Tunataka katiba mpya, hiyo iliyopo wangapi wameisoma?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Tusiende kwa mkumbo tu. Seriously ukiwauliza wana JF, at least walio na elimu ya shahada, kuwa ni wangapi wana kopi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kitakuwa ni kichekesho kwa kugundua kuwa hawatafika hata 20.

Nunua katiba muisome, vinginevyo mtaumbuka mkijidai kuchangia mada na weledi.
 
Hatuna haja ya kuisoma katiba yote ili kuunga mkono uundwaji wa katiba mpya. Watanzania wengi washa jua mapungufu ya katiba na hicho ndicho wanachokipigania. na hiyo haihitaji kuisoma katiba kujua hilo!!!!

Kwa taarifa yako hakuna nchi yeyote duniani ambayo wananchi wake walau 1 % wanaijua katiba. TZ haina tofauti na hao. Hata Kenya, au Zimbabwe siyo kuwa wananchi wake walikuwa wanaijua katiba ndiyo wakaamua kuandika mpya.
 
Katiba iliyopo haifai kwa vile ndiyo inayowezesha watawala wasio wajibika kwa wananchi kuendelea kuhujumu rasilimali za nchi, wakipendeleana wao na ndugu zao na wapambe wao huku umma wa watanzania wakishindia mlo mmoja, elimu duni na kukosa huduma za afya. Katiba iliyopo haifai maana viongozi wezi wa mali za umma wapo tu wakidunda na V8 mitaani. Anayepinga katiba mpya aidha haelewi anachopinga au ana nufaika na mfumo wa upendeleo uliopo.
 
Kuna watu hata kusoma hawajaui... Kwahiyo tungoje kwanza tuwafundishe kusoma ili wasome katiba na watwambie kama ni nzuri au mbaya???

Thats why kuna representatives.... ambao wamesoma na wametwambia mapungufu..... sasa kama wewe unaona hakuna mapungufu ebu twambie....??

People dont need kusoma katiba kujua uzuri wake wakati effects zake zinaonekana kila siku...... Hili la Raisi kuwa na mamlaka makubwa nadhani kila mtu limemgusa na hakuna ambaye haoni effects ya hii issue.....
 
Hiyo katiba iliyopo inayompa Rais umungu mtu hatuitaki, kwani unatakiwa usome katiba ndiyo ujue shida zako?? So long as wananchi wanaelewa wanavyodhulimiwa na serikali inayowaongoza, katiba mpya ni LAZIMA...
 
Kadi yako ya ccm ni namba ngapi vile ili uhakikiwe kabla ya kupewa Ukuu wa wilaya?
 
Tusiende kwa mkumbo tu. Seriously ukiwauliza wana JF, at least walio na elimu ya shahada, kuwa ni wangapi wana kopi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kitakuwa ni kichekesho kwa kugundua kuwa hawatafika hata 20.

Nunua katiba muisome, vinginevyo mtaumbuka mkijidai kuchangia mada na weledi.

kama wewe ni muislam,je umeshaisoma quran yote?au ni wachristu wangapi wameisoma biblia? viongozi wao masheikh na mapadri wamesoma vitabu hivyo na kutafsiri maana ya maandiko hayo,na hivyo huwahubiria waumini wao,hata nao wakajua general ideas za mistari iliyomo.Nini kinafanya baadhi ya watu kudhani ili kujua kilichomo ktk katiba ni lazima uwe nayo,au uwe ushaisoma?Dr slaa,JK,mnyika,pinda,kafulila,kombani wakiisoma wakatuhubiria contents na tafsiri za maana yake,haitoshi walau kujua strengths na weaknesses za katiba? Mbona mnakua majuha?
 
Katiba iliyopo haifai kwa vile ndiyo inayowezesha watawala wasio wajibika kwa wananchi kuendelea kuhujumu rasilimali za nchi, wakipendeleana wao na ndugu zao na wapambe wao huku umma wa watanzania wakishindia mlo mmoja, elimu duni na kukosa huduma za afya. Katiba iliyopo haifai maana viongozi wezi wa mali za umma wapo tu wakidunda na V8 mitaani. Anayepinga katiba mpya aidha haelewi anachopinga au ana nufaika na mfumo wa upendeleo uliopo.

Una ibara unazozijua ambazo zinasababisha maovu uliyoyataja?
 
Hatuna haja ya kuisoma katiba yote ili kuunga mkono uundwaji wa katiba mpya. Watanzania wengi washa jua mapungufu ya katiba na hicho ndicho wanachokipigania. na hiyo haihitaji kuisoma katiba kujua hilo!!!!

