Tunaweza kubadili maisha ya wasanii wetu,kudumisha maadili na utamaduni wetu nakulinda kizazi chetu

magis

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
391
590
Hbr wapendwa.
Naomba kuwasilisha mawazo yangu ktk mahali hapa ili kutoa ninachoona kinaweza kubadili mtazamo wa jamii kwa wasanii wetu.Na pia kubadili mtazamo wa wasanii wetu ktk mbinu wanazozitumia ktk kukuza soko la sanaa yao.

Binafsi niombe kuwaomba wana jamii kutambua fursa hii iliyojitokeza ktk upande wa sanaa ambayo imetokea kuajiri vijana wetu.

Natambua umuhimu wa kuhifadhi mila na desturi zetu ktk kulinda utamaduni kitu ambacho muhimu sana.Lkn tutambue kama jamii ndio tunaolea kizazi.Hivyo aina ya malezi tunayowapa watoto wetu,ndiyo yanayobeba hulka zao ktk makuzi.Ndiyo yanayobeba matendo yao na ndiyo yanayowaelekeza aina ya mfumo wa maisha watakayoyafuata.

Kwa bahati mbaya jamii yetu imeingia ganzi kiasi sasa kila mtu kaachwa afanye atakavyo ktk familia yake tukisahau kuwa ni kuasi kidogo sana cha sumu kinachotumika kuua.

Vijana hawa tunaishi nao ktk mazingira yetu hivyo ni vyema walelewe na waelekezwe ili ubunifu wao ulinde jamii ijayo kwa kuwa hata hao vijana wa leo ndio watakaokuwa wazazi wajao hivyo wanawajibu wa kulinda utamaduni kwa faida ya vizazi vijavyo.

Kwa wasanii ,rai yangu ni kuwaomba watambue kuwa wao ni watu walio na nafasi
1:Kulinda thamani ya asili yao.Wao wanapoanza kuiga basi wanajenga sumu ya kuua utu wao (Utanzania)
2:Wanaposema wao ni kioo cha jamii basi wasibaki na wazo la aina moja ya kioo.Vipo vioo vya aina tatu

_Kinachotoa picha sawa na ya kitu husika_

_Kinachokuza picha tofauti na kitu husika_

_Kinachopunguza picha tofauti na kitu husika_

Kwa maana hiyo kioo hakisemi ukweli kwa kuwa kina toa picha unayoitaka wewe.

Cha muhimu ni wao kujitambua wanachotakiwa kukifanya ktk jamii yao.Hivyo ni wao waitazame jamii na si jamii kuwatizama wao.

3:Usanii ni biashara.Wao ni watafuta soko hivyo jamii ndio wateja wa kazi zao hivyo ni vyema

1:Wajifunze kabla ya kutoa bidhaa ambayo wao ndiyo kazi yao.

2:Wasitake kuiga utamaduni wa wengine kwa kuwa watakuwa wanapunguza kiasi cha wateja.

3:Wajiepushe na uharaka wa kupata pesa,watoe sanaa kwa vigezo ili wajitathmini na kutathmini kipato chao huku wakijizuia na matumizi ya pesa yasiyofaa.Wajifunze kutumia kipato chao kuboresha kazi zao.

Kutojihusisha na matumizi yasiofaa ya mitandao.Wasitafute waungaji mkono kwa kufanya matendo yasiyokubalika na jamii na hilo litawashushia soko.

Wajiepushe na matumizi yasiyofaa ya
Lugha
Mavazi
Wachezaji na
Mazingira wanayoyatumia.

Kujiepusha na tabia ya kutegemea uwasilishaji wa ujumbe wa aina moja(Mapenzi)
Hii ni ngumu kulingana na utamaduni wetu,wanashindwa kuuvaa uhusika na hivyo kupoteza mvuto wa mchezo au mziki.

Wanamuziki wacheze mziki na si kuwatumia Wachezaji ambao nao hushabiiana karibia miziki yote na ndio maana watu husubiri Audio na si Audio hivyo kuwapotezea pesa
Yapo mengi naomba niwasilishe haya kwa sasa.
Asanteni na karibuni
 
Back
Top Bottom