Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Nilipoanza kusoma hii mada ilibaki kidogo nikuunge mkono lakini baada ya kumaliza kusoma nimegundua ni ya kishenzi isiyotakiwa kuungwa mkono,unaposema wananchi wanatakiwa kusukuma taifa una maana gani?haya wamejitahidi kusukuma kidogo kilichopatikana kimechukuliwa na wajanja wachache wakina Chenge na kukificha ulaya,unapotulinganisha na China na Urusi ni kwa njia gani?huyo mama aliyefariki tumeambiwa alipigwa mtama na Polisi hivi hata mwanamke mama mtu mzima Polisi anathubutu kumpiga mtama?mada yako ni ya kipuuzi na kishenzi kabisa
 
Kwa taarifa yako, kuna baadhi ya sectors huko hufanya kazi zaid ya masaa 8. Sometimes hadi usiku kucha(over working). Na of course muda wa kazi unafahamika (hususan kipindi cha kazi au msimu wa Kilimo kwa Bongo).

Sasa M-Tz anagusa ofisini saa moja then anachepuka bar jirani kunitundika! Au Baba anatelekeza kazi za shambani kwa mke na watoto then anashinda kutwa nzima,wiki & mwezi mzima Bar anakunywa wanzuki,mnazi, #Ulanzi na kadhalika. Unatarajia jamii & Taifa litasonga mbele?

Kwani Tanzania haisongi mbele kwa kuwa watu wanakunywa pombe au kwa ufisadi uliokithiri kwa viongozi waliopo madarakani na uuzwaji wa rasilimali za Taifa?
 
Mkuu; Dunia ya leo si ya kale! We people have changed. We have grown a sortie of aggression.

Ushauri wako ni bora na umetoa mchango ulioutukuka ktk mada hii. Bravo!

Hope Polisi na wakubwa wao wangezingatia dhana hiyo. Si kila purukushani hutulizwa na Purukushani. Wanapaswa kuongeza weledi na maarifa zaid.

Pia, ni vyema nasie wananchi kujitahidi kuwa na simile. Kuna matukio au visa tunavifanya sometimes kwa namna ambayo haipendezi. Tujitahidi kuheshimu Mamlaka na kuwa watulivu ktk nyakati fulanifulani za matukio na visa. Sio kuwa aggressive na ushabiki usio na msingi.
Ushauri mzuri sana Mheshimiwa, lakini hata hiyo Mamlaka iwapende na kuwalinda wananchi, ikitokea hiyo mamlaka ndiyo inayowachukia na kuwaondolea uhai ama inasababisha wananchi wafe haina budi kuoneshwa kwamba vitendo hivyo havikubaliki kwa njia kama hiyo ya wananchi wa Ilula. Polisi inatakiwa ijitafakali kwa kina, kwa nini wananchi wanaigeuka badala ya kuigeukia? Hapa kuna kitu hakijakaa sawa, kuna haja ya kurudi nyuma na kutafakali kuangalia sehemu walipojikwaa ili kujifunza kuwa makini katika mwenendo wao. Lasivyo tuendako ni kubaya zaidi ya haya ya Ilula.
 
Kwa taarifa yako, kuna baadhi ya sectors huko hufanya kazi zaid ya masaa 8. Sometimes hadi usiku kucha(over working). Na of course muda wa kazi unafahamika (hususan kipindi cha kazi au msimu wa Kilimo kwa Bongo).

Sasa M-Tz anagusa ofisini saa moja then anachepuka bar jirani kunitundika! Au Baba anatelekeza kazi za shambani kwa mke na watoto then anashinda kutwa nzima,wiki & mwezi mzima Bar anakunywa wanzuki,mnazi, #Ulanzi na kadhalika. Unatarajia jamii & Taifa litasonga mbele?
Kuna watu wanafany kazi usiku,mfano walinzi,wahudumu wa guest,wanaouza biashara ya vyakula stendi,manesi,madoctor etc muda wao wa leisure ni mchana,sasa kwanini uwazuie wasiburudike kama wale ambao kazi zao ni za mchana na muda wa kupumzika ni jioni?tusiwapangie watu muda na namna ya kutumia hela yao
 
Acha kushabikia mauaji. Sera nzuri ni kuwaelimisha wananchi kuhusu maendeleo na sio kuwalazimisha na kuwaua!

polisi wa tanzania wanastahili kupigwa na raia maana wanatumika kisiasa kukandamiza democrasia kwa raia kupitia chama cha mapinduzi na hiyo ndiyo iliyo chochea chuki kwa raia dhidi ya polisi maana wanaona kwa mamcho yao kuwa haku na usawa katika kutekelea majukumu yao kwenye siasa.
 
