Mr Beast
Senior Member
- Nov 8, 2023
- 194
- 302
Haraka haraka na kwa ufupi sana,
April 26 mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar walifunga ndoa kisheria na kila April 26 ni anniversary ya Tanganyika na Zanzibar,hapa tunakubaliana wote,
Kwenye ndoa wenza hasa mke hupendelea kutumia baadhi yamajina ya mume na hili kisheria linakubalika ikiwa ni baada ya kula kiapo kwa makamishina wa viapo kama mawakili au mahakimu, nadhani na hili wote tunakubaliana.
Chukua mfano huu, Mimi naitwa Israel Yusuph Suleiman nikamuoa mrembo Hamisa Mobetho,Japo naamini haiwezekani,
Hamisa kisheria anaweza akaitwa Hamisa Yusuph Suleiman bila kupoteza Sifa ya Birthday yake nadhali na hili tutakubaliana wote,
Wala hii haina maana tarehe ya birthday ya Mobetho ashindwe kusheherekea kisa jina lake sio Hamisa Mobetho tena ila ni Hamisa Yusuph Suleiman, nadhani mmeanza kunielewa,
Wale wenye vichwa vigumu nadhani mtaelewa kwa kupitia mfano huu mujarabu kabisa.
January 12 Kila mwaka ndio siku ya Uhuru/Mapinduzi matukufu ya Zanzibar lazima washerehekee na tarehe Dec 9 ni tarehe ya Uhuru wa Tanganyika lazima isherehekewe hata kama jina la Tanganyika baada ya ndoa limekuwa Tanzania ila haki ya birthday ya Tanzania, inabaki palepale kama ilivyo kwa Hamisa Mobetho ambae Sasa anaitwa Hamisa Yusuph Suleiman.
Happy independence day, Tanzania.