Tunawatathmini vipi Wanaharakati NCHINI na vuguvugu la kisiasa (Live on Star TV)

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za JUMAPILI wanaJF;

Leo tunaangazia harakati za makundi ya Wanaharakati NCHINI katikati ya upepo huu wa siasa zinazovuma NCHINI

Tunazungumza na
Marcus Albany - Policy forum
Ussu Malya - Mkurugenzi TGNP
Zainabu Nyumba - Mjumbe baraza kuu CUF

Tunakaribisha maoni na mtazamo wenu wanaJF kufuatia kauli za hivi karibuni kutokana na kulaumiwa Wanaharakati kuchochea vurugu.
RobotArray


Join Date : 11th February 2006
Location : Here...!
Posts : 8,538
Rep Power : 100000


[h=2]
icon1.png
Re: Tunawatathmini vipi Wanaharakati NCHINI na vuguvugu la kisiasa (Live on Star TV)[/h]
Wanasemaje juu ya mfumuko wa bei wa sasa? Dar nasikia 'sado' ya nyanya iliyokuwa inauzwa 2,000 mwezi Disemba leo inauzwa 7,000!


Tunairejea mada hii kama nilivyodokeza Jumapili ya wiki iliyopita na tutaanzaia hapa kwa hoja hii ya Mkuu INVISSIBLE na hoja nyinginezo ambazo hatukuzikamilisha:

Mada Jumapili ya leo itasomeka kama: Wanaharakati na Juhudi za kuikwamua Jamii ktk Lindi la Umaskini

Karibuni wadau kwa mawazo, michango, na maswali.​


 
Kwanza nawapongeza wanaharakati wa Tanzania katika kusimamia mambo yenye tija kwa Taifa hili.

Tatizo langu ni kwamba wanaharakati wengi wa Tanzania wamekuwa kama mavuvuzela wanapiga tu kelele bila kuchukua hatua, mfano kipindi kile cha majadiliano ya muswada wa katiba, walisema wataanzisha maandamano ili tuwaunge mkono ila wakapoozwa, wakakaa kimya.

Otherwise nawapongeza katika kutuelimisha masuala mengi ya kisiasa.
 
Jukumu la Wanaharakati ni kubadili mifumo kandamizi na kuweka mfumo wa kiliberali - Ussu Mallya
 
Pia serikali isione wanaharakati kama adui yao bali wakubali challenge kutoka kwa wanaharakati katika kulinda rasilimali za nchi.

Swali: Kwanini wanaharakati wengi wanaikosoa serikali wakiwa nje ya system na wakipewa ulaji serikalini wanakaa kimya na kuitetea serikali? Hii ni kusema kwamba wanatuaminisha kusema kwamba wengi wao wanatumia uanaharakati ili kujinufaisha?

Naomba Yahya uulize hili swali
 
Nadhani bado hatujaweza kuelewa umuhimu wa wanaharakati na pia hawajapata a fair platform ya kuweza kuwasilisha ujumbe kusudiwa.

Tuna bahati tuna wanaharakati wenye upeo mkubwa na quality ambazo ni unique, ila pia nina tatizo moja hasa kwa baadhi ya wanaharakati wa dunia ya kwanza, sometimes baadhi ya radicalists na hata fannatics huhamia kwenye uanaharakati, kiasi tena cha kuzidisha chumvi.

WE NEED TO SUPPORT OUR WANAHARAKATI, KWANI MCHANGO WAO NI MUHIMU SANA
 
Unaleta vurugu tu pale unapotaka ku hold government accountable kwa njia pekee ambayo mwananchi wa kawaida anayo ni kuandamana kwa amani hakuna njia nyingine.

Wananchi wakiandamana kudai uwajibikaji ndio wanaonekana wanafanya fujo ila wakiandamana kuipongeza serikali hapo wanaitwa raia wema au wenye kupenda amani.

Hatutaki kupachikwa vilemba vya ukoka
nataka watanzania tujulikane kama wananchi wazalendo ambao tuko tayari kwenda front line kwa kuandamana kuliko kumuachia mwaribifu mmoja kuharibu nchi yetu nzuri.
 
