Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

Habari ndugu zangu. Kwa katika forum hii kuna mijadala mingi kuhusu kilimo cha miti ya mitiki ambayo inq miaka zaidi ya mitano sasa. Nimeona kuwa itakuwa na tija sana kama kuna mtu alianza kilimo cha miti hii zaidi ya mwaka mmoja hadi sasa. Tunaomba atueleze kwa ufupi changamoto za kuanza zoezi hilo. Asante
 
Tatizo lako una panda ekari 2 . Miti ukitaka udaidi panda kuanzia ekari 50.

Imagine 50×400= unakua na miti 20000.

20,000x20000= 400,000,000

Hii ina maana kila baada ya miaka 10 unavuna mil 400

Sent using Jamii Forums mobile app
Mjadala hapa ni changamoto za gharama za utunzaji, moto nk gharama za kuhudumia acre 50 kwa miaka 15 si lelemama kwa mtanzania!

Mwaka huu nimeshuhudia zaidi ya acre 1000 zimeteketea kwa moto kuanzia lwangu kuelekea madaba. Waliopita njia hii kabla mvua hazijaanza ni mashahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjambo jamani, kuna hii biashara ya Utomvu wamekuja nayo wachina kule Mafinga. Wanagema utomvu kama Ulanzi kwenye miti ya pines. Utata uko kwenye bei, wanunue kwa kilo au kwa mti? niliwashauri wanunue kwa kilo. Ikikubalika basi tutaanza kula miti yetu kuanzia miaka saba. Unagema utomvu na kujipigia hela kiulaini kabisa. Mchina hajaacha kitu
 
Malila ulini- inspire sana kny miti bless up, moto ni changamoto kubwa sana lakini mapambano yanasonga mbele.

Kuna kitu kinafikirisha sana,
Week iliyopita, kuna mteja ana hela kiasi anataka kununua miti kwa Tsh 2.5M kwa eka. Nikamwambia jamaa yangu mmoja ana eka 40 pale Igeleke Mufindi. Nikampa hesabu hizi, Chukua hiyo 100,000,000/, atoe 12,000,000/ gharama za uwekezaji.

Kisha achukue 50,000,000/ anunue shamba lenye miti midogo ya 5yrs hivi, na atoe kama 10,000,000/ matunzo ya shamba jipya. Hizi 28m twende samaki samaki tukafanye yetu, hataki. Nikamkumbusha habari ya moto, asije kuja hapa kutulilia.

Wewe ungemshaurije? Maana yy anataka bei ifike 5m kwa eka apate 200M hivi akachukue Hammer kabisaaaaaa.
 
Kuna kitu kinafikirisha sana,
Week iliyopita, kuna mteja ana hela kiasi anataka kununua miti kwa Tsh 2.5M kwa eka. Nikamwambia jamaa yangu mmoja ana eka 40 pale Igeleke Mufindi. Nikampa hesabu hizi, Chukua hiyo 100,000,000/, atoe 12,000,000/ gharama za uwekezaji. Kisha achukue 50,000,000/ anunue shamba lenye miti midogo ya 5yrs hivi, na atoe kama 10,000,000/ matunzo ya shamba jipya. Hizi 28m twende samaki samaki tukafanye yetu, hataki. Nikamkumbusha habari ya moto, asije kuja hapa kutulilia.

Wewe ungemshaurije? Maana yy anataka bei ifike 5m kwa eka apate 200M hivi akachukue Hammer kabisaaaaaa.
Ushauri mzuri sana.

Tatizo unachoona wewe sicho anachokiona yeye.

Hivi ushafikisha eka ngapi za miti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjambo jamani, kuna hii biashara ya Utomvu wamekuja nayo wachina kule Mafinga. Wanagema utomvu kama Ulanzi kwenye miti ya pines. Utata uko kwenye bei, wanunue kwa kilo au kwa mti? niliwashauri wanunue kwa kilo. Ikikubalika basi tutaanza kula miti yetu kuanzia miaka saba. Unagema utomvu na kujipigia hela kiulaini kabisa. Mchina hajaacha kitu
Malila. Habari Mkuu!!
wachina utomvu wanaufanyia kitu gani? Je wanaupeleka China?
 
Ustake chai inipalie,
piga ua galagaza sisemiiiiiiiii, we jua kila mwaka naotesha miti sana, basiiiiii.
Mkuu.

Leo nilikuwa naongea na mtu kuhusu mradi unaosimamiwa na Kilombero Teak Company.

Unapewa miche halafu wakati wa kuvuna wanakupa chako.

Ushawahi sikia huu mradi? Nini maoni yako.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjambo jamani, kuna hii biashara ya Utomvu wamekuja nayo wachina kule Mafinga. Wanagema utomvu kama Ulanzi kwenye miti ya pines. Utata uko kwenye bei, wanunue kwa kilo au kwa mti? niliwashauri wanunue kwa kilo. Ikikubalika basi tutaanza kula miti yetu kuanzia miaka saba. Unagema utomvu na kujipigia hela kiulaini kabisa. Mchina hajaacha kitu
Huu utomvu wakigema miti haikauki?
 
Mkuu.

Leo nilikuwa naongea na mtu kuhusu mradi unaosimamiwa na Kilombero Teak Company.

Unapewa miche halafu wakati wa kuvuna wanakupa chako.

Ushawahi sikia huu mradi? Nini maoni yako.?

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo la miradi kama hii na sera zetu, huishia kumliza mtu binafsi. Grl kule Mufindi walituhamasisha sana tuingie kwenye hewa ya Ukaa, tukaingia, mara paap hela hakuna, mara ofisi ya VP Mazingira inashughulikia, mpaka jioni hii hakuna kitu.

Nikija kwenye case yako, hao unaoingia nao mkataba, uwepo wao kwenye huo mradi ukoje? Maana wanaweza uza project na wakasepa, mkabaki mnang`aa macho. GRL wameuza misitu yao yote wamesepa, tuliokuwa tunapata support yao tunahemea juu juu.
 
Miaka 15 sio mchezo,hakuna miti inayokua kwa haraka?
Mosi; kuna changamoto ktk uwekezaji huu, usiweke hela kwenye miti kama cash flow yako ni ya mawazo sbb unaweza kuambulia majivu.

Sio uwekezaji wa muda mfupi, ili upate faida ni lazima uende zaidi ya miaka 15 mpaka 23 hivi. Aina ya miti na scale ni muhimu sana kuijua ili kufikia malengo.

Pili; mabadiliko ya sera, anguko la uchumi kwenye jamii linaathiri sana uwekezaji huu.

Tatu; kwa wenye pumzi huu ni uwekezaji mzuri kama sector nyingine.
 
Ipo mkuu, unapata. ila mbegu hutoka Zimbabwe mara nyingi
Mkuu kuna aina ya miti inaitwa GMELINA ARBOREA (kitaalam) ama white teak/teakmaji ni aina ya miti inayomea fasta (10yrs) na vizuri huku pwani(kisarawe) vipi kwa ukanda huo umewahi kuiskia/kuiona ...
 
Back
Top Bottom