Mpwayungu Village
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 14,305
- 29,852
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi .
======
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao, kuna haja kufanya kila linalowezekana kubadili katiba ili kuwaondoa walimu kuusimamia.
Amesema mabadiliko wanayoyataka katika mfumo huo wa uchaguzi ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi.
Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Shirati, mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Oparesheni +255#KatibaMpya inayofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho nchi nzima.
“Pendekezo langu ni kwamba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka ujao na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, tufanye lolote linalowezekana tubadilishe Katiba na mfumo wa uchaguzi.
“Kama tusipofanya linalowezekana kuhakikisha kwamba walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi tena kama ilivyo kwa nchi nyingine, na kama ambavyo imependekezwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa ambao wanaangalia uchaguzi wetu, mjue kwamba uchaguzi huo utakuwa kama wa 2020.
“Tusipofanya linalowezekana kubadilisha Katiba na kuwa na Tume huru ya Uchaguzi badala ya hii iliyopo sasa, tujue yatatokea ya 2020. Tusipotengeneza sheria na Katiba inayokataza watu kupita bila kupingwa, mjue enguaengua haitoisha,” alisema.
Lissu alisema kudai Katiba Mpya pamoja na kubadilishwa mfumo wa uchaguzi ni jukumu la kila mtu na si la CHADEMA pekee.
“Lazima tulazimishe kufanyike mabadiliko katika eneo hili, na kama tusipolazimisha tumekwisha. Na hilo ni jukumu letu sote. Tutengeneze vuguvugu la kitaifa nchi nzima kuhakikisha hatuendi katika uchaguzi ujao bila Katiba Mpya.