Tusimung'unye maneno, barabara ya Kusini ilijengwa chini ya viwango!

Nilikua Mtwara tarehe 22 mwezi wa nne 2024 inasikitisha Sana Sana, wengi wanaongea kwa kuangalia picha, mimi nimefika huko, kile kipande cha kuanzia daraja la mkapa Hadi Somanga mbele mbele kule Hadi Nangurukuru ni Aibu Sana. Ndio maana Ajali haziishi
Inasikitisha sana namna tunavyoshindwa kusimamia miradi muhimu ya miundombinu kwa manufaa yetu wenyewe
 
Kwenye hii Barabara kipande Cha kuanzia ikwiriri Hadi somanga ndo kipande korofi mno , sasa kuna mambo mengi
1. Hiki kipande kina mito mingi mno maana ndo sehemu matawi ya mto rufiji yanaenda baharini hivyo maji yakua yameathiri sana
2 baada ya kujengwa hiki kipande lami yake ilikua na muonekano mweupe hivi , nadhani kokoto zilizotumika sio za lugoba, huenda zimetumika zile ya ubuyo ambayo ambazo water absorption zake hua ni kubwa kwa sababu ni porous kwa hiyo asphalt mix design huenda haikua efficient
3 Hii Barabara imekamilika miaka zaidi ya 15 iliyopita, huenda lifespan yake imeshaisha ukizingatia Barabara zetu nyingi design lifespan ni miaka 10 tu
4 Usanifu wa hii Barabara haukuconsider sudden load ya dangote factory, malori ya cement nayo yamechangia uchakavu wa hii Barabara to some extent, coz imagine dangone ana fleet kama 600 hivi , jumlisha na watu watu wengine hii Barabara lazima iharibike tu hasa kama Usanifu haukuzingatia huo mzigo ambao kimsingi haukuwepo kabisaaa

Ifanyike impact analysis kwa hiki kipande Cha km 60, kijengwe upya kwa kuzingatia new design assumptions
Let's be constructive na tuiache kunyooshana vidole hasa kwa hizi mvua A mwaka huu ambazo zipo juu ya kiwango Cha kawaida.
 
Leo unajipa utaalam wa kujuwa afya za watu humu JF. Mbona huishi kushangaza!
Tatizo lako ni lilelile la siku zote. Unao unafiki mkubwa sana. Leo ukikutana na huyu unasema hili, kesho akiwa hayupo huyo wa mwanzo, unaanza kumsema aliyepita. Hili ni tatizo kubwa kuliko hata hilo la uliyemwelezea wewe hapo.
Mkuu mada ikiwa juu ya uwezo wako kudadavua, we sepa tu uelekeo wa chit-chat!
 
Mkuu mada ikiwa juu ya uwezo wako kudadavua, we sepa tu uelekeo wa chit-chat!
Hakuna lolote la mada kuwa juu. Sijaanza kukusoma leo, na wala hakuna jipya katika uliyo andika katika mada hiyo unaloweza kudai lipo juu ya uwezo wa wengine kulitambua.
Nimekupa ushauri, bila shaka umekuingia akilini vya kutosha.
 
Mkuu usilazimishe kulumbana na akili kubwa.
Kubali tu ukomo wako wa kufikiri.
 
Sasa Mbona wanasema baada ya Masaa 72 pawe pametengenezwa? Tunaziba maji ya Mto kwa Mawe? Halafu mto unarudi ulipotoka?
 
