tusaidiane kuhusu Mboga na kachumbari

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
wengine wanasema ni zile za majani tu yaani vegetables ndizo zinazopaswa kuitwa MBOGA, wengine wanasema makundi yote ya vitoweo kama nyama, mbegu, mizizi, wadudu (kama kule buhaya), matunda, majani nk. yoye yanapaswa kuitwa MBOGA. wengine wanasema kwa mlo wenye vitoweo vingi vya aina mbalimbali, ni kile litoweo kikuu pekee (yaani kile ambacho kikiondolewa chkula hakiliki) ndicho chapaswa kuitwa MBOGA na vilivyobaki ni KACHUMBARI tu.

sasa kwa wale wanotumia chai au uji pamoja na samaki ama nyama au mboga za majani kama matembele na kismvu kama kifungua kinywa nao wanakula MBOGA? je wanaokunywa supu, mchemsho, wanaochoma, kukaanga ama kutokosa nyama kama mbuzi, kitimoto, kuku nk. sehemu za starehe nao wanakula MBOGA? vipi kuhusu maziwa yanapotmiwa pamoja na chakula nayo yaweza kuitwa MBOGA?

ni neno gani moja la kiingereza linaloweza kutamkwa likimaanisha neno la kiswahili "MBOGA"? na lipi hutumika kumaanisha KACHUMBARI?

tusaidiane tafadhari.......................
 
mboga ni za majani ambazo zimepikwa/zinapikwa kabla ya kula(vegetables)
kachumbari inaliwa mbichi/mboga maalum zisizopikwa(salad)
nafikiri ndio hivyo kwa ninavyoelewa
 
mboga ni za majani ambazo zimepikwa/zinapikwa kabla ya kula(vegetables)
kachumbari inaliwa mbichi/mboga maalum zisizopikwa(salad)
nafikiri ndio hivyo kwa ninavyoelewa

thanks mzee, tusaidiane tena:
je nyama, samaki, maziwa karanga, njugu, kunde nk vikiandaliwa kama kitoweo unaweza kuviita mboga? na je neno mboga kiingereza chake ni nini?
 
thanks mzee, tusaidiane tena:
je nyama, samaki, maziwa karanga, njugu, kunde nk vikiandaliwa kama kitoweo unaweza kuviita mboga? na je neno mboga kiingereza chake ni nini?

nyama,samaki vikiandaliwa kama kitoweo ni mchuzi huo sio mboga bali kitoweo, kiingereza ni curry au stew.
karanga,njugu,kunde na maharage zote mboga,vegetables

mboga=vegetables(green vegetables inluding mchicha,kisamvu etc some are not green)
 
Kwa mujibu wa Kamusi nya Kiswahili Sanifu toleo la 2, mboga ni majani yanayoliwa na binadamu aghalabu baada ya kupikwa au kitu kama vile nyama, maharage n.k kinachotumika kutowelea chakula
 
Nyama,mayai, maaharage , kunde, samaki , kisamvu, matembele,majani ya maboga ,
vyote hivyo na kwa mapishi tofauti vinapoliwa pamoja na Ugali , Wali ,Mihogo, na Ndizi,
huitwa kitoweo. au mboga.

Kwa mtazamo wangu lakini...
 
Back
Top Bottom