Tundu Lissu ahojiwa kwa kumwita Rais Magufuli "Mtakatifu". Aachiwa...

nimesoma ulicho kiandika hakika na wewe umeandika kichadema ....
Lissu na Mbowe wanajua Ben alipo




POLISI WANAHITAJI MSAADA KUTOKA KWA RAIA WEMA KUPUNGUZA UHALIFU NCHINI


KWANINI USIENDE POLISI KUTOA MAELEZO YAKO SABABU TUNAMTAKA BEN?

 
Mtakatifu ni tusi Mbele ya watenda dhambi huku kwetu Roma Italia
 
Yaan hlo jalada ndo wanalifungua sasa hv....wakat saanane kapotea mda mref sana....hili jeshi la polisi bhana....ila nashkuru Tundu Lissu washamshndwa.....
 
Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameachiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na pia polisi mkoa wa kipolisi Ilala.

Amehojiwa ni kwanini anamwita Mheshimiwa kuwa ni Mtakatifu.

Amehoji akiita "lile jina" ambalo limemfanya awe na kesi kadhaa mahakama ya Kisutu ni shida. Je, na hili la Mtakatifu ni shida?

Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu.

Amehojiwa pia kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na kurejeshwa alfajiri Central.

Amewaambia yeye ameongea na walioteswa na kuna wapo walio tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho.

RCO wa Ilala amekana na kusema kuwa watuhumiwa huwa hawateswi.

Lissu pia amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho waseme Saanane yuko wapi.

Lissu amekuwa polisi akiwa na Wakili Fred Kihwelo tangu saa nne hadi saa kumi na nusu.

Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo.
Huyu mtu anadharau na kukejeli rais wa jamhuri wakati wote. Asiwachwe kupumua hadi awe na adabu na heshima kwa kiti cha rais wa jamhuri na amiri jeshi mkuu. Kitendo cha lissu kumkejeli rais wa jamhuri ni dharau kwa wananchi.
 
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana polisi muda huu baada ya kumshikilia kwa saa kadhaa leo.

Alikuwa ameshikiliwa kwa mahojiano juu ya Press Conference aliyofanya na kuitaka serikali ieleze alipo Ben Saanane na pia kuhusu watu saba waliookotwa Mto Ruvu na kuzikwa bila uchunguzi.

Walimhoji pia kuhusu uwepo wa Makambi ya Mateso ambayo aliyatamka siku ya Press Conference.

Aidha RCO ilala amechukua maelezo yake kuhusu Ben kwa hoja kuwa Polisi Ilala wamefungua rasmi jalada la Uchunguzi kuhusu
Ben Saanane

Ameachiwa kwa dhamana ya Polisi kwa kuwekewa udhamini na mtu mmoja.
Awamu hii mengi tutayaona
 
Tafadhali Mwenye Kujua, Hivi Zile Fedha Ambazo Hutolewa Kama Dhamana Huwa Zinarudishwa Au Hakuna ?
 
Hii ya kumwita mkuu wanchi Mtukufu, mheshimiwa Tundu Lissu hakwiianza leo, ni baada tu ya kesi dikteta uchwara, kabadili Gia angani na kumwiita MTAKATIFU, mbona polisi hawajamkamata, tangia wakati huo, anakuja kukamatwa leo
 
Mi sizonje kaniita malaika ila hakupenda umalaika wangu so kanishusha nimekuwa shetani mbona hata sijamfungulia mashtaka? Kweli Mungu tuepushe kikombe hiki.
 
Kweli Tanzagiza tuna jeshi imara wanaacha kudili na majambazi na wauza madawa ya kulevya wanadili na wanasiasa wa upinzani.
 
Back
Top Bottom