Tusipoangalia kanda ya ziwa itatuletea tyranny of the majority

Kanda ya ziwa ndyo kila kitu kwa Nchi hii ila kwa wanaoelewa. Na na ndyo kanda inayotoa watu makini sana kwa wanaoelewa pia wanaelewa hili

..ni kanda yenye watu wengi, rasilimali nyingi, na viongozi au wawakilishi wabovu.

..kanda ya ziwa ingekuwa na viongozi makini wenye upo ingekuwa na hali bora ya kiuchumi kuliko maeneo yote hapa nchini. Yaani Watanzania tungekuwa tunakanyagana kujaribu kuhamia huko.

..so far viongozi wa CCM toka kanda ya ziwa wamekuwa WABINAFSI wa kutetea maslahi yao na ya chama chao badala ya kuwatetea wapigakura wao.
 
Ni kweli na wanasiasa wakubwa wanakanyagana kuiteka Lake Zone lakini bahati mbaya kule watu wachorwa mihuri ya JPM na watu wananongwa kweli.

Penda usipende bado hali ya hewa si nzuri kwa CCM kule kanda ya ziwa na kuna wimbi la vijana wengi watakuwa wapiga kura wapya 2025 ambao ni kizazi kilichomshuhudia JPM.

..nimeambiwa Wabunge toka kanda ya ziwa ni MATAJIRI kuliko wabunge wa maeneo yote ya Tanzania.

..Utajiri huo wa wabunge wa kanda ya ziwa hauko translated ktk ubora wa maisha ya wapiga kura wao.
 
Mheshimiwa Mpina asikutishe hata kidogo, anayo hulka ya kujiweka juu sawa na marehemu JPM ni asili yao hiyo, hata ukimtazama Kalemani utagundua yupo hivyo hivyo.

CCM watakuwa wanajua namna ya kuishi na kanda hiyo inayokuwa kwa kasi haswa Samia ambaye boss wake wa zamani ni mtu wa kanda yetu pendwa.
Tofautisheni usukumani na kanda ya ziwa maana siyo kila mwenye asili ya kanda ya Ziwa ni msukuma

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Kanda ya ziwa wameishaujua mtaji wao kwenye siasa za Tanzania. Wanajua jinsi walivyo wengi. Na bahati mbaya au nzuri ndiyo wanaongoza kwa kuzaliana nchini. Dalili zinaonyesha wanataka kuutumia mtaji huo kukandamiza wengine. Leo hii hata wabunge wao ni kama hawasemehi majimbo yao tena bali kanda ya ziwa yote. Ni kama kila mbunge wa eneo hilo anawakilisha kanda yote.

Tusipokuwa makini watatukandamiza nchi yote sababu ya wingi wao. Watataka lazima mtu fulani mkubwa serikalini atoke kwao. Watalazimisha gawio kubwa la miradi nk. Nadhani huko mbeleni mfumo wa majimbo hautahepukika.
Huwezi kuikwepa reality !
Kama hivyo ndivyo ilivyo basi itakuwa hivyo tu !🙏
 
..nimeambiwa Wabunge toka kanda ya ziwa ni MATAJIRI kuliko wabunge wa maeneo yote ya Tanzania.

..Utajiri huo wa wabunge wa kanda ya ziwa hauko translated ktk ubora wa maisha ya wapiga kura wao.
Mifumo ya uchaguzi ndani ya CCM ni uozo.
 
Ewe Wakili wa shetani ...
Naomba nikupe taarifa hii wewe na hao mashetani unaowawakilisha humu JamiiForums ......
HUB YA UCHUMI WA NCHI HII IKO KANDA YA ZIWA!

1- HIFADHI KUBWA YA TAIFA KWA MAPATO- "SERENGETI "
2- ZIWA KUBWA KWA MAPATO
-"Lake VICTORIA"
3- MIGODI MIKUBWA YA DHAHABU- GGM,BUZWAGI na NORTH MARA.
4- MGODI MKUBWA WA ALMASI"MWADUI".
5- UZALISHAJI WA ZAO LA PAMBA.
6-VUADILIFU NA UZALENDO KWA TAIFA.
7- UKAKAMAVU NA ULINZI KWA TAIFA.
8- UKWELI NA UWAZI KWENYE SIASA ZA NCHI HII.
9- RASLIMALI WATU.
10- ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YETU, Na Nchi zote za maziwa makuu!

kwa hiyo kabla mleta mada hujaongea upuuzi wako kwa sababu ya wanaokutumia!

Jitafakari na hayo machache hapo juu!
Jiulizeni kwa nini mkoloni wa kijerumani aliamua kwanza kuleta Reli ya kati huku "KANDA YA ZIWA" la Mama Tanzania
 
Kanda ya ziwa wameishaujua mtaji wao kwenye siasa za Tanzania. Wanajua jinsi walivyo wengi. Na bahati mbaya au nzuri ndiyo wanaongoza kwa kuzaliana nchini. Dalili zinaonyesha wanataka kuutumia mtaji huo kukandamiza wengine. Leo hii hata wabunge wao ni kama hawasemehi majimbo yao tena bali kanda ya ziwa yote. Ni kama kila mbunge wa eneo hilo anawakilisha kanda yote.

Tusipokuwa makini watatukandamiza nchi yote sababu ya wingi wao. Watataka lazima mtu fulani mkubwa serikalini atoke kwao. Watalazimisha gawio kubwa la miradi nk. Nadhani huko mbeleni mfumo wa majimbo hautahepukika.
Ukificha upumbavu wako itasaidia na vile mtu mzima
 
Mgawanyo haujawahi kuisha. Hata US wanajitambua kuwa kuna wahispania, walatino, weusi, weupe ambao nao kuna wajerumani, wascotland, Waireland, Waingereza wa England, Wafaransa, Waitaliano, Wayahudi, Wascandnavia
Kuna red na blue states, kuna kusini, Kaskazini, Mashariki na magharibi
 
Back
Top Bottom