Tunza Mkeo ili usimchoke na usimkinai

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
TUNZA MKEO ILI USIMCHOKE NA KUMKINAI

Anaandika, Robert Heriel
Baba

Ubongo wa binadamu unahitaji vitu tofauti Kila siku ili ubudurike. Kuona kitu kilekile, kusikia kitu kilekile, kunusa na kuonja kitu kilekile kunaufanya ubongo ukinaiwe na kuhisi uchovu. Unachoka.

Kijana lazima uelewe kuwa ni jukumu lako kumfanya Mkeo apendeze, kuna tofauti ya kupendeza na kuwa msafi. Kuvaa kitu kilekile kila mara au kila Siku hakumfanyi MTU apendeze kwani kitu kile kinazoeleka machoni pako na machoni pawatu. Mwanamke anaweza akawa msafi lakini asipendeze.

Ni hatari kuoa Mwanamke alafu usimpe Haki yake ya urembo, ni Haki ya Mwanamke kujiremba na kupendeza. Na Haki hizo atazipata Kwa Mumewe ambaye ni wewe.

Mahitaji ya Mwanamke ndio humfanya mwanaume kuwajibika na kutafuta Pesa Kwa nguvu zote ili kumtunza Mkewe na watoto. Mwanaume Hana excuse katika kufanya kazi Kwa juhudi na bidii zenye Akili katika Jambo hili.

Wahenga waliosema; Mwanamke anapigwa Kwa kipande cha kanga " hawakuwa wamekosea.

Mambo mawili makuu ambayo Mkeo lazima akuheshimu nayo ni;
1. Kumpenda ambapo imebeba Kumjali, kumtunza(kumhudumia), kufanya Jambo lolote kwaajili yake.
2. Kumfikisha Kileleni. Yaani kumpa mkuyenge mpaka umtoe mafuta yote mwilini.

Mwanamke ukishindwa kumhudumia na kumtunza automatically huwezi kumfikisha Kileleni kwani tayari hatakuwa na hisia na wewe, hataona unampenda, ataona haumjali tena.

Pia Mwanamke usipomtunza hata wewe mwenyewe hautamfurahia, hatakuwa mtamu tena, yaani hautamtamani. Hamtafanya tena Mapenzi Bali mtafanya ngono kama wanyama.
Mapenzi yanahusu hisia na upendo wa ndani.

Hivi kama Mwanamke kila Siku anavaa chupi ileile, nguo zilezile, msuko uleule, marashi yaleyale, Sura imemparama, ngozi imesinyaa na kunyauka kisa Hana matunzo unafikiri utavutiwa naye?

Kwa nini Mume lazima Amtunze Mkewe?

1. Kwa MASLAHI ya mwanaume mwenyewe.
Wanaume tunatamaa na vitu vizuri na virembo. Uzuri tuu hautoshi kumvutia Mwanamke bali urembo Pia. Uzuri haubadiliki hivyo unazoeleka Ila urembo unabadilika hivyo hauzoeleki.
Mavazi, Vito vya thamani, misuko ya nywele ni moja ya mambo yanayoleta mwonekano Mpya unaotuvutia wanaume.
Unamhudumia Mkeo Kwa MASLAHI yako mwenyewe.

Ili uzidi kumpenda Mkeo, azidi kukuheshimu, familia iwe imara, kupunguza migogoro ndani ya familia, kuheshimika kwenye jamii.
Huwezi heshimika kwenye jamii inayokuzunguka ilhali unashindwa kumtunza Mkeo.

Kwanza ili mwanaume aitwe mwanaume lazima aweze kumtunza Mkewe na Watoto.

2. Kwa MASLAHI ya Mkeo.
Mkeo naye anahitaji kuheshimiwa na jamii. Kumtunza ni kumpa heshimu, ni kumheshimu.

Ukiona mwanaume yeyote anasema amemchoka au kumkinai mkewe, basi Kwa Sisi tuliosoma Cuba tunamuelewa Kwa jibu moja tuu kuwa Hamtunzi Mkewe. Na ukitaka kuthibitisha jibu langu hili nenda kamuangalie huyo Mkewe alivyo, utamkuta amechoka, chakula kizuri halishwi, nguo nzuri havalishwi, misuko au nywele haziweki vizuri, hapaki mafuta mazuri, Mbaya zaidi amechakazwa kimwili na kihisia, kihisia hapati upendo Kwa mumewe, kila Siku kesi za hapa na pale,
Mwanamke wa hivyo lazima umchoke na umkinai kwani hatakuwa na uzuri wala urembo wowote.

Ni Dhambi na dhulma kubwa kushindwa kumtunza Mkeo na watoto. Kama huwezi majukumu hayo ni Bora usioe na kuzaa Watoto kuliko kufanya dhambi na dhulma hiyo.

Kama uchumi wako sio mzuri, ni vizuri wote na Mkeo mkasaidizana kuzalisha Mali ili kupunguza mzigo WA kumtunza Mkeo.
Mfano, unaweza ukamuanzishia Mkeo biashara, Isiwe yake bali yeye ndiye awe msimamizi Mkuu, kama ni mradi WA kuku au Duka au biashara yoyote.
Sehemu ya Mapato lazima kwenye basic needs za familia urembo Kwa Mwanamke lazima iwepo, urembo ni basic need Kwa Mwanamke. Hiyo ndio namna ya wao kujiamini(ingawaje sol wote Ila 99% ya Wanawake bila kujiremba hawajiamini).

Ikiwa uchumi wako uko below Milioni 5 Kwa mwezi kimapato basi unahitaji msaada wa mkeo kukusaidia kuzalisha Mali.