Kwa taarifa yako hakuna nchi yeyote duniani ambayo wananchi wake walau 1 % wanaijua katiba. TZ haina tofauti na hao. Hata Kenya, au Zimbabwe siyo kuwa wananchi wake walikuwa wanaijua katiba ndiyo wakaamua kuandika mpya.

Jifunze kufikiri sasa kama huijui katiba "kuuku" kama wakibadilisha kava wakabadili vipengele vichache si utarukaruka kama ZUZU kwa kupata KATIBA MPYA???????? usikubali kufanywa pakacha la mawazo ya wenzio, jifunze kufikiri ukishindwa tutafute tukufundishe kufikiri
 
Si Lazima wote tusome katibu, walioisome ndio hao watatueleza kuwa kuna kitu gani hakitufai, cha kwanza nikijuacho ni kwamba madaraka ya rais ni makubwa mno
 
Kwa sisi tulioisoma katiba haina budi kubadilishwa-sisi tutakuwa tunawakilisha jamii nzima-si wote wataweza kuisoma-maana kuna watu huko vijijini hata kusoma hawawezi-kama unataka kila mwananchi aisome hawa wataisomaje?
 
Katiba mpya ni muhimu hata kama watanzania hawaijui vizuri. Ila nashauri ni vizuri watanzania wajijue hii iliyopo kusudi hata wakati wa mchakato wajue ni nini cha kubadilisha. Maana haitakuwa na maana kutaka mabadiliko na wakati wa mchakato hawajui cha kubadilisha, matokeo yake itakuwa ni kupelekeshwa na wanasiasa tu.

Pia nadhani sasa imefika wakati wa watanzania kuanza kusoma hata vitabu, katiba zinazoihusu tanzania.
 
Hatuhitaji Katiba mpya ili tushinde mtihani. Hivyo usilazimishe kila mtu aisome. Watawala 'waliificha' wakagawa katiba ya CCM kila kijiji, kila shule ili wajifunze siasa ya chama. Na sasa miaka 50 ya uhuru ndo unakumbuka wote tusome katiba!

Ninachofahamu ni kwamba kila mtu kisha tawaliwa kwa katiba hii na kuona ubaya au manufaa yake. Kila mtu anaweza kukupa sentensi moja ya kile anachokitaka ktk nchi hii, Inatosha. Kazi ya ofisi husika ni kuweka maoni kama hayo ktk lugha inayokubalika. Baaasi!!
 
Tusiende kwa mkumbo tu. Seriously ukiwauliza wana JF, at least walio na elimu ya shahada, kuwa ni wangapi wana kopi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kitakuwa ni kichekesho kwa kugundua kuwa hawatafika hata 20.

Nunua katiba muisome, vinginevyo mtaumbuka mkijidai kuchangia mada na weledi.

Hivi ni watanzania asilimia wanaojua kusoma?
 
Kwa sisi tulioisoma katiba haina budi kubadilishwa-sisi tutakuwa tunawakilisha jamii nzima-si wote wataweza kuisoma-maana kuna watu huko vijijini hata kusoma hawawezi-kama unataka kila mwananchi aisome hawa wataisomaje?

Nimesema at least wenye digrii moja angalau wawe nayo kama reference, hata wasipoisoma. Kwa sasa mwenye digrii ndicho 'kiazi kikubwa'. 'Viazi vidogo' hamna hata haja ya kuijua katiba kwa sababu haiwasaidii 'sana' hata ikiandikwa upya. They can sway in the elites' way; as they don't have much to loose.
 
Katiba mpya ni muhimu hata kama watanzania hawaijui vizuri. Ila nashauri ni vizuri watanzania wajijue hii iliyopo kusudi hata wakati wa mchakato wajue ni nini cha kubadilisha. Maana haitakuwa na maana kutaka mabadiliko na wakati wa mchakato hawajui cha kubadilisha, matokeo yake itakuwa ni kupelekeshwa na wanasiasa tu.

Pia nadhani sasa imefika wakati wa watanzania kuanza kusoma hata vitabu, katiba zinazoihusu tanzania.

You are very right.
 
Wanaofananisha Kenya na Tanzania wanachemsha! kwani Kenya katiba yao wanaisoma kwenye somo la uraia mashuleni kinyume na Tanzania!

TATIZO: WENGI WETU TUNAPIGANIA TUSICHOKIJUA! Tunafuata mkumbo na upepo unakoelekea!
Zaidi ya yote wengi wanaotaka mabadiliko ya katiba hii mbovu tuliyonayo wanapigania katiba kwa maslahi yao binafsi na si kwa ajili ya Tanzania na Watanzania wake.
 
Back
Top Bottom