Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Hajaanza leo, ni tangu akiwa waziri. Kwahiyo inabidi tumzoee, Mr. Haambiliki.
Siyo tu u waziri hata alipokuwa mwalimu ngesemera akiwa zamu akikuta watoto watapiga kelele aliwapeleka staffroom mbele na kuwapigisha magoti akija hmaster akawarudisha darasani na yeye akirudi asiwakute alikuwa anapiga kazi kwa week mbili mpk mkuu aende kumbembeleza
 
Kuwa na nia njema ni jambo moja ila njia ya kufikia malengo ya nia njema ni muhimu sana.

Hakuna uwezekano katika maisha kutumia mbinu mbaya kufanikisha jambo jema. Hivi mtu akivunja benki na kuiba pesa kwa nia ya kuwasomesha watoto yatima na kuwatibisha wagonjwa atafungwa?

Bashite alikuwa na nia njema ya kupambana na madawa ya kulevya ila alitumia njia mbaya ya kuvunja sheria kwa hiyo hakufaulu. JPM ametumia pia njia mbaya, angefuata sheria kufuta mikataba iliyosainiwa na serikali ya ccm angefanikiwa sana katika lengo lake zuri alilonalo.
  • Kufuta mikataba ya kitu gani?
  • Nia njema katika kufikia lengo gani?
  • Mikataba ipi iliyosainiwa na serikali ya CCM?
Unapoleta mada jaribu kutoa ufanunuzi au hoja iliyojitoleza ili kumpa urahisi mchangiaji. Sasa hapa hata hujaeleweka unazungumzia kitu gani.
 
Lissu lissu who's Lissu in this country..huyu mtu ni mdogo sanaa katika circle ya watu kwa hii nchi..sana sana ni mpiga maneno tu yasio na tija kwa nchi hii..hebu atulie watu wafanye kazi...hapa kazi tuu
 
kwanza nashukuru kwa maoni ya wanaojiita wasomi ni kweli wanajiita wasomi
wametoa maoni yao walioyaita ya kisomi,sasa mimi ctaki kuwanukuu ila mimi kama Darasa LA Saba natoa maoni Yangu
1:Kwanini uogope kumuita mwizi MTU wakati anakuibia
2:Kwanini tuwaogope Acasia eti watatushitaki na tutawalipa mapesa mengi
3:Kwanini tushindwe kesi kabla ya kwenda mahakamani,hapa hakuna aja ya kuogopa maana Nina uhakika tu hata wakienda mahakamani watashindwa sababu wametuibia
4:Je kama Acasia wanatuibia unafikiri wana heshimu mikataba na kama mnapoingia mkataba na mmoja akaipindisha sheria inasemaje
6:Waende tu mahakamani ila hakuna mchanga kwenda nje
7:Kwanini wasomi wengi wanatuambia kuwa tutalipa mamilioni je kama ushahidi ukionesha ni kweli Acasia wametuibia itakuwaje
Fear of unknown
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu


NADHANI HAYA MAONI NIMEYAINA MAHALA FULANI YANAFAA SANA KUMUELEZEA HUYU MHESHIMIWA TUNDU LISSU NA HUU USHAURI NI WA MWANA UPINZANI:
Kaka XXXXX umemsikia Tundu Lisu hivi ana ukweli na anachokisema?

Nimemsikia TUNDU LISSU anafahamu ukweli wote ila anafanya siasa.

Ndugu yangu XXXX tumekuwa tunaibiwa sana kupitia madini na rasilimali zingine tulizobarikiwa kwa miongo mingi.

Haya makampuni ya mabeberu silaha yao kubwa ni sheria walizojitungia ili kulinda maslahi yao pale yatakapotikiswa. Wanachofanya huwatumia maafisa wetu na viongozi waandamizi kuingia mikataba ya kinyonyaji isiyo na tija kwa Taifa.

Kwa hili lililofanyika tumejitoa muhanga kama Taifa kupigania haki yetu inayoporwa na mabeberu. Wabobezi wa sheria kama Lissu ambaye amekuwa akipigania haya kwa muda mrefu anapaswa kuwa upande wa nchi. Lakini ameamua kuwa upande wa mabeberu anawaonesha udhaifu tulionao anashabikia tunyolewe kwa chupa anayafanya hayo kwa sababu za kisiasa.

Mimi najua kiungwana ukikuta ndugu yako anapigana ingilia msaidie kumpiga adui kwanza mkoshamshinda adui ndio muonye ndugu yako asipende kuanzisha ugomvi. Hivi ndivyo walipaswa kina Lissu kufanya.

