Tungempenda Mungu kama tunavyoipenda Miungu Simba na Yanga tungekuwa mbali

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna michezo ipo mingi hapa Tanzania, kama kukimbia, kuogelea, mpira wa mikono nk ila mpira wa miguu unapendwa sana.

Kumekuwa na hizi timu za watani wa jadi ambazo hucheza mpira wa miguu yaani Simba na Yanga basi mchezo huu unapendwa sana na watanzania wengi.

Kama kuna kitu nimekiona watu wengi wameweka mapenzi yao kwa mpira zaidi ndio maana nikasema "kama tungempenda Mungu kama tunavyoipenda timu ya mpira ya Simba na Yanga tungefika mbali".

Huu mchezo wa hawa watani wa jadi Simba na Yanga Kuna nguvu za Miungu ndani yake sio bure.

Watu wameweka mioyo yao yote kwa timu hii na ni kama wanaziabudu vile, yaani hizi timu zimekuwa kama ni Miungu kwa watanzania walio wengi.

Siku mpira ukichezwa huu wa hawa watani wa Jadi kuanzia mamlka za juu za nchi za Tz mpaka kwa watanzania mmoja mmoja kunakuwa na hali ya kuzitukuza..

Watu wanagombana sana hasa timu hizi zikishapata matokeo, watu wanakosa maelewano kisa utani wa timu hizi.

Utani huu ambao watu wanauona ni wa kawaida ila imepelekea watu pabaya.

Wengine wanakosa na furaha hata kufanya kazi zao wanashindwa kisa huu mpira kwa miungu Simba na Yanga.

Kuna watu wanapoteza maisha pia kwasababu ya mapenzi kwa hizi timu mbili za watani wa jadi Simba na Yanga.

Kumekuwa na nguvu za giza pia ambazo zimekuwa zikitumika katika timu hizi, ili waweze kushinda michezo yao.

Si hivyo tu hizi timu zikichezwa kuna ndoa nazo hazielewani siku hiyo maana kuna nguvu za giza zinazotokana na mapenzi ya Miungu Simba na Yanga.

Achana na hayo kuna wanaopigana mpaka kuumizana kisa Miungu ya Simba na Yanga si bure kuna nguvu za giza.

Kuna nguvu kubwa na giza ya Miungu katika hizi timu, watu wawe makini.

Pia wawe na kiasi katika kupenda.

Maana Mungu wetu ni mwenye wivu, amesema mwenyewe katika neno lake.

Pia katika zake amesema kuwa Mimi ni bwana Mungu wako usiwe na miungu mingine ila mimi.
 
Kuna watu wanamtumainia Mungu Mkuu ila bado ni maskini na wanaishi maisha matakatifu, na hawana time na dunia, hawa unawasemaje? Maana hawakufika mbali na ndoto zao wanazotaka.

Kuna watu wanazishabikia timu hizi mbili, ila ni matajiri wa kutupwa, wana Kila kitu na wengine wamefanikisha malengo yao, je hawa unawasemaje?

Mi naona maisha hayana formula kabisa, Mungu yupo, Yesu Kristo yupo sikatai ila maisha hayana formula kabisa, nimeona watu wakijaribu kuishi maisha matakatifu wakiwa hawana maendeleo, wengine wanasalitiwa na wenza wao, wengine mambo yao hayaendi kabisa but still hawajaacha imani Yao, wanatukanwa kila uchao.

Kiufupi maisha ni nidhamu, juhudi na bahati basi eidha umuamini Mungu ama la.
 
Utajiri wa Mungu haupatikani kirahisi, ila hao unawaona wanajua mbinu zao...

Tena usikute nyie masikini mnatumiwa kama kafara kwa kupenda msichokijua, kumbuka hao matajiri ndio wamewekewa pesa zao za kimiungu...
 
Utajiri wa Mungu haipatikani kirahisi, ni lazimaila hao unawaona wanajua mbinu zao...
Utajiri wa Mungu unapatikanaje? Na kwanini si kirahisi wakati Mungu wetu ni muweza yote? Tumesoma Biblia tunaona Mungu Mtakatifu akifanya ishara na maajabu, akiwapa utajiri wakina Ayubu, Daudi na Sulemani, akiwapandisha cheo wakina Morderkai na Danieli, akiwatia nguvu Samsoni na Sauli .

Ningependa kujua siri za utajiri wa Kimungu, nimesoma Mithali naona siri ni kufanya kazi kwa bidii, naona kila mtu anafanya kazi kwa bidii hasahasa watumishi na wengine wakiomba hadi masaa matatu ila maisha yao hakuna mabadiliko.
 
Neno lake linasema.

Utafute kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo mengine yote utazidishiwa.

Kabla hujafanya kazi kwa bidii kwanza uhakikishe umemtafuta yeye.

Mungu anautaratibu wake.

Mungu anakanuni zake.
 
Sawa tutaanza kulala kanisani hata mapenzi tuliyonayo kwa familia tutaacha na hela ya matumizi hatutoa tutaenda kutoa sadaka.
 
Kuna watu wanamtumainia Mungu Mkuu ila bado ni maskini na wanaishi maisha matakatifu, na hawana time na dunia, hawa unawasemaje? Maana hawakufika mbali na ndoto zao wanazotaka.

Kuna watu wanazishabikia timu hizi mbili, ila ni matajiri wa kutupwa, wana Kila kitu na wengine wamefanikisha malengo yao, je hawa unawasemaje?

Mi naona maisha hayana formula kabisa, Mungu yupo, Yesu Kristo yupo sikatai ila maisha hayana formula kabisa, nimeona watu wakijaribu kuishi maisha matakatifu wakiwa hawana maendeleo, wengine wanasalitiwa na wenza wao, wengine mambo yao hayaendi kabisa but still hawajaacha imani Yao, wanatukanwa kila uchao.

Kiufupi maisha ni nidhamu, juhudi na bahati basi eidha umuamini Mungu ama la.
Kiufupi maisha ni nidhamu, juhudi na bahati basi eidha umuamini Mungu ama la.
 
Acha kupoteza muda, huwezi kuwapangia watu kipi cha kufanya. Mpira ni starehe na si mungu kama ulivyoandika. Alafu hizi team ni za watu kwahiyo waache wafurahie team zao. Mahubiri yako peleka mitaani huko.
 
Back
Top Bottom