Tundu Lissu kwenye kivuli cha Papa John Paul II!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Mitandao ya kijamii imehamaki na kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu kuwa atakwenda Chato kumuombea hayati Magufuli. Amesema akifika Chato atamuamsha Magufuli aone CCM yake. Akienda mbali zaidi amesema Magufuli ana mambo yake lakini sio mikataba ya ovyo kama huu wa bandari.

Kiukweli Lissu anavuka mstari ambao si mwepesi kibinadamu. Alishindiliwa risasi na kunusa malango ya mauti kabla Mungu hajaamua kumuokoa na kumbakisha duniani amtumikie. Sio kitu chepesi lakini ni historia ya watu wachache duniani waliwahi kusamehe wale waliofikiri walikusudia kuondoa uhai wao.

Pope John Paul II alipigwa risasi 4 mwilini na kunusa mauti lakini baada ya kupona alikutana na mtesi wake na kumsamehe baada ya hapo aliendelea kumuombea. Pope John Paul II hakubaki duniani bure zaidi ya kuwa papa aliyesafiri dunia nzima kueneza injili kuliko mapapa wengine lakini pia alishiriki kikamilifu kuhakikisha ukomunisti na Urusi inasambaratika.

Mfano mwingine ni mzee Nelson Mandela, huyu alifungwa jela miaka 27 lakini alipotoka hakulipa kisasi bali alisamehe wote na kuikomboa Afrika kusini. Huu si moyo wa kawaida.

Ndugu yetu Tundu Lissu ametamka atakwenda kumuombea mtu ambaye tuhuma za mashambulizi dhidi yake zilikuwa moja kwa moja kwake kutoka wapinzani wake. Lakini wengi tusichojua Tundu Lissu anakwenda kutimiza moja ya nguzo muhimu katika Ukristo na hasa Wakatoliki ya kuwaombea marehemu na pia fursa ya kuachilia msamaha kama sehemu ya toba kwake binafsi pia.

Hii ni safari mpya, historia mpya, kama tunavyoamini Wakatoliki kuwa mauti ni juu ya mwili tu lakini roho zi hai! Katika ulimwengu wa kiroho huko Chato linakwenda kufanyika jambo jipya.

Saa ya ukombozi ni sasa! Majira ya ukombozi ni haya! CCM wajiandae!!
 
Maombi hayo labda ayaweke kwenye maandishi na kusoma wote tukisikia,

Tofauti na hapo sioni Lissu akiruhusiwa kuingia pale!!!
 
Wakuu,

Mitandao ya kijamii imehamaki na kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu kuwa atakwenda Chato kumuombea hayati Magufuli. Amesema akifika Chato atamuamsha Magufuli aone CCM yake. Akienda mbali zaidi amesema Magufuli ana mambo yake lakini sio mikataba ya ovyo kama huu wa bandari.
Hata umsafishaje chiba; ukweli ni kwamba leo amechemka. Vyuma vilivyobaki mwilini vinamchanganya🤣
 
Lissu ni kinyonga
EhDzHAaWoAIa791.jpg
 
Wakuu,

Mitandao ya kijamii imehamaki na kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu kuwa atakwenda Chato kumuombea hayati Magufuli. Amesema akifika Chato atamuamsha Magufuli aone CCM yake. Akienda mbali zaidi amesema Magufuli ana mambo yake lakini sio mikataba ya ovyo kama huu wa bandari.

Kiukweli Lissu anavuka mstari ambao si mwepesi kibinadamu. Alishindiliwa risasi na kunusa malango ya mauti kabla Mungu hajaamua kumuokoa na kumbakisha duniani amtumikie. Sio kitu chepesi lakini ni historia ya watu wachache duniani waliwahi kusamehe wale waliofikiri walikusudia kuondoa uhai wao.

Pope John Paul II alipigwa risasi 4 mwilini na kunusa mauti lakini baada ya kupona alikutana na mtesi wake na kumsamehe baada ya hapo aliendelea kumuombea. Pope John Paul II hakubaki duniani bure zaidi ya kuwa papa aliyesafiri dunia nzima kueneza injili kuliko mapapa wengine lakini pia alishiriki kikamilifu kuhakikisha ukomunisti na Urusi inasambaratika.

Mfano mwingine ni mzee Nelson Mandela, huyu alifungwa jela miaka 27 lakini alipotoka hakulipa kisasi bali alisamehe wote na kuikomboa Afrika kusini. Huu si moyo wa kawaida.

Ndugu yetu Tundu Lissu ametamka atakwenda kumuombea mtu ambaye tuhuma za mashambulizi dhidi yake zilikuwa moja kwa moja kwake kutoka wapinzani wake. Lakini wengi tusichojua Tundu Lissu anakwenda kutimiza moja ya nguzo muhimu katika Ukristo na hasa Wakatoliki ya kuwaombea marehemu na pia fursa ya kuachilia msamaha kama sehemu ya toba kwake binafsi pia.

Hii ni safari mpya, historia mpya, kama tunavyoamini Wakatoliki kuwa mauti ni juu ya mwili tu lakini roho zi hai! Katika ulimwengu wa kiroho huko Chato linakwenda kufanyika jambo jipya.

Saa ya ukombozi ni sasa! Majira ya ukombozi ni haya! CCM wajiandae!!
Well said.
Mimi pia nimeipenda hii move
 
Back
Top Bottom