Tupia utabiri wako kuelekea kufungwa kwa dirisha la EPL leo jumapili

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,130
Leo jumapili 22/05/2022, dirisha la EPL litakuwa linafungwa huku bingwa akiwa bado hajapatikana. Man City na Liverpool watakuwa wanawabia ubingwa. Huku kukiwa na tofauti ya point moja tu.

Man City itashuka dimbani Etihad kuwakaribisha Aston Villa huku ushindi ukiwahakikishia ubingwa.

Liverpool watashuka dimbani Anfield kuwakaribisha Wolves huku wakitaka kushinda na kuwaombea mabaya Man City. Je nani atatwaa ubingwa?

Upande wa pili, vita ya top 4 kati ya Spurs na Arsenal. Spurs watakuwa ugenini dhidi ya Norwich huku Arsenal wakiwa nyumbani dhidi ya Everton.

Na mwisho kabisa, vita ya kushuka daraja, ambapo Leeds na Burnley mmoja wapo atatakiwa ashuke ili kuungana na Norwich na Watford ambao washashuka tayari.

Leeds Utd (timu yangu hii) itakuwa ugenini dhidi ya Brentford, huku Burnley watakuwa nyumbani dhidi ya Newcastle Utd. Je nani atashuka daraja kati ya Leeds au Burnley?

Mechi zote 10 zitapigwa muda mmoja, kuanzia saa 12:00 kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Utabiri wangu:
Bingwa: Man City
Top 4: Spurs
Kushuka daraja: Leeds Utd
 
Back
Top Bottom