Tuongee Asubuhi 2.1.11 7:30am LIVE ON Star TV

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Heri ya Mwaka mpya wanaJF

Katika kipindi cha kesho: Mada ni majumuisho ya matukio muhimu ya kisiasa katika mwaka 2010. Tutagusia kuhusu Mageuzi ya Kisiasa Nchini, Nafasi ya Akinamama katika mabadilio, Jukumu la wanahabari na bila shaka Katiba kwa Uchache sana...Maana kazi ilipofikia inahitaji subira na hekima pia.
Ninapendekeza LIVE TEXT fupi tu katika namba 0717 000 013. na zitasomwa LIVE.
Naomba kuwasilisha.
Yahya M
 
Ndugu Yahya, heshima yako na kheri ya mwaka mpya; hayo mengine ni mambo matamu lakini hekima na historia inahitaji tuzungumzie suala la Katiba mpya na kujadili hotuba ya Kikwete hususan kwenye suala hilo. Ningependa kuwa mchangiaji kama suala hilo litapewa kipaumbele. Hayo mengine tuyazungumze wakati mwingine, tusiogope kugonganisha vichwa vyetu.
 
heko Star TV kinara wa kuchochea mijadala iletayo tija kwa maendeleo ta nchi yetu.
 
Ndugu Yahya, heshima yako na kheri ya mwaka mpya; hayo mengine ni mambo matamu lakini hekima na historia inahitaji tuzungumzie suala la Katiba mpya na kujadili hotuba ya Kikwete hususan kwenye suala hilo. Ningependa kuwa mchangiaji kama suala hilo litapewa kipaumbele. Hayo mengine tuyazungumze wakati mwingine, tusiogope kugonganisha vichwa vyetu.

Heshima kwako pia Mkuu, sina shaka licha ya kuyaweka hayo katiba itashika usukani kwani haipekukiki...Nimenukuu makala ya Majjid aliyopost hapa na chanagamoto za WanaJF inaleta matumaini katika kujadili suala hili kwa kina. Soma Inbox pia

Yahya M
 
heko Star TV kinara wa kuchochea mijadala iletayo tija kwa maendeleo ta nchi yetu.

Ni kwa mawazo na michango ya Kipekee kutoka Jamvini sasa watanzania wanaelewa umuhimu wa mawazo chanya na matumizi ya teknolojia kuharakisha maendeleo.
Ahsante sana kwa niaba ya wapiganaji wote
Yahya M
 
hili la kinamama bado hawajaweza kusimama kwa miguu yao hata wenye uwezo bado wanataka kubebwa hivyo kuwanyima sifa ya kusema wamefaulu mfano anne makinda kafanikiwa ila si kwa nguvu zake amebebwa na mvutano wa makundi ndani ya ccm na nafasi za viti maalum bado wenye maamuzi ya mwisho kuhusu uwakilishi huo wa Wanawake ni wanaume kwani cc nyingi majority ni wanaume hivyo kuwafanya Wanawake kutokuwa na nguvu
Inayotarajiwa hata utendaji wao huwa wa kuwapendezesha viongozi wa vyama na si Wanawake waliowachagua kwa hiyo Wanawake hatua wamepiga lkn wengi si nguvu na uwezo wao kiutendaji bali wamebebwa
 
Yahya,happy new year,nikupongeze ww pamoja kituo chenu kwa kazi nzuri ya kuibua mijadala inayojenga nchi,kuhusu katiba naomba sasa tujikite kujadili mambo muhmu tunayotaka yawemo katika katiba mpya ili kuwapa uelewa wtz walio wengi.TUKO PAMOJA MKUU
 
yahya akuna taabu tutashirikiana kwa ukaribu wa hali ya juu kuhusu maendeleo ya taifa letu
 
Yahaya M.
Idea ni njema kabisa. Nadhani Mwanakijiji amesema kilichopo ndani ya akili yangu.
Kuna hili suala la public missinfomerd ambalo serikali inaplay big role hapo. angalia suala la takukuru na chenge, suala la Werema kutoa maoni tofauti na bosi wake kuhusu suala la katiba. Suala la DOWANS ambapo serikali inagoma kumtaja mmiliki wake. Hizi ndizo lines zinazosumbua wengi. Viongozi wanatofautiana ktk kauli zao na pia hawaongei ukweli. Mfano, Ngeleja anasema kuwa mgao umesitishwa lakini within a week Tanesco wanatangaza mgao nchi nzima.
hayo ni baadhi ya matukio ya kutia shaka kuhusu umakini wa viongozi na suala zima la katiba.
 
Back
Top Bottom