Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hoja yangu ni juu ya makato makubwa ya kodi tunayokatwa ktk mishahara yetu, jamani maisha yamepanda bei sana.

Mishahara ipande, maisha magumu huku mtaani!

Pia kuna swala la WARAKA KANDAMIZI KWA WATUMISHI WA UMMA HASWA WALIMU, usiotambua elimu ya mtumishi hata kama akijiendeleza pia unanyanyasa mtumishi kutumikia miaka 9 ndipo apande daraja tofauti na miaka 3 ya awali. NB. Ufatilieni kwa undani.
 
Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.

Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.

Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.

Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema
Mie kero yangu ni umeme. Ni aibu kwa Tanzania kulia na umeme wakati tuna mito kibao tena isiyokauka! Lakini wanasiasa wanasema eti ni tech ya kizamani. Sweden mpaka sasa wanatumia hii tech mpaka wanauza umeme nje. Hoja yangu tujenge umeme wa maji mto Rufiji ambako wataalamu wanasema kuna uwezekano wa kupata mpaka mw 6,000. Hayo majenerator ni miradi ya watu na mafuta. Serikali ikipinga cdm chukua huo mradi wa Rufiji, maana najua mna uchungu na wananchi. Kama wazungu wanapewa ardhi, nanyi mpewe rufiji mwekeze
 
Tunaitaka tanganyika yetu, mambo ya kuwapa ardhi wapemba sasa basi, mambo ya ikulu yetu kukaliwa na wapemba sisi kwao hawaturuhusu sasa basi, lengo la mwalimu la kuiunganisha afrika kwa kuanza na zenzi limeshindikana sasa turudishieni tanganyika. Sera yenu ya serikali tatu siiitaki kabisa leteni tng. Muungano gani unowaruhusu wageni wakae ikulu yenu tu upuuuuuuuuuuuuuuzi
 
1.ujenzi wa barabara nyingi umesimama na wakandarasi hawajalipwa pesa zao.mfn marangu-mkuu rombo nk.2.kuwe na ukomo wa uongozi ktk teuzi za wakurugenzi mashirika ya uma.punguzo la paye
 
Mimi maoni na maswali yangu nataka niyaelekeze kwa mbunge wa Arusha Godbless Lema kama ifuatavyo:
1)Siku hizi mji wa Arusha umekuwa mchafu sana, nilitaka kujua yeye kama mbuge wetu anafanya nini kuakikisha usafi wa jiji hili la kitalii usafi una-boreka?
2)Pia ningependa kupitia hapa Jamvini(JF) atueleze ktka hii miaka yake 2 ya ubunge ni yepi kayafanikisha na yapi anayashughurikia. Sisi tuliomchagua tungependa sana kupata taharifa ya mafanikio na changamoto anazokutana nazo.

hilo ni swali la kumuuliza lema sio la kupeleka bungeni.hapa tunataka maoni/maswali kwenda kuiuliza serikali
 
Kero kubwa ni bunge kushindwa kazi zake,hasa kazi kubwa ya kuisimamia serikali,ningependa sana kama ingepelekwa hoja binafsi ya wabunge kujiuzulu,ili wananchi tufanye maamuzi thabiti ya kuchagua chombo kitakachoweza kuisimamia serikali bila kujali itikadi za uchama
 
REF; kero yangu sheria ya ajira na mahusiano mahala pa kazi ya 2004 iliyoanza kufanyakazi 2007 namba 6 na 7 vyama vya wafanyakazi na wafanyaka kwa ujumla hawana haki haki zote za kisheria amepewa mwajiri CHADEMA SOMENI HII SHERIA VIZURI KWA MAAKINI INAMAPUNGUFU MENGI BUNGE IPITIE UPYA na kwanini kuwe na shiria mbili za kazi ya WAFANYAKAZI WA UMMA NA WAFANYAKAZI WA MASHIRIKA BINAFSI? sisi sote tunatumikia Taifa letu iweje kuwe na tofauti kwenye miongozo ya kazi.
 
WILLIAMSONDIAMONDS hawataki kutengeza mkataba wa hali bora COLLECTIVE BAGGEINE AGGRIMENT uliopo umeisha 1999 mpaka leo union ikiomba kuongea na wamiliki wanaambiwa kampuni inafanyakazi kwa hasara kwakuwa SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO INAWABANA UNION NA WAFANYAKAZI WANASHINDWA LA KUFANYA { CMA} baraza la kazi waogopa kwenda ukitoka huko tajiri ankufukuza na amepewa uwezo wa kisheria kukutimua CHADEMA SEMENI HII BUNGENI KERO
 
Kero yangu ni kuhusu umeme;Kuna wakati president wetu katika awamu ya kwanza mwaka wa pili wa utumishi katika uraisi alituahidi an na kuwuahidi wawekezaji kuwa ndani ya miaka miwili kukatika kwa umeme kungebakia kuwa historia.Hakuna kilichofanyika hadi leo,mbaya zaidi badala ya serikali kuiwezesha shirika lake kununua mitambo,serikali imeamua kuziwezesha kampuni zinazozalisha umeme.Zipo taarifa kuwa tanesco wananunua umeme kwa bei juu na kuuza bei chini.Huu mpira unaochezwa baina ya serikali na wawekezaji wasioitakia mema utaendelea hadi lini,hawa wawekezaji wanaingiza vitu vyao free
'NIELIMISHENI BADO NAAMINI KUSOMA SIYO KUFUTA UJINGA,KAMA HATUTAFIKA MAHALI TUSEME SASA BASI IMETOSHA NAZIDI KUAMINI VYUONI TUