Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Hivi kweli watu mnaona watu wanakufa na hawachoki na kweli mnaamini ni "nchi za Magharibi" ndio zinawafanya wajitokeze kila siku kuuawa? Ni kweli mnaamini wale waliokuwa wanaandamana Tahrir square walifanya hivyo kwa sababu nchi za "magharibi" zinataka hivyo? Kweli kabisa mnaamnini yule aliyejitia moto kule Tunisia alifanya vile kwa sababu Marekani "ilikuwa inamuunga mkono"? Mnaamini maandamano yanayoendelea huko Bahrain yanatokana na nchi za magharibi? Inawezekana kabisa wenzetu mnaamini wale waliokuwa wanaandamana kule Yemen kutaka Ali Saleh ang'oke walifanya hivyo kwa sababu Washington DC na London walikuwa wanataka ang'oke?
Jamani, tuwe wa kweli - mwanadamu ana kikomo chake cha kuvumilia haijalishi yuko wapi. Tuliyaona haya Georgia, tuliyaona haya Kiev, tumeyaona haya Beijing, tumeyaona haya hata London na DC kwenyewe! Yametokea haya Mississippi na yametokea Detroit. Tumeyaona Shaperville na yakajirudia Soweto! Tumeona haya mambo Arusha na tumeyaona Nyamongo; tumeyaona haya Mwembechai kama tulivyoyaona Pemba. Msije kufikiria kuwa hayawezi kutokea Temeke, Sinza, Kirumba, Magomeni, Mabatini, au kwenye mji wowote. Wananchi wana kikomo chake hawahitaji Mmarekani kuwaambia kuwa wanaishi katika maisha ya kukandamizwa?
Hivi ni nani kati yetu anaweza kuishi katika hali ya hatari ya kudumu - unazaliwa unakuta hali ya hatari na unakufa bado hali ya hattari ipo?