Tunatakiwa kumuomba Mungu, kumsifia na kumshukuru kwa mambo gani na nyakati zipi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,658
46,322
Kumuachia Mungu matatizo yaliyo ndani ya uwezo wa kibinadamu, kumuomba upendeleo, suluhisho kwa kila jambo au kumsifia kwa baadhi ya mambo ni sawa? Au ni uchovu wa akili?

Huwa nikiwasikiliza baadhi ya watu wanaotoa kauli za kusubiria Mungu awaadhibu waonezi au wadhulumaji wao au awatatulie baadhi ya mambo naona kama watu waliojikatia tamaa kwa kila kitu na hawajui chochote cha kufanya.

Mfano umeibiwa, umedhulimiwa kitu au fedha, umedhalilishwa mbele ya hadhara, umefukuzwa kazi kwa figusu tu za boss n.k Unapomuachia Mungu unataka afanye nini hasa?

Huwa naona hata wapinzani wa kisiasa nao wanatoa kauli za kumsubiria Mungu atende jambo kwa wale wanaoona hawawatendei haki au wanashangilia jambo baya linapowapata wapinzani maadui wao kana kwamba ni malipo kutoka kwa Mungu!

Hata kama unaamini yuko Mungu anayejibu ni ujuha kumsubira au kutamani awape mikasa maadui au watesi wako, hasa kwa Wakristo ambao wameambiwa wasamehe kwa kila jambo. Ni ujuha kumuomba akusaidie upate upendeleo tofauti na binadamu wenzako katikati mambo mbalimbali, ni aina fulani ya "narcissism". Unaweza kukuta msomi fisadi wa TRA au mfanyabiashara mkubwa mkwepa kodi amevaa T-shirt "Sisi ni wale tunaosaidiwa na Bwana!" Kwamba wale masikini wanaotoseka kwa kukosa huduma nzuri kutokana na ufisadi hawasaidiwi na Bwana?

Mimi nafikiri dini zetu wakati mwingine zinatuondolea kabisa kuyaona maisha katika uhalisia wake. Kwamba mdhulumaji au Mtesi anaweza kuishia maisha yake tena yakiwa marefu sana kwa raha mustarehe kabisa hapa duniani, kwamba kuna mambo mengi yaliyo ndani ya uwezo binadamu na kwa uhakika ambayo tunapaswa kuyatatua kwa akili zetu badala ya kumuachilia na kumsubiria Mungu na kwamba sehemu kubwa ya maisha ya binadamu hata kwa wale wanaomuani Mungu yanaweza kuelezewa kwa bahati zaidi au randomness/chance/coincidence kuliko kitu kingine.
 
Kwa yote, kila siku.

Kama ni zuri, basi ni baraka zake. Kama ni baya, basi anakupitisha kwenye tanuru ili ung'ae

Kama huwezi kulielewa, muachie yeye yatushindayo ni mamlaka yake

Kasema anaweza kila kitu
 
Katika imani nyingi, sala, sifa, na shukrani kwa Mungu ni sehemu kama:

Wakati wa Msiba:
  • Kwa wengi, nyakati za majonzi na huzuni ni nyakati muhimu za kuomba na kutafakari kuhusu msaada wa Mungu.
Nyakati za Furaha:
  • Wakati wa furaha na mafanikio, ni muhimu kumshukuru Mungu kwa baraka na neema zilizopokelewa.
Nyakati za Shida na Majaribio:
  • Katika nyakati ngumu, sala na kuomba msaada na nguvu ni njia ya kukutana na changamoto na majaribu.
Nyakati za Kutoa Shukrani:
  • Kutoa shukrani kwa Mungu mara nyingine hufanyika kwa kusherehekea sikukuu, matukio ya familia, au nyakati za kushukuru kwa mambo madogo madogo maishani.
Wakati wa Kuanza au Kumaliza Kazi:
  • Kuanza au kumaliza kazi au miradi inaweza kuambatana na sala na kumshukuru Mungu kwa uwezo na fursa.
Wakati wa Kuomba Uongozi na Maarifa:
  • Wakati wa maamuzi muhimu au kipindi cha kubadilisha maisha, sala za kuomba hekima, uongozi, na uelekeo zinaweza kuwa muhimu.
Nyakati za Ibada na Ibada:
  • Sala, sifa, na shukrani zinaweza kutokea wakati wa ibada na ibada, ikiwa ni pamoja na misa, sala za jumuiya, na matukio mengine ya kidini.
 
Unaweza kukuta msomi fisadi wa TRA au mfanyabiashara mkubwa mkwepa kodi amevaa T-shirt "Sisi ni wale tunaosaidiwa na Bwana!"
Amekiuka amri ya mungu, haki yako utaipata mbinguni naye atapata mshahara wa uovu wake kwenye ule moto wa milele
 
Back
Top Bottom