Yahya,

Yote yanayowakuta (na yanayoweza kuwakuta) wanaharakati hayana budi kutokea maana ni kawaida kutokea.

Wanatakiwa kuwa imara na kamwe wasikatishwe tamaa! Wajiepushe na kuegemea upande wowote, wasimame upande wa wananchi bila kujali itikadi zao.

Inasikitisha, mara zote wanaharakati wanaposimamia suala ambalo linaigusa jamii huitwa 'wachochezi', 'vibaraka wa nchi za magharibi', 'wanatumiwa na wapinzani' n.k; hawatakiwi kukatishwa tamaa na mambo kama haya kwani hayana budi kutokea.

Bahati mbaya, wanaharakati wa Tanzania wameamka ikiwa ni too late, lakini walau wameanza!

Note: Wanapoamua kutangaza maandamano ya amani basi wajiepushe kusitisha mwishoni, wanatakiwa kujua kuwa hii inawakatisha tamaa na kuwaondolea imani watanzania wanaokuwa tayari wamejiandaa kuwaunga mkono!
 
Pia serikali isione wanaharakati kama adui yao bali wakubali challenge kutoka kwa wanaharakati katika kulinda rasilimali za nchi.

Swali: Kwanini wanaharakati wengi wanaikosoa serikali wakiwa nje ya system na wakipewa ulaji serikalini wanakaa kimya na kuitetea serikali? Hii ni kusema kwamba wanatuaminisha kusema kwamba wengi wao wanatumia uanaharakati ili kujinufaisha?

Naomba Yahya uulize hili swali
Hapo penye nyekundu panahitaji ufafanuzi, ingalau muuliza swali angetoa mifano kuliko kutoa sentensi ya jumla jumla.
 
Nawapongeza sana wanaharakati mnafanya kazi nzuri na tunawaunga mkono sana lakn mkiahidi kufanya kitu tendeni hvyohvyo kwani nakumbuka kauli ya Kibamba kipindi kile tuliishangaa maana hakukua application
 
Mkuu Yahya,falsafa ya umwanaharakati ni kujitoa hata maisha yako kutetea haki za watu wote! Hawa wetu hawataki au wanaogopa misukosuko!
 
Wanaharakati wana mchango mkubwa sana katika nchi yetu hasa katika kutoa elimu ya demokrasia na haki za wananchi kitu ambacho serikali haijafanya. Inapotokea wanaharakati wanatekeleza serikali hutoa vitisho ili kukwamisha majumukumu yao. wito wangu wasikate tamaa wananchi tupo pamoja nao.
 
Hapo penye nyekundu panahitaji ufafanuzi, ingalau muuliza swali angetoa mifano kuliko kutoa sentensi ya jumla jumla.

Wanaharakati wengi haimaanishi kuwa ni wote,na wanaharakati wapo wengi sana.Tanzania,nahisi uelewa wako unadhani akina Maurus,Kibamba na Nkya ndo wanaharakati pekee,mfano kuna dada mmoja au mama ambaye ni naibu wazir wa wizara fulani aliwah kusema kuwa alikuwa mwanaharakati na alitumia muda mwingi kumponda Tundu Lissu kipindi kile cha muswada wa katiba,wapo wengi ambao tayari wameshamezwa na serikali
 
Hatua ya pili Wanaharakati wanasema watahakikisha waliohusika katika uzembe uliosababisha Vifo wanaondoka akiwemo Waziri na Naibu wake - Marcus Albany
 
Nawapongeza wanaharakati kwa kazi yao ila nataka wanijulishe.