Moja ya vitu amabvyo hujaviongelea ni malalamiko ya wananchi, jana pale Ilula ilikuwa kama "trigger" maanan walikuwa wakilalamika police kuwanyanyasa bodaboda sana, mfano bodaboda yupo kwenye mwendo police anakuja na gari anamuwekea kwa mbele, wanasema zaidi ya watu sita wamepata vilema kwa style hiyo na mmoja amekufa lakini hatua hazichukuliwi>
Swala la pili ni kwamba kwa mfumo wa uchumi ulivyombovu huwezi wapangia watu mda gani wafanye kazi na mda gani wapumzike, wananchi wengi vijijini ni wachapakazi sana, wanaamka saa 10 kulima kufika saa4-6 wanakuwa wamemaliza wanaenda kwenye urabu, ndo maana hausikii wamepewa chakula cha msaada zaidi ya kusikia mazao yao hayana soko.
Mwisho serikali ya kijiji inakusanya ushuru kila siku pale kilabuni, na operation kama zile huwa zinafanywa na sungusungu, kuna hisia kuwa police wanawakamata watu vilabuni makusudi na kuwepeleka kituoni alafu wanaweka sharti la kila kichwa kutoa 50000-200000 ili kutoka.

USHAURI
Police ikiimarish kitengo cha mahusiano (nadhani Mwema alijaribu na ilileta mafanikio kwa kiasi kidogo).
Serikamli ianzishe kitengo maalumu cha usuluhishi wa migogoro kwenye vituo vya police vya kikanda bila hivyo maafa makubwa yasubilia, mwishi police isiwe kwa watu waliofeli darasa.
 
inaonekana haujui operation za kijiji kata au taarafa zinafanywaje..serikaki za mitaa kupitia migambo wa kijiji au askari husika wa kijiji tajwa wanaandamana na Mtendaji,Mk wa mtaa nk.
kwanza kabisa inatakiwa wananchi wawe wame elimishwa kuhusu the so called by law.
by laws ni local government laws sio laws zinazo govern nchi hii,kwenye katiba sioni sehemu pameandikwa usifungue kilabu cha pombe SAA moja asubui,au bar SAA moja asubui (I stand to be corrected) lakin kwenye local government kuna by laws zimewekwa labda SAA 3 asubui hadi sita usiku,sasa hawa askari walikuwa wanatejeleza sheria ipi?
kuna mikoa mwingine ukienda,let's say Tabora kuna sehemu panaitwa ngambo,pake ni kula ulabu 24hours nenda shinyanga maeneo ya stand ya manyoni utakuta wamejiwekea Pepe kale yao wanaserebuka na kula ulabu Kama kawa na shughuli za maendeleo zinaendelea.
kwa MTU mwenye akili ndogo Kama huyu mleta mada ambae ajui operation za vijiji vinafanywaje ndie anaweza kulinganisha by law na law..sheria za China na Tz.
Hao police waliripoti kwa Mtendaji,au mwenyekiti kwamba wanaenda kufanya msako? mbona the previous day walipewa elfu ishirini wakamuacha,waliporudi kwa Mara nyingine ndio akawa Hana ndio wakamkata mtama,na kukutwa na mauti?
 
Angalieni muda alioweka hii post,kama yuko tanzania ni wazi kakosa usingizi au mamsap/bamsap kamnyima unyumba hivyo hasira zake kazimalizia Ilula.Mwenye information atujuze huo mtaa anaongoza wa chama gani?

Exactly mi mwenyewe nadhan itikadi za chama zinahusika hapo. Mi ni mkazi wa Ilula Mwaya. Ni kweli katika uchaguzi wa serikali za mtaa CCM walichukua ushindi mitaa mingi ya Ilula. Lakini kwa mtaa wa Ilala ambako ndo sakata hilo lilitokea CHADEMA ndo ilishinda!
 