Kwenye hii Barabara kipande Cha kuanzia ikwiriri Hadi somanga ndo kipande korofi mno , sasa kuna mambo mengi
1. Hiki kipande kina mito mingi mno maana ndo sehemu matawi ya mto rufiji yanaenda baharini hivyo maji yakua yameathiri sana
2 baada ya kujengwa hiki kipande lami yake ilikua na muonekano mweupe hivi , nadhani kokoto zilizotumika sio za lugoba, huenda zimetumika zile ya ubuyo ambayo ambazo water absorption zake hua ni kubwa kwa sababu ni porous kwa hiyo asphalt mix design huenda haikua efficient
3 Hii Barabara imekamilika miaka zaidi ya 15 iliyopita, huenda lifespan yake imeshaisha ukizingatia Barabara zetu nyingi design lifespan ni miaka 10 tu
4 Usanifu wa hii Barabara haukuconsider sudden load ya dangote factory, malori ya cement nayo yamechangia uchakavu wa hii Barabara to some extent, coz imagine dangone ana fleet kama 600 hivi , jumlisha na watu watu wengine hii Barabara lazima iharibike tu hasa kama Usanifu haukuzingatia huo mzigo ambao kimsingi haukuwepo kabisaaa

Ifanyike impact analysis kwa hiki kipande Cha km 60, kijengwe upya kwa kuzingatia new design assumptions
Let's be constructive na tuiache kunyooshana vidole hasa kwa hizi mvua A mwaka huu ambazo zipo juu ya kiwango Cha kawaida.
Respect mkuu kwa kujadili mambo ya kimsingi kabisa kihandisi.
Hii barabara yoote DSM TO MTWARA, hasa Ikwiriri -Somanga, iko katika failure mode.

Serikali kupitia wizara husika itake note hydrological facts kutokana na mvua za mwaka huu.
 
View attachment 2983070
View attachment 2983106

Kwa wale mliopitia habari za barabara ya Dar es salm, Kibiti, Lindi Mtwara hivi karibuni, sasa tunajionea madudu ya kale.
Barabara hii imejengwa chini ya viwango.
Na tukumbuke waziri aliyehusika na barabara hii kwa kupewa misifa mingi isiyo stahili.

Barabara ina katika kila leo kwa mvua ambazo ilistahili kuhimili.
Kiwango cha ujenzi wa barabara hii huwezi kabisa kulinganisha na kiwango cha kwa mfano Iringa akambako.
Wakandarasi ni wale wale -wachina.

Serikali ijionee sasa na msimamo wake usioendelevu- ati anapewa kazi-LOWEST BIDDER!
Ujinga huu sasa unasababisha usumbufu kwa maelfu ya wananchi, ukiacha ajali zinazosababisha vifo kutokana na barabara kutokidhi viwango.

Tunavuna tulichopanda kwa misifa isiyostahili.

NB INAHITAJIKA TECHNICAL REVIEW/AUDIT
Sasa hivi kunahitajika kuwepo a Technical Review au Audit ya ujenzi wa barabara hii. Nina uhakika madudu mengi tu yatagundulika.
Hata ya Bagamoyo ilijengwa chini ya kiwango na Waziri Husika alikuja kuichukulia hatua na Riasi na Kawambwa wanawabagamoyo walikuwepo
 
Mkuu ndio tatizo kubwa, tuliwekeza kimasikini sasa tunalipia udhaifu huo.
Tuta la barabara ni dogo, madaraja ni hafifu, ni mvua kama hizi za El Nino na Vimbunga ndio tunatambua kuwa viwango havihimili misukosuko.
Na matengenezo kurejesha mawasiliano ni ghali mno.
Barabara hii sasa irudiwe ili iwe na viwango kama vya Iringa-Makambako.
Ile ya makambako benki ya dunia wamekopesha wanajua shaba ya Zambia na mizigo ya Malawi itawalipa
 
Bila shaka ilijengwa na wale jamaa wa Kharafi.
Lakini ni Bora watu wakusini wamesahau yale mateso ya nangurukuru, somanga nk.

Kipindi cha masika na mvua Mtwara kulikuwa hakuendeki, option ya Meli ilikuwa 2days.

Hizi barabara shida ni umasikini wetu lakini kuwapa wachina plus kupenda urahisi na rushwa tunabaki na majanga
 
Halafu hapo mnazi mmoja hadi Masasi ni pa zamani mno na ubovu wake
Sasa kama hadi Muhoro -Somanga pameharibika ,si upuuzi maana pamejengwa juzi tu
Lami ya masasi ya zaman sana ila Muhoro hapajakaa sana viraka kama vyote
 
Back
Top Bottom