Sote tunajua sheria za mabeberu hawa zinawabeba wao katika kutuibia lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kwamba tuache kupambania haki yetu kwa kuwa sheria.

Ukiwasoma hao wanasheria wa LEAT utaona wanapigana na kutumia taaluma yao upande wa nchi na wako tayari kujitolea kuitumia taaluma yao kuitetea nchi dhidi ya mabeberu Lissu nae alipaswa kusimama upande wa nchi na sio upande wa mabeberu.

Kuna wanasiasa wanasema hii vita Rais akishinda basi amejitengenezea njia 2020 kwa hiyo wao kwa sababu hizo za kisiasa wanaona bora wasimame pamoja na mabeberu Rais ashindwe ili upepo wa kisiasa 2020 ukae vizuri.

Binafsi nakiri kuna watu walikosea huko nyuma (dumuzi) lakini kwa sasa tumeshachokoza vita na mabeberu tupigane kwa pamoja tukiwashinda hawa mabeberu ndio tutawageukia dumuzi kuwashughulikia waliotufikisha hapa. Inayoibiwa ni nchi na sisi wananchi.

Kwenye hili nasimama na Nchi yangu iwe inapatia au inakosea. Siko upande wa mabeberu.
 
Acha tunyolewe nyie si mlikuwa mkilalamikia suala ilo leo limefanyiwa kazi et tutanyolewa acha hayo mambo tupo tayar hata kunyolewa para
 
Nimekaa nikafikiria nikaona nilete humu tujadili, kumekuwa na kauli za watu wengi kuhusu makontena ya michanga yaliyozuiliwa na raisi Magufuli. Moja ya watu wanaotoa mawazo ni ndugu yetu mwanasheria lissu.
Lissu alisema kuzuia michanga ni kukimbiza wawekezaji na tutashitakiwa kwenye mahakama za kimataifa, na ana uhakika tutashindwa na kulipa fidia kubwa.
Ushauri aliotoa ni kwamba raisi angeanza kujitoa kwenye mikataba ya kimataifa kama MIGA nk.
Ndipo tudeal na hawa wawekezaji wa madini.

Kwangu Mimi naona ushauri huu si mzuri kwa sababu kuu ifuatayo,
Kujitoa MIGA, BITs na kwingineko huko ndio kufukuza wawekezaji kabisa na si wa madini Tu Bali hata sekta zingine. Makampuni mengi yamewekeza sababu tuko kwenye hiyo mikataba tukijitoa ndio yatakimbia na wala wengine hawatakuja kuwekeza kwa sababu itakuwa ni risk kwao. Sioni kama huu hi ushauri mzuri kutolewa na mwanasheria aliyebobea kama lissu.

Lissu amekuwa akisema kwamba michanga sio Mali yetu nj ya mwekezaji kulingana na mikataba, kweli sibishi hilo Ila raisi hajazuia michanga ili aitaifishe, amezuia ili kujiridhisha kwamba kinachoandikwa kwenye makaratasi ndio kilicho kwenye kontena, kama wanaandika kuna gramu 200 za dhahabu halafu kumbe ndani ya kontena zimo gramu 400 huo hi wizi, mikataba ni mibovu ndio lakini basi hata kile tunachotakiwa kukipata kama mrahaba yaani 4% tuipate sio na yenyewe tuibiwe.
Hiki ndicho anachosimamia raisi kwa sasa,
Ni maoni yangu Tu.
 
What is Lissu! Utuambie kama siyo michezo ya paka na panya ya kucheza na polisi, Lissu aliwahi kukamilisha kitu gani chenye hadhi ya kitaifa! Hutapaswi kupoteza muda na Lissu & Co.
kutowa ushauri siyo jambo baya lakini
 
Tundu lisu ni tobo haelewi lolote. Akina prof kabudi wameshaliona na kumshauri vyema jpm. Halafu anapaswa kujua kuwa kudeclare kiasi tofauti kilichomo ndani ya mchanga ni kuvunja mkataba automatically. Mi niliwaambia tundu lisu ni mweupe Wa Sheri anashindaga vi case vya kitoto sana.
Hata hili anatetea wezi mana ingekuwa yeye angeshindwa mchana kweupe mana anaona maluweluwe. Kilaza.
hapana ni ushauri tu kwani kuna ubaya i think its ok there is no problem bro just an opinion
 
Back
Top Bottom