Tunaweza kujifunza lipi kutoka kauli hii ya kiongozi wa New Zealand?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
My vision is straightforward:
New Zealand should be a place where people know that they can get ahead, a place where the rest of the world wants to live and a place that we can all be proud of. I've got a strong sense of where I want to take New Zealand to achieve that vision, and what we need to do to get there.


Let me start with an example.

The former Finnish Prime Minister, Esko Aho, largely untested, came into office in 1991.
He was almost immediately faced with a banking crisis.
Jobs were disappearing.
Its stock market was tanking.
Its future was hugely doubtful.
Aho's message to the Finnish people was blunt and honest:
They had big problems. No-one else was going to fix them.
And most importantly: only their brains and talent were going to take them forward.
Collectively, the people of Finland took that message on board.
They moved forward.
They transformed their economy through innovation and talent.
They put at the centre of everything they did great teachers and schools and great science, research and development.
Aho made bold decisions.
He was, I need to say, voted out at the next election.
He thought it was more important to make a difference than to get re-elected.
Though our prescription might differ, we could all take a lesson from that.


I can tell you that I have no interest in being a prime minister who just cautiously tinkers.
If you can't change things for the better, you have no business being in the 9th floor of the Beehive.
Today Finland's economy is way ahead of ours.
Twenty years ago, though, its problems were the same as ours.
Of course, twenty, and thirty, and forty years ago, we had those problems too.
We were talking about making changes even before Britain joined the common market in the early 70s.
We've talked about added value, lamb-burgers, Knowledge Waves, and NZ Inc, and yet somehow success is still just over the horizon.
People have grown tired of hearing about it. Many of them are sceptical it'll ever happen.
At a certain point, you have to stop talking about what you're going to do, and start doing it.


If Finland, Singapore and Israel can change their small economies, then we can too, in our own NZ way.
We have to bite the bullet.

Mtazamo wangu:

Wakati umefika kwa watanzania kusema imetosha! Ni wakati wa kufanya maamuzi magumu, tusikubali kubaki maskini miaka nenda rudi. Haitoshi kufanya sherehe za mabilioni kushangilia miaka 50 ya umaskini!
Hatuhitaji wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu tawala na wakurudenzi wa Idara mbalimbali za serikali ambao hawana mwamko wa kuleta maendeleo. Kiongozi ajipime mwenyewe katika muda wake wa uongozi amefanya mangapi katika kuleta maendeleo ya nchi yetu. Hatutaki viongozi wa kufungua mikutano na kufungua majengo tunaowaona kila kukicha kwenye TV. Hivi kweli wanafanya kazi za maendeleo saa ngapi? Haipiti siku bila kuona Waziri Mkuu au jk wakihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa jengo fulani, wanakata utepe, wanaweka jiwe la msingi, ama wanafungua vikao na sherehe mbalimbali. Mara ni siku ya Maji, mara siku ya Mazingira, mara siku Utamaduni n.k. Sote tunaelewa hayo yote ni masuala muhimu katika jamii, lakini kiongozi wa nchi anapokuwa 'PR' officer kwenye kila shughuli wakati hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kuwa mbaya ni dhahiri kuna walakini katika sera zetu!
Viongozi wa nchi zingine wanajitoa kuleta maendeleo, wa kwetu wamekazana kuonyesha sura zao hadharani!
 
watawala wetu inabidi washinikizwe pia kuachana na matumizi mabovu ya mali ya umma, kila kukicha tunaona misafara inamiminika, huku ni kupoteza muda, nguvu kazi pamoja na pesa ya umma . tusipokemea sasa itafikia kipindi hata houseboy wa waziri atakuwa anaendeshwa na msafara wake pia wa magari Ishirini. Sijui huko Kenya wenzetu nao wana upuuzi kama huu?!
 
Kwanza kabla ya yote, tusiwalaumu viongozi peke yao. Tukumbuke kuwa hivyo "vichekesho na usanii" wanauoufanya, wanaufanya kwa sababu sisi tunawaruhusu waendelee kufanya hivyo. Tatizo la nchi hii si viongozi peke yao tu, na sisi wananchi tunachangia pakubwa.

Tunachagua nani wa kuongoza, hatuchagui nini kitaongozwa; tunachagua watu na itikadi, hatuchagui sera na utekelezaji. Na madhara yake ndio haya. Nchi hii haitabadilika kwa kubadilisha viongozi, kwanza tubadilike sisi, tujikwamue kimawazo, tuwe na utamaduni mpya (na wala sio ile tafsiri tuliyoimbishwa shuleni kuwa "utamduni ni ngoma za asili), utamaduni wa kuwajibika, wa kutooneana haya, wa kutolindana, wa kutokubali kurubuniwa kwa chupa ya bia, kofia ya kijani au ya pink; utamaduni wa kutoziona huduma tunazotakiwa kupewa kuwa ni "ni hisani" bali haki zetu.

Kiongozi mmoja mzuri hawezi kuleta mabadiliko ya watu milioni 40 ambao nusu yao ni mbumbumbu, sio umbumbumbu wa akili bali wa mwamko. Inaonesha kama ama Watanzania tumekata tamaa au tumelemaa. Ndio maana hatusafishi mtaro wa tunapoishi mpaka aje mfadhili atusafishie, tunachangia mamilioni ya arusi lakini tunashindwa kulipa ada ya shule ya watoto wetu, tunakaa maofisini na makazini kwetu kuhesabu kalenda mshahara utatoka lini badala ya kujiuliza iwapo kile tuichoajiriwa tunakifanya ipasavyo. Na ndio maana daktari anauza madawa nje, mwalimu anauza vifaa, mtengeneza barababra anauza saruji, nondo na kokoto, mwendesha gari anauza mafuta na vipuri, trafiki analiruhusu basi bovu hata kama saa mbili baadaye litaua watu 40...kwa sababu tupo BONGO, tunaishi kibongobongo, kiujanjaujanja...halmuradi ugali umeingia ndani.

Nchi zilizoendelea hazikuendelea kwa umahiri wa kiongozi mmoja bali wananchi wote kuwajibika kama siafu, kama nyuki, kila mmoja anatekeleza wajibu wake. Viongozi wana wajibu wa kuongoza, lakini muongozwa ana wajibu wa kuwajibika. Kweli "baba na mama" katika nyumba wana wajibu wa kuwalea na kuwahudumia watoto wao, lakini na watoto nao wana wajibu wa kufuata maelekezo ya wazazi/walezi wao.
 
Back
Top Bottom