Tunawezaje kuendesha nchi tukashindwa kuendesha bandari?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
943
4,458
Kama wenye nchi ni wananchi kwanini tunaaminishwa tunaweza kuendesha nchi lakini watu hao hao wanaotambia nchi inaenda vizuri wanashindwa kuendesha bandari?

Kwanini waziri mwenye dhamana anakiri bungeni kwamba yeye na watendaji wameshindwa kuendesha bandari na bado anaendelea kubaki ofisini? Kwa hiyo kila waziri anaweza akatangaza sekta anayoongoza imekwama then akabaki kuwa waziri wa ukodishaji?

Walioshindwa kuendesha bandari ni wananchi au ni serikali? Kama ni serikali na tunajua serikali iliyopo madarakani huwa inaweza kutoka kwanini isitoke kulinda sekta hiyo inayochangia asilimia 40 ya bajeti ya nchi ?
 
Kama wenye nchi ni wananchi kwanini tunaaminishwa tunaweza kuendesha nchi lakini watu hao hao wanaotambia nchi inaenda vizuri wanashindwa kuendesha bandari?

Kwanini waziri mwenye dhamana anakiri bungeni kwamba yeye na watendaji wameshindwa kuendesha bandari na bado anaendelea kubaki ofisini? Kwa hiyo kila waziri anaweza akatangaza sekta anayoongoza imekwama then akabaki kuwa waziri wa ukodishaji?

Walioshindwa kuendesha bandari ni wananchi au ni serikali? Kama ni serikali na tunajua serikali iliyopo madarakani huwa inaweza kutoka kwanini isitoke kulinda sekta hiyo inayochangia asilimia 40 ya bajeti ya nchi ?
Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”

Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.

Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.

unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.

Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.

ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.

Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.

Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?

Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.
 
Waziri unasimama kabisa unaongelea eti delays za loading and offloading, yaani kabisa tumeshindwa kuwa na means za kuondoa hii mpaka tumuarike muarabu kwenye pilau?.

Eti tunaongelea upigaji na wahuni pale bandarini, yaani Serikali yenye vyombo vyote vya ulinzi na usalama imeshindwa kabisa kuyadhibiti haya na kuifanya bandari kuwa salama?

Sasa tutaweza nini kama mambo madogo madogo kama haya yanatushinda?
 
Back
Top Bottom