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

Unadhani hii ni jamuhuri ya KONDOO wa kupangiwa kila kitu na manjagu.Saa ya kula kunywa kulala kutembea...nk,total rubbish!
 
Unadhani hii ni jamuhuri ya KONDOO wa kupangiwa kila kitu na manjagu.Saa ya kula kunywa kulala kutembea...nk,total rubbish!

mwambie mkuu,we are not in curfew tuwe restricted na kupangiwa muda wa kula,kunywa,kwenda msalani nk.
alafu mbona kwenye police mess wanakunywa asubui tu..hata hao wana ilula walikuwa wanakunywa muda huo walikuwa wametoka night shift.
alafu another thing huwezi kunywa bila kuwa na hella,which means hao watu walikuwa wanakunywa ni wachapa kazi.maybe wao kazi zao ni za usiku,mchana wanaburudika.
 
Kwa taarifa yako, kuna baadhi ya sectors huko hufanya kazi zaid ya masaa 8. Sometimes hadi usiku kucha(over working). Na of course muda wa kazi unafahamika (hususan kipindi cha kazi au msimu wa Kilimo kwa Bongo).

Sasa M-Tz anagusa ofisini saa moja then anachepuka bar jirani kunitundika! Au Baba anatelekeza kazi za shambani kwa mke na watoto then anashinda kutwa nzima,wiki & mwezi mzima Bar anakunywa wanzuki,mnazi, #Ulanzi na kadhalika. Unatarajia jamii & Taifa litasonga mbele?

Hiyo sheria ya kutokuwa kunywa pombe wakati wa saa za kazi imeanza lini? Mbona enzi ya Nyerere hatujaiona hiyo sheria, sheria zipo maofisini ukija umekunywa utapewa onyo ikizidi utafukuzwa napo inategemea labda ushindwe kuwajibika lakini kama unafanya kazi vizuri, hata mimi sikufukuzi kazi, nakumbuka Hospitali ya Muhimbili kulikuwa na Profesa Shaba huyo alikuwa hafanyii maiti uchunguzi mpaka awe bwiii chakali kwa pombe na alikuwa anafanya kazi yake vizuri sana na Mwalimu Nyerere alikuwa anajua lkn maadamu yupo kazini na mchapakazi kuna shida gani?
Na ukiangalia walevi wengi ndio genius na wachapa kazi na wanategemewa maofisini, kuna maboss wengine bila kunywa hata kuweka signature inakuwa ngumu mkono unatetemeka aki sign cheque ikienda Bank inakataliwa.
Uzembe wa kufanya kazi ni mtu mwenyewe, wengine wakifika ofisini anaongea na simu muda wote, wengine wanafika ofisini wanakaa kidogo wanaenda kwenye miradi yao na wengine wanaishia guest.
Unajua kama Serikali inaingiza pesa nyingi za TAX zinapatikana kwenye pombe, huoni kama walevi wanaliongezea taifa pato kubwa? Halafu leo tunasema wanatuletea umasikini kwa Taifa sio kweli. Serikali kama inaona shida wafunge viwanda vyote vya bia, Serikali ndio itafirisika na kukosa wataalamu wazuri kwani bila pombe wengine akili zinalala.
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Ni mawaidha mazuri kama polisi wangeonekana live pia wakiwakong'ota na kuwatia pingu watu wanaoiba mali za umma kama vile escrow, richmond, meremeta, wanaotorosha twiga, wezi wa meno ya tembo, wanaosababisha huduma hospitalini, shuleni, maji kuwa mbovu na wauza madawa. Lakini badala yake polisi wanaonekana live wakiwapiga watu wanaopinga dhuruma na wizi huu (akina lipumba, ulimboka, mwangosi, vijana wa jkt, n.k) bila huruma. Polisi wanakula rushwa kutoka kwa raia waliopigika pia kimaisha kutokana na sera mbovu za watawala. Hivyo raia wanaliona jeshi lao la polisi kama jeshi la mkoloni mweusi. Ifike mahali polisi na raia tutambaue kuwa sisi sote ni watanzania tunaojenga nyumba moja, akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu, polisi utampigaje mtanzania mwenzako kwa kutumwa na mtu aliyeshindwa kutimiza majukumu yake kwa umma kama vile kutoa huduma za afya, maji, umeme, elimu, kuondoa umaskini, kutoa ajira, n.k? na wewe raia utachomaje kituo cha polisi kilichojengwa na kodi zenu? Jambo la msingi hapa ni kuwa raia na mtawala hakuna msafi, kunywa pombe wakati wa kazi sio sawa na kuongoza vibaya na wizi wa mali za umma sio mzuri pia, issue ni kwamba polisi wanapiga wanaokunywa pombe wakati wa kazi na kuwaacha wale wanaoiba mali za umma? Ni nani atakayewatuma polisi wakawakong'ote pia wala rushwa na wezi wa mali zetu za umma? Tuanzie wapi kama watanzania?
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

