Tuombee upinzani Tanzania umoja, maelewano, kupendana, kuheshimiana kuaminiana na kusikilizana

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,686
13,052
Afya, ustawi na kushamiri kwa Demokrasia, Haki, Usawa na Maendeleo yoyote duniani mathalani kiuchumi, kijamii au kisiasa, huchochewa sana kwa namna moja ama nyingine, na uwepo na msukumo wa upinzani imara wenye, sauti moja , nia moja, mipango madhubuti, lengo na uelekeo mmoja.

Tumuombe Mungu wa Mbinguni kama Taifa, tena bila kushurutishwa na yeyote, awabariki sana viongozi wa upinzani. Wamefanya kazi kubwa. na bado wanafanya kazi kubwa

Mungu mwenyewe awajaalie moyo mkuu wa uvumilivu, ustahimilivu, hekima na Busara.

Awape Subra na kauli njema na thabiti za kiungwana, kwa wananchi, miongoni mwao upinzani na dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Mwenyezi Mungu abariki mipango na nia zao njema za kukusudia na kutamani kuongoza nchi.

Tuwaombee kwa ujumla wao ili ukosoaji wao ulete tija ya maendeleo, amani na mshikamano miongoni mwa waTanzania.

Contrary Tanzanian voices, deserve to be represented and managed by United and Vibrant oppositions.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Amen,

Watawala wajue kuwa, Mungu anachukia sana wizi wa kura.

Imani na mshikamano utadumu kama Sanduku la kura litaheshimiwa.

Wakubali Tume huru na Katiba mpya.

Mungu ibariki Nchi yetu nzuri TANZANIA 🇹🇿
 
Amen,

Watawala wajue kuwa, Mungu anachukia sana wizi wa kura.

Imani na mshikamano utadumu kama Sanduku la kura litaheshimiwa.

Wakubali Tume huru na Katiba mpya.

Mungu ibariki Nchi yetu nzuri TANZANIA 🇹🇿
Aimen 🙏

Mungu bariki Umoja katika mgawanyiko Upinzani.

Amen
 
Back
Top Bottom