1. Hivi Chadema wakikosa wanaweza kutoka nje na kuwapinga?.
2. Kila wakati waalimu wanatishia kugoma kwa madai yao ya msingi, ninyi wanaharakati kwanini Msisaidie CWT kufanikisha madai yao, badala ya kusubiri wagome ndiyo waingilie kati? Bora kinga kuliko tiba
 
Yahya,

Kwa nchi kama Tanzania ambapo watu wengi hawaelewi haki zao wanaharakati wana nafasi kubwa sana ya kuwajulisha watanzania kwamba adui yao mkubwa ni Serikali inayoshindwa kupamabanua na kutatua matatizo yao. Wananchi tumeipa Serikali mamlaka kwa mujibu wa katiba kusimamia raslimali za nchi na tumekubaliana kikatiba tulipe kodi lakini baadae tuone kodi yetu na raslimali za nchi zikirudi kwetu katika mtindo wa huduma kama Elimu nzuri, huduma za afya bora, maji safi na salama ya kunywa, barabara nzuri, uhakika wa masoko na chakula N.K.

Katika hayo Yayha, Ni lipi Serikali yetu imefanya kwa ufasaha kukidhi mahitaji ya mtanzania?
 
Yahya,habari za asubuhi?
mimi nawapongeza wanaharakati ila napenda kuwauliza ni kwa nini kwa masuala haya kama mgogoro wa madaktari,dowans ,mabomu gongolamboto,mv spice n,k, mbona hatuwasikii wakiomba kuonana na mkuu wa nchi au waziri mkuu ili kumuuliza hatua sahihi serikali inazozichukua,ikiwa ni pamoja na uwajibishaji wa wahusika?(maana wengi wao bado wanapeta na nyadhifa zao) hatua hii inafaa kuchukuliwa kabla ya kwenda mabarabarani,
Na endapo hawakusikilizwa na huko,basi Hatua hii itawajengea uhalali zaidi kuingia mabarabarani wakiwa na full support ya raia wema,pia itawafamya kuepuka mtego wa serikali kwamba ni wachochezi,
Pia kabla ya maandamano mnapaswa kufanya bidii kubwa kuielimisha jamii ili iwaelewe.
Kwa kina nyinyi kama taasisi na malengo yenu,kwa mikutano na vipindi kwenye tv koote nchini na sio kukaa dare salaam peke yake.

Yahya naomba uwaulize hili tafadhali
 
Jukumu la Wanaharakati ni kubadili mifumo kandamizi na kuweka mfumo wa kiliberali - Ussu Mallya
Mfumo wa kilibebari usu mallya unahamisha nguvu kutoka kwa umma na kuweka kwenye mikono ya serikali na kuwa na kitu kinaitwa nanny state ambao watu wengi wanakuwa wanahamisha uwezo wao kujiletea maendeleo na kukabidhi mikononi mwa seriakli na kuamini kuwa serikali itaweletea maendeleo na kusahau kuwa unapoipa serikali nguvu maana yake ni unakaribisha rushwa na umangimeza wa hali ya juu.

Cha kufanya ni kutengeza mfumo ambao nguvu na mamlaka ya nchi yanakuwa mikononi mwa wananchi wenyewe kuwa maendeleo yangu na familia yangu ni jukumu langu mimi mwenyewe self empowerment.

Kwahiyo kila policy inayotungwa inabidi iwalenge wananchi kwa maana ya kuwapa nguvu wananchi na sio kuipa nguvu serikali kama ambavyo inavyotokea hapa nchini kwetu wakati serikali yetu imefeli ku deliver almost ktk sekta zote za maisha kila siku inaongezewa majukumu pamoja na kwamba imesha prove failure.

Kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuanza zoezi la kuamisha nguvu za serikali na kuamishia mikononi mwa wananchi mfano mzuri tulipokaribisha wananchi kuwekeza kwenye sekta mawasiliano angalia kilichotokea wakati mashirika ya simu ya watu bunafsi yakizidi kushamiri TTCL inakufa hiyo ndio faida ya kuamisha majukumu kutoka serikalini na kwenda kwenye sekta binafsi.

Kila policy inabidi ipimwe kwa kipimo hiki how does this policy empower citizens? How does this economy policy generate growth? The best way to empower the young people in our country is to give them the best education money can buy.
 
Back
Top Bottom