Turudishiwe Utanganyika wetu!

JuaKali

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
776
118
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia habari mbali mbali kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa jinsi mambo yanavyoendelea huko hatuna budi Tanzania bara tukaanza kudai serikali yetu ya Tanganyika kwa nguvu zote. Tutakuja juta mambo yakienda mrama. Hawa jamaa ni ma-selfish wakubwa wanapenda kuvuna wasipopanda lakini vya kwao wanavijengea ngome. Tuungane pamoja kudai taifa letu. Mungu bariki Tanganyika
 
Muungano ni kama ndoa ya kikristo haina talaka. Zanzibar ni mke katika ndoa hii analeta chochoko ili apate talaka. Dawa ni kumuadabisha na sio kurudia useja. Tanganyika haiwezi kurejewa na muungano utadumu licha ya kelele za mke as long as yuko kwenye ndoa ya lazima.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Daini yakhe. Halafu tutaona jinsi gani nanyi mtakuwa mnailalamikia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Muungano ni kama ndoa ya kikristo haina talaka. Zanzibar ni mke katika ndoa hii analeta chochoko ili apate talaka. Dawa ni kumuadabisha na sio kurudia useja. Tanganyika haiwezi kurejewa na muungano utadumu licha ya kelele za mke as long as yuko kwenye ndoa ya lazima.
Mungu ibariki Tanzania.

Sisi watanganyika hatuna ubavu wa kuiwacha Zanzibar uiende watanganyika tunaojua historia ya zanzibar tuna uhakika isingekuwa muungano leo hii wale wangekuwa ni moja ya nchi tajiri duniani na nchi iliyoendela. Kwani kwa uchache tu ni nchi ya kwanza afrika kuwa na taa za barabarani,tv ya rangi,magazeti zaidi ya matano ya kila siku,nchi iliyokuwa inachangia bajeti ya nchi ya omani.

Hayo ni machache tu! na ni sisi tulioirudisha nchi ile nyuma kutoka kusaidia bajeti ya maendeleo Omani mpaka Kina Raza kusadia kulipa mishahara ya wafanyakazi wa Serikali ya Zanzibar.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom