bila kuzingatia sheria," alisema Kamanda huyo.
CHANZO: NIPASHE; Na Waandishi wetu -3rd July 2010.
HIVYO: wana jf, tatizo langu ni hapo kwenye rubrics. je, ni haki kisheria/kishariya, kutumia fedha za walipa kodi ambao baadhi yao ni makafiri, kugharamikia mahakama tajwa? without prejudice to the ongoing tallks between the GoT and BAKWATA/muslims, naombeni michango yenu.