Tupeane Taarifa benki zinazosuasua ili tutoe fedha zetu kabla hazijatangazwa mfilisi

kwahyo kufilisi benki nzima ndio usalama sio? afadhali uje geto uniibie....tutakabana ukinishinda ndo unachukua, sio huko benki nataifishwa milioni zangu na wa kugombana nae hayupo!
 
Tunaweka pesa benki kwa kuwa ni mahali salama, kutimiza malengo, fursa ya mkopo au akiba ya siku za usoni.
Lakini tunapohitaji pesa hizo furaha yetu ni kuzipata kwa wakati muafaka ili zitumike kwenye lengo kusudiwa.
Napewa fidia ya 1.5M na zilizosalia natakiwa nisubiri kwa muda husiojulikana na kwa masharti ya kupeleka vielelezo vya kutosha ili kuthibitisha dai langu.
Swala hili la kusubiri kwanza linanipotezea muda, madhara ya kiuchumi, vifo kwa kukosa pesa ya matibabu, watoto kufukuzwa shule kwa kukosa karo, kuingia kwenye madeni na hatimaye kufilisiwa na mengine mengi.
Pia kuna uwezekano wa kupoteza kabisa pesa yangu pale nitakaposhindwa kupeleka vielelezo muhimu.
Kufikia hapo nakosa umuhimu wa kuweka pesa zangu benki bora niwe kama Mzee Shinyanga aliyekuwa mmiliki wa Shinyanga hoteli mtaa wa lumumba Mwanza aliyekufa na Mamilioni ya pesa yakaungulia ndani ya nyumba.
 
kwahyo kufilisi benki nzima ndio usalama sio? afadhali uje geto uniibie....tutakabana ukinishinda ndo unachukua, sio huko benki nataifishwa milioni zangu na wa kugombana nae hayupo!
Bank zinaweka bondi kule BOT na hiyo bondi itafidia madeni na dhamana zote za wateja, hakuna atakaye poteza. Ingawa kutakakuwa na usumbufu /
 
Kuna hatari katika hilo. Mara tu watu wakipata taarifa kuwa benki yao inakaribia kufirisika, watakimbia kwenda kuondoa fedha zao. Matokeo yake benki hiyo inakuwa hatarini zaidi kuporomoka.
 
Kuna hatari katika hilo. Mara tu watu wakipata taarifa kuwa benki yao inakaribia kufirisika, watakimbia kwenda kuondoa fedha zao. Matokeo yake benki hiyo inakuwa hatarini zaidi kuporomoka.
Kwa hiyo bora lipi watangaze kabisa ili watu wajihami na vinsenti vyao, au watangaze ghafla ili watu wapoteza pesa zao.
 
Haki za mteja bank inapo filisiwa

Benki inapokua inafilisiwa, Deposit Insurance Board (DIB) ambayo ipo kwa mujibu wa kifungu cha 36 na 37 cha Sheria Na. 5 ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, hufanya utaratibu wa kuwalipa wateja amana zao.

Members wa bodi hiyo ni Gavana wa BOT (Mwenyekiti), Makatibu Wakuu wa Hazina wa Tanzania Bara na Visiwani, na Wajumbe wengine watatu ambao huteuliwa na Waziri wa fedha ambao ni wajuzi na wabobezi k atika masuala ya kibiashara, utaalamu au taaluma na wenye tabia na mwenendo mzuri na uzoefu ktk sekta ya zinazohusiana.

Bodi hutoa malipo ya awali kwa wateja wote ambayo kiwango cha kuanzia huwa Tsh milioni moja na nusu. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na. 198 la mwaka 2010.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao wakati wa ufilisi ni chini ya na hakizidi tshs 1.5m hao watalipwa amana zao zote kulingana na kiasi walichokuwa wameweka.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao kitakuwa kimezidi 1.5m hawa kwanza watapokea hiyo 1.5m kama malipo ya awali kisha kiasi kilichobakia watalipwa baada ya mali zote za benki kuthaminishwa na kufilisiwa.

Ni wajibu wa yeyote anayeidai benki inayofilisika kuwasilisha maombi ya madai ukiambatanisha ushahidi wa nyaraka kwa hiyo bodi.Ili fedha ziweze kulipwa kutoka kwenye "protected deposit" ya bodi ambayo vyanzo vyake vya fedha hutokana na michango ya kila mwaka kutoka kwenye hayo mabenki nk.

Ikifikia hatua ya liquidation na kuteuliwa kwa mfilisi bodi itachukua au kupokea kiwango kilichozidi kutoka kny assets za benki kilichofidiwa kwa depositors. Hii kiutaalamu tunaiita "subrogation right".

Hivyo kiwango cha 1.5m ni kiwango cha awali na sio kiwango cha mwisho,baada ya kulipwa 1.5m ,unaandika maombi ya madai ukiambatanisha nyaraka zote kwa board ambapo utalipwa pesa zako zote kupitia protected deposits.

Chanzo: Maelezo kutoka Wataalamu wa Fedha/ Uchumi

SIGNATUREReport
Like
Mkuu ni nyaraka zipi hizo tunaambatanisha ili kupata stahiki zetu baada ya benki kufilisiwa.
 
NBC Ipo hoi. Inabebwa tu kwa sababu ina dhamana kubwa za serikali na mashirika mengi ya serikali yapo kule.

Lakini ni hoi bin taabani NBC.

Kuweni Macho.

(Nilisikia sikia kwamba ipo chini ya Baclays bank ili kuboost mtaji nk).
Barclays bank waliinunua bank mama ya NBC ambayo inaitwa ABSA.
 
Tujuzane benki zilizo kwenye hali mbaya ambazo serikali inaziangali kwa jicho la tatu ili tukachomoe visenti vyetu haraka

Hili swala linaumiza sana mtu umejibana miaka kadhaa halafu ghafla inatangazwa benki yako imefilisika haina mtaji...

Pamoja na kwamb ulihifadhi milioni zako kadhaa lakini unalipwa milioni moja na laki tano tu...

Huku ni kupunguziana miaka ya kuishi.

Tujuzane na njia zingine za kuhifadhi fedha.

Huu uchumi unavyowayawaya haijulikani kesho benki gani itatangazwa mfilisi.

Hizi ni benki zilizo kwenye hatari ya kufilisiwa muda wowote kwa mjibu BOT.

1.Benki ya Ushirika Kilimanjaro.
2.Benki ya wanawake Tanzania TWB
3.Benki ya WananchiTandahimba.

Sasa jamani tutakimbilia wapi au ndio wanataka vyuma vikaze hadi kutabana shingoni ili tufe?
NSSF hawatoi mafao ya watu,mara ooh bank zinafungwa kwamba hata kiasi kidogo ulichohifadhi kwa kujinyima kinakwenda na maji. Huu utawala una laana huu,si bure.
 
Sasa jamani tutakimbilia wapi au ndio wanataka vyuma vikaze hadi kutabana shingoni ili tufe?
NSSF hawatoi mafao ya watu,mara ooh bank zinafungwa kwamba hata kiasi kidogo ulichohifadhi kwa kujinyima kinakwenda na maji. Huu utawala una laana huu,si bure.
Bora tunaofanya forex kuliko kuweka million 30 benki ifilisiwe upewe 1.5 million!!!
Screenshot_20180102-133502.png
 
Sitegemei kuweka pesa banki,naweka nakojua mm hata wife hawezi jua ila bank huwa nakusanyia baada ya nwezi natoa napeleka nakojua mm,mtu huna mapesa mengi unahangaika na mabenki ya kazi gani
 
Back
Top Bottom