Tupia vimbwanga vya siku ya mtihani wa darasa la saba

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,257
12,877
Kwa kuanza tuwaombee dua wanetu, wajukuu zetu, wadogo zetu wanaofanya mitihani yao leo na kesho...

Turudi kwenye mada,

Nakumbuka siku moja kabla ya mtihani wangu wa darasa la saba tulikwenda shule kuosha madawati, tulikuwa na viwembe kukwangua michoro na maandishi yote kwenye madawati. aisee tulisugua na kukwangua mpaka madawati yakawa kama yamepigwa randa.

hebu na wewe tupia tukio ulilofanya wakati wa mtihani wa darasa la saba.

CL
 
Nilikuwa Bingwa wa Kucheza na Akili za wasimamizi CABED nakumbuka bado hiyo Code wakati naingia kufanya mtihani.
 
Nilimuona jirani yangu anahangaika nikawa namwachia adese ila jamaa akawa haelewi halafu msimamizi alikua mdada yuko poa tu.
 
Nakumbuka matukio mawili.
1. Kuna jamaa tulimfaulisha akaingia deko kiulaini kabisa, tulikua tunamjazia majibu au tunampa karatasi akopi ila chujio la form two lilimpenda zaidi akabaki.

2. Kuna kama alikua anatuongozea toka darasa la 3 had Ia saba, nlijua had I seko atakua anaongoza yeye ila pepper la from two hakuweza chomoka
 
hivi huko madarasa ya chini kuna vituko kama vyuoni? 😂😂😂😂 maana vyuo ni shinda sana mtu kumeza karatasi ya kibomu bila maji ni kiti rahisi sana...

elimu yangu ya msingi nilikuwa katoto sana hatukuwa na vituko kabisa
 
Rubber band zilitumika sana kutransfer chabo (unaweka kikaratasi kwenye rubber band kisha unamlenga mhusika), msimamiz alikuwa zake bize anasoma gazeti la michezo
 
Kwa kuanza tuwaombee dua wanetu, wajukuu zetu, wadogo zetu wanaofanya mitihani yao leo na kesho...

Turudi kwenye mada,

Nakumbuka siku moja kabla ya mtihani wangu wa darasa la saba tulikwenda shule kuosha madawati, tulikuwa na viwembe kukwangua michoro na maandishi yote kwenye madawati. aisee tulisugua na kukwangua mpaka madawati yakawa kama yamepigwa randa.

hebu na wewe tupia tukio ulilofanya wakati wa mtihani wa darasa la saba.

CL
Nilikuwa na kalamu za biki 3 na kompasi utazani nilikuwa na mchoro wa hesabu wa kuchora. Ila nilifaulu vizuri sana Math 47, Lugha 44, Maarifa (Siyo yamii) hapa naamanisha Geo, Sayansi, Historia, S/Kimu, S/Kilimo nk 49 nikapelekwa shule nzuri sana enzi hizo tunaita za vipaji
 
Umenikumbushà mbalii
 
Nakumbuka siku ya mtihani kwa vile tunashinda shuleni kutwa nzima, hivyo tunaenda na chakula, jamaa mmoja jina nimemsahau alikuja na machapati magumu hayo af yanaunga..... hakuwa na soda wala maji anayatafuna ivo ivo....... dah....... mademu wakamuonea huruma walimrundikia mamisosi, mzee baba alikula kinoma... kufika class tumbo likaanza kuzingua..... dadek..... kila akienda toi, akirud kabla hajakaa..... kainuka..... ilikuwa balaa. ikabidi atoke na mwalimu mmoja wakae karibu na toi hadi amalize pepa.
 
Nilikuwa na kalamu za biki 3 na kompasi utazani nilikuwa na mchoro wa hesabu wa kuchora. Ila nilifaulu vizuri sana Math 47, Lugha 44, Maarifa (Siyo yamii) hapa naamanisha Geo, Sayansi, Historia, S/Kimu, S/Kilimo nk 49 nikapelekwa shule nzuri sana enzi hizo tunaita za vipaji

Matokeo ya Primary hayabandikwi, ulijuaje?
 
Shuleni Kwetu Tulifundishwa Mbinu za Kusaidiana kwenye Chumba cha Mtihani ikiwa Mtihani umekuwa mgumu so tulifundishwa alternative way, Mfano Mko kwenye Chumba cha Mtihani na Msimamizi kakomaa kweli kapiga jicho lote..... Na mnashindwa kubadilishana Karatasi za Majibu kutoka kwa kinara wa Darasa, mloandika kwa Pensel ... mwanafunzi wa Mwisho wale Backbanja .. anadondosha kalamu au Rula alafu anagonga Dawati Kumwita Msimamizi ...so Msimamizi akiinama tu kuokota Ile Rula au Kalamu ... Tayari Wanafunzi Walioko karibu na Vinara wa Darasa wanafanya Exchange fasta Bin haraka !!!, .... Pia ukiona Msimamizi amegoma kuokota Kalamu au akatoa Ruhusa kwa Mwanafunzi kuokota ile Rula ...hapo anajitokeza Mmoja anagonga Dawati ...ili aombe Ruhusa aende kukojoa chooni Hapo piga ua lazima Msimamizi atoke na yule Msimamizi ili akamkanidhi kwa asikari amsindikize Chooni ... Hapo Darasa Lina Exchange Papers....... Miaka hiyo bhanaa acha kabisa Tulifaulu Karibia wote
Kama sio Gilman Rutihinda hyo shule!basi private!
 
Back
Top Bottom