Tupeane Taarifa benki zinazosuasua ili tutoe fedha zetu kabla hazijatangazwa mfilisi

EXIM Vepee, maana wanakaukiwa sana kwenye ATM zao
Wameanza kufunga baadhi ya matawi, niliona message walimtumia jamaa yangu kwamba tawi la babati linafungwa december 31, nadhani wameshalifunga toka last week... tusubiri tuone kama watafunga na mengine
 
Nyie hamjui mchezo unaochezwa...kufilisi benki ndogo ndogo ambazo ndo zina afueni ya moja kwa moja kwa wananchi ni mkakati wa serikali na mabenki makubwa ili ukaweke hela zako NMB au CRDB ili uwape hati wafilisi nyumba....so huja pa kukimbilia.

Kwasasa nimetoa hela zangu zote pale NMB samora, kama milioni 82 hivi cash kwa mpigo hadi Teller akaanza kurembua kumbe mm nahamishia kwangu..nimezitandaza chini ya godoro, nikiamka asubuhi nachomoa elfu 10 yangu ya kutwa naingia mtaani
Hii kamba ndefu sana
 
Bank zinaweka bondi kule BOT na hiyo bondi itafidia madeni na dhamana zote za wateja, hakuna atakaye poteza. Ingawa kutakakuwa na usumbufu /
Bora nibaki na chenchi zangu ndani. Kesho asubuhi nadamkia benki.
Bank zinaweka bondi kule BOT na hiyo bondi itafidia madeni na dhamana zote za wateja, hakuna atakaye poteza. Ingawa kutakakuwa na usumbufu /
Kwa undava uliopo unaweza zungushwa hadi umauti unakufikia kwa msongo wa mawazo.
 
Nyie hamjui mchezo unaochezwa...kufilisi benki ndogo ndogo ambazo ndo zina afueni ya moja kwa moja kwa wananchi ni mkakati wa serikali na mabenki makubwa ili ukaweke hela zako NMB au CRDB ili uwape hati wafilisi nyumba....so huja pa kukimbilia.

Kwasasa nimetoa hela zangu zote pale NMB samora, kama milioni 82 hivi cash kwa mpigo hadi Teller akaanza kurembua kumbe mm nahamishia kwangu..nimezitandaza chini ya godoro, nikiamka asubuhi nachomoa elfu 10 yangu ya kutwa naingia mtaani

Dah, JF kuna member full comedy.
 
NBC Ipo hoi. Inabebwa tu kwa sababu ina dhamana kubwa za serikali na mashirika mengi ya serikali yapo kule.

Lakini ni hoi bin taabani NBC.

Kuweni Macho.

(Nilisikia sikia kwamba ipo chini ya Baclays bank ili kuboost mtaji nk).
Acha uongo NBC iko vizuri.
 
Haki za mteja bank inapo filisiwa

Benki inapokua inafilisiwa, Deposit Insurance Board (DIB) ambayo ipo kwa mujibu wa kifungu cha 36 na 37 cha Sheria Na. 5 ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, hufanya utaratibu wa kuwalipa wateja amana zao.

Members wa bodi hiyo ni Gavana wa BOT (Mwenyekiti), Makatibu Wakuu wa Hazina wa Tanzania Bara na Visiwani, na Wajumbe wengine watatu ambao huteuliwa na Waziri wa fedha ambao ni wajuzi na wabobezi k atika masuala ya kibiashara, utaalamu au taaluma na wenye tabia na mwenendo mzuri na uzoefu ktk sekta ya zinazohusiana.

Bodi hutoa malipo ya awali kwa wateja wote ambayo kiwango cha kuanzia huwa Tsh milioni moja na nusu. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na. 198 la mwaka 2010.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao wakati wa ufilisi ni chini ya na hakizidi tshs 1.5m hao watalipwa amana zao zote kulingana na kiasi walichokuwa wameweka.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao kitakuwa kimezidi 1.5m hawa kwanza watapokea hiyo 1.5m kama malipo ya awali kisha kiasi kilichobakia watalipwa baada ya mali zote za benki kuthaminishwa na kufilisiwa.

Ni wajibu wa yeyote anayeidai benki inayofilisika kuwasilisha maombi ya madai ukiambatanisha ushahidi wa nyaraka kwa hiyo bodi.Ili fedha ziweze kulipwa kutoka kwenye "protected deposit" ya bodi ambayo vyanzo vyake vya fedha hutokana na michango ya kila mwaka kutoka kwenye hayo mabenki nk.

Ikifikia hatua ya liquidation na kuteuliwa kwa mfilisi bodi itachukua au kupokea kiwango kilichozidi kutoka kny assets za benki kilichofidiwa kwa depositors. Hii kiutaalamu tunaiita "subrogation right".

Hivyo kiwango cha 1.5m ni kiwango cha awali na sio kiwango cha mwisho,baada ya kulipwa 1.5m ,unaandika maombi ya madai ukiambatanisha nyaraka zote kwa board ambapo utalipwa pesa zako zote kupitia protected deposits.

Chanzo: Maelezo kutoka Wataalamu wa Fedha/ Uchumi

SIGNATUREReport
Like
Mkuu hiyo ipo tu kwenye maandishi... utekelezaji ni zero.Unakumbuka bank ya meridian baada ya kufilisika hadi leo zaidi ya maika 20 watu hawajambulia chochote hela zao ndio zimekwenda na maji..hawa wasubilie 1.5 za Bima nyingine zilizobaki wakeshe na kuomba ili Roho ya Bwana ifanye Miujiza
 
Standard Charter nayo haijui saa wala dk atakapo kuja mwana wa Adam kumnyakua.....

Mm hela zangu zote nimeziingiza kwenye miradi, hela niyo baki nayo ni ya kula na kununua vocha....

Kama unajiweza kuepuka na kuweka hela beki kiasi kikubwa halafu mwisho wa siku uambiwe ukachukue milion moja na laki tano bora ukafungue a/c nje ya nchi

Bank iliyo salama ni NMB
Huna Lolote.
 
Back
Top Bottom