1. Hao Polisi walikwenda kutekeleza ilani gani unayosema na kumaanisha? Kwani jeshi lina ilani au ni ya chama cha mapinduzi? Na kumbe ilani yenyewe ni ilani ya kuua RAIA?

2.Inakuwaje kila siku mnakuja na nyimbo za kuua raia kwa bahati mbaya? Hilo jeshi hamna kitu lijitazame upya, haya mambo ya jeshi kutekeleza Ilani siyo!
 
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

Hao majambazi polisisiem kwa nini wanaonea watu wa vijiji ni?Huku mjini watu wanakunywa pombe tangu saa 12 asbh mbona hawawakimbizi?Kuna bar pale Kkoo kama unaenda Kamata kwenye stand ya Mbagala inaitwa Kwa Immanuel watu wanakugonga gambe 24 hrs iweje Ilula iwe nongwa na wakati yule mama Ndio alikuwa anaandaa kinywaji?Naona bado ccm damu za watu hazijawatosha wanaendelea kuzitafuta...
 
Kama kweli mnajali uzalishaji mbona tukizalisha nyie mna iba? Mala escrow mala rich mond mala mabilioni ya uswis, huku mna tuua mkituswaga tukazalishe, wakati nyie mnaiba
 
Mimi ckubaliani na mtoa maada: 1 polisi hufanyakazi ktk mifumo ya kikoloni ya kutisha watu ndio maana hata yule mama alikufa kwaajil ya kuwaogopa polisi, 2: polisi hawana Elimu ya kutosha (waledi) Kwani wengi wao wamepata kazi km za urithi, 3: raia wengi hatuna elimu juu ya mswala ya kisheria ndiyo polisi hufanya wanachoweza kufanya kwasababu wanajua hatuna elimu.(mara nimefika vituo vya polisi na wakiwatisha hata watu wanaowaita wao ni wazuluraji kwamba hii kesi hutoki ni kesi mbaya sana ili kumjengea woga atoe rushwa) Na pointi yangu ya mwisho:Tanzania ni nchi ya kulima na wafanyakazi na wafanyabiashara lakini uti wa mgongo wa Taifa hili ni kilimo na ndio hao wamezalisha mazao mpaka umeshindwa kwa kuyapeleka na wanalima hayo mashamba yao wao kwa hiyari bila marungu wala kukimbizana na mtu. Na hao mnaowaita wafanyakazi ukienda hata ofisini unakuta wapo watu wawili au hata mtu mmoja ofisini unapohitaji huduma:wanakuambia msubili fulani kaenda kunywa chai, akifika na yule uliyemkuta na yeye anaondoka, ukimweleza shida yako alitoka kunywa na yeye anakujibu msubili fulani ameenda lunch. Na ndiyo wala rushwa, mafisadi, wezi wa mali ya umma na kila aina takata ni wao lkn hatusikia wakipigwa marungu; na km yupo aliyewahi sikia mkulima fisadi au mla rushwa basi akomenti hapa chini " Wito wangu; tusiwanyanyase wasio na elimu kwasababu nafasi zetu bali tutumie nafasi zetu kuelimisha sisi kwa sisi. Kwa kuwambusha tu baadhi, sisi wengine tulisomeshwa na wauza pombe lkn ndio hao hao uti wa mgongo wa Taifa. Be free in free state
 
Back
Top Bottom