Zingatia; Ni jukumu la MKE wako naye kukutunza na kukuhudumia, vinginevyo naye atakuchoka na kukukinai.
Ni lazima Mkeo ahakikishe unavaa nguo Safi, unapaka mafuta mazuri, anapiga pasi nguo zako, viatu vyako ni visafi, kichwani umekaa Poah! Hapa nazungumzia vile atakavyokuona yeye unapendeza.

Moja ya viashiria kuwa Ndoa au familia Fulani iko imara ni pamoja na uvaaji wa wanandoa na rutuba ya miili Yao.
Mwanaume kuwa mchafu, kuvaa hovyohovyo, ni dalili kuwa Ndoa yake inamigogoro.

Mwanaume kuvaa akapendeza lakini mkewe yupo varuvaru ni ishara kuwa amemegeuza Mkewe kijakazi na Mtumwa.
Mwanaume anarutuba, na Mwili wenye afya alafu muda huohuo Mkewe yupo dhoofu Hali, jua hapo huyo Mwanaume hampendi Mkewe.

Baadhi ya Wanawake wamekuwa wakinipigia simu wakijaribu kueleza Tabia za ukatili na unyanyasaji wanazofanyiwa na Waume zao, mathalani,;
1. Mwanaume kuwa mchoyo.
Hii nitaianzishia Uzi kabisa maana ukiambiwa hautaamini kama kuna wanaume wapuuzi hivyo. Hivi mwanaume kamili anaweza kuficha Maziwa au kuamrisha maziwa au nyama atakula yeye pekee alafu MKE na watoto wamtazame, hautaamini lakini Ipo hivyo.

Mwanaume anakunya karibu kila Siku Bia mbili lakini huwezi amini nyumbani kwake kununua tuu juisi Mkewe na watoto wanywe ni kipengele.
Huo ni ukatili na unyanyasaji.

Au ATI mwanaume anaficha rimoti ya TV mpaka jioni atakaporudi, na akirudi Rimoti anamiliki yeye bila kujali wengine kwenye Familia, Seriously!
Kumtunza Mkeo ni kuhakikisha unatunza hisia zake, Akili yake, Mwili na Roho yake.

2. Kuwajali wengine kuliko Mkeo.
Wanawake wengi wamekuwa wakipitia maumivu Makali Kwa tabia mbaya Hii waliyonayo wanaume.
Unakuta MTU anasikiliza marafiki au wazazi wake kuliko MKE, alafu Wakati huohuo anataka amsilkilize yeye tuu, yaani kama mwendawazimu Fulani hivi asiyejitambua.

Kama kuna mtu unamjali na kumsikiliza kuliko yeyote basi hiyo ndiye unatakiwa umuoe au kuolewa naye.
Sio ulete upumbavu wako Kwa Watoto wa Watu. Unaweza usielewe ninamzungumzia nini lakini hakuna kitu kibaya kuwa kwenye Ndoa na MTU anayejali Watu wa nje kuliko Mkewe au mumewe au Watoto wake.

Mara nyingi Watu wanaopenda kusikiliza na kujali maneno ya Watu ndio wanatabia Hii. Mtu anashindwa kumsaidia Mkewe Jambo Fulani Kwa kuogopa jamii itamuonaje. Kuna wengine ni wepesi kutoa Ofa na kuweka heshima Bar lakini nenda nyumbani, utabaki mdomo wazi.

Nani atakuheshimu Kwa upumbavu wako huo?
Binti zangu, nazungumzia Binti za Tibeli hawawezi kumvumilia mwanaume wa namna hiyo. Na Mimi Baba Yao nilishawaambia nini chakufanya.

Mwanamke kama ilivyowajibu wako kumheshimu Mumeo ndivyo huyo Mumeo alivyo na wajibu wa kukutunza na kukuhudumia.
Ndio maana Sisi wanaume tumepewa misuli na nguvu kuwashinda, ndio maana tumepewa Akili kuwashinda,
Muulize Mumeo hiyo misuli na nguvu alizonazo ni zakazi gani ikiwa anashindwa kufanya majukumu yake?

Achana na wale wanaosema ATI Wanawake wanaakili kuliko wanaume, wanawadanganya, hata ninyi mnajua kuwa ninyi hamuwashindi wanaume Kwa uwezo wa Akili. Wanawaambia hivyo ili kuwatishwa mzigo wa majukumu na kukimbia nafasi Yao kama Wanaume.

Kwa wale Wanawake Wakora, wajinga na wapumbavu, ninyi maelekezo yenu Vijana WA Tibeli wanajua nini chakuwafanya, Ila wale Binti zangu walioamua kuchagua kuwa Wanawake kamili ni jukumu la mwanaume kuwatunza.

Taikon nimemaliza, mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwakweli umeongea ya mwaka mzima na nusu.subiri uone wanaume selfish watakavyokupinga
 
Kwakweli umeongea ya mwaka mzima na nusu.subiri uone wanaume selfish watakavyokupinga

Ingawaje wapo Wanawake wengi wanazingua lakini Kwa Sisi wanaume Kesi nilizonazo ni kuu mbili;
1. Usaliti, kwamba wanaume wengi sio waaminifu kwenye Ndoa, ni Chesters

2. Ubinafsi,
Uchoyo unaosababisha ukatili na unyanyasaji. Yaani kuna visa ukisikia utacheka ukidhani ni Uongo.
Ikiwa Mkeo kapika, keshafua, na kufanya kazi zote na yupo nyumbani, unajua kabisa atakuwa Lonely bado unaficha Rimoti😂😂 Haya muwekee haya internet Bundle pia Hautaki, alafu hapohapo unamuambia asiende Kwa majirani,
Hivi kuna Jela zaidi ya hiyo?
 
Back
Top Bottom