Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,999
- 46,826
Kabla ya mwaka 1948 sio ardhi yote ya eneo hilo ilikuwa ya Waarabu Wapalestina. Sehemu ya ardhi ilikuwa inamilikiwa na Wayahudi wachache, Sehemu kubwa ilikuwa ni ardhi ya umma iliyokuwa inamilikiwa na Uingereza.
Kabla ya Utawala wa Uingereza, Palestine ilikuwa sehemu ya Ottoman Empire kwa miaka 400 tangu mwaka 1516. Kipindi hichi chote Wayahadi walikuwepo japo wachache sana kulinganisha na Wapalestina waliokuwa wengi na wakiongezeka kadri muda ulivyoendelea, hata hivyo hakukuwa na taifa rasmi linalojitegemea eneo hili. Baada ya kuanguka kwa Himaya ya Ottoman katika vita vya kwanza vya dunia ndipo eneo hilo likachukuliwa na kuwekwa kwa uangalizi chini ya utawala wa Uingereza mwaka 1920.
Mwaka 1948 Mataifa makubwa yenye nguvu ya magharibi walipoona umuhimu wa kuwa na taifa rasmi la Wayahudi ndipo wakaja na mpango wa kuwarudisha katika eneo lao la zamani la Kihistoria. Wayahudi walijipatia Sehemu kubwa ya ardhi yao ya mwanzo kutoka kwa Serikali ya Uingereza, hawakuwanyang'anya au kuwapora Wapalestina.