Tundu Lissu: Hamas Siyo Magaidi ila Wale waliopora Ardhi yao. Unayemuona Gaidi Wewe kwa Wenzako ni Mpigania Uhuru mfano Mandela!

Kwa hiyo Lissu kuwaunga mkono Hamas maana yake anakubali njia wanazotumia kudai uhuru wao?

Hamas wameua mpaka ndugu zetu watanzania, unasema vipi hawa sio magaidi?

Huko Chadema kutoa uhai wa wengine hata wasiohusika kwenye vita yenu, ili kudai uhuru wako ni sawa?

Kumlinganisha Mandela na Hamas ni ujinga mwingine aliofanya, Mandela aliwasamehe makaburu, Hamas wanaua mpaka wasiohusika na vita vyao na Israel.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Israel kama nchi ilitambulika rasmi na Umoja wa mataifa mwaka 1948. Lakini hiyo haimaanishi kabla yake haikuwepo.

Tanganyika ilitambulika na Umoja wa Mataifa lini? Je, inamaanisha nchi ya Tanganyika au ardhi ambayo sasa inaitwa Tanganyika, kabla ya 1961, haikuwepo?

Na kabla ya kuanzishwa Umoja wa mataifa ina maana hakukuwepo na nchi hata moja?

Canaan ilikuwepo tangu enzi kabla ya Yesu. Na ni kutoka kwenye hiyo ardhi ya Canaan, kumepatikana Jordan, Lebanon, Israel, na eneo jingine lilitengeneza sehemu ya Misri, Iraq, na Syria.
Umeambiwa hicho kipande cha Ardhi wamepewa na Uingereza, sasa Wewe unasema kabla ya 1948 walikuwa wapi!!
 
Wakati wewe unaona ametulia, mimi naona amekosa utulivu. Kama Wapalestina walikuwepo toka enzi za torati, nani hakuwepo enzi za torati? torati yenyewe anayoisema hawakupewa wapalestina, walipewa wana wa Israeli chini ya mkono wa Musa. Utawaskia watu wanasema waisraeli wale siyo hawa je, wale walienda wapi hata wasiache uzao? Tundu kachemka.
Mwambie Lissu mimi ni Rasta cha kwanza ni kupinga dhuluma na amani itawale!
 
Tundu Antipas Lissu ameuchambua kwa kina mgogoro wa Gaza na kusema Palestine ipo tangu Enzi za Torati lakini Israel ilianzishwa mwaka 1947 kwa Azimio la Umoja wa Mataifa.

Lisu anasema mwaka 1916 Uingereza ilijitwalia eneo la Mashariki ya Kati na kulitawala ikiwemo Palestine, Jordan, Syria, Saudi Arabia nk

Lissu anazidi kufafanua baada ya Vita Kuu ya kwanza palizuka Makundi ya Kigaidi mawili ya Wayahudi ambayo yalikuwa yanauwa Waarabu hasa Wapalestina na waliwahi kuchoma moto Kijiji kizima cha Wapalestina na kuuwa Wanawake na Watoto Zaidi ya 100 pia walilipua Hotel ya King David

Baada ya kuona hatari ya Wayahudi na hasa baada ya kufyekwa na Hitler na kubakia wachache Uingereza ilipelekea pendekezo UN ili sehemu ya koloni lake la Palestine wapelekwe Wayahudi. Ndipo Azimio la Umoja wa Mataifa namba 181 la mwaka 1947 likapitishwa huku Wayahudi takribani 650,000 wakipewa 56% ya Ardhi ya Palestine na Wenyeji Palestine waliokuwa takribani 1,350,000 wakiachiwa 44% ya Ardhi yao

Lisu anasema baadae Wayahudi wakajiongezea eneo na kufikisha 80% huku Wapalestina wakisongamanishwa kwenye 20% ya Ardhi yao

Na kama haitoshi 1967 baada ya kushinda Vita na Misri na Syria Wayahudi walijimilikisha 100% ya Ardhi ya Wapalestina na kuchukua pia maeneo ya Sinai na Golani

Lisu anasema Hamas ilianzishwa miaka ya 1982 na awali Wayahudi waliwatumia Hamas kuidhoofisha PLO lakini baadae Hamas walijitambua ndipo Wayahudi wakaanza kuwarubuni Fatah wawe ndio Chawa wap

Hamas walijiimarisha na Kwenye Uchaguzi Huru mwaka 2006 Hamas ilishinda viti Vya Ubunge 78 Kati ya viti 132

Lisu anasema Azimio la Umoja wa Mataifa namba 242 la mwaka 1967 linatambua uwepo wa Mataifa Mawili ya Israel na Palestine hivyo Hamas Wana Haki zote kuitetea Ardhi ya Babu zao na Watoto wao

Wewe ukiwaita Hamas ni Magaidi Wenzako Wapenda Haki na Waarabu wote wanawaita ni Wapigania Uhuru

Hata Mandela na ANC waliitwa ni Magaidi na Condolesa Rice alipokuwa Waziri wa Foreign wa USA alisema anapata tabu Wakati anapomualika Waziri mwenzake wa Foreign Affairs wa SA Kwani inabidi kwanza atengue ile kanuni ya Ugaidi wa ANC ndipo apewe visa, amesema Lisu

Lisu anasema Wayahudi kama wanaamini wataifuta Hamas.basi wanajidanganya sana

Lisu anamalizia kwa kusema kichekesho kilichopo ni Kuwa Waisrael karibia milioni 20 Wako New York Marekani Wakati pale Israel Wako milioni 7 na ushee tu na Zaidi ya nusu ya raia wote wa Jordan ni Wapalestina

Nawatakia Dominica Njema 😀
Anatoswa soon na Ulaya.

Wakikusapoti usiwakosoe
 
Hamas siku za usoni itabadilika
Screenshot_20231216-231425.png
 
Kujua thamani ya ardhi yako ni jambo moja, na njia unazotumia kuipigania ni jambo lingine.

Kumbe ndio maana serikali kuna wakati huwa inanyamaza kwenye baadhi ya mambo, ili kukwepa mitego kama huu uliomnasa Lissu.

Lissu amekurupuka.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Lisu amewafungua macho wale walioamini mgogoro huu ni wa kidini

Hongera Kwake 😀
 
Back
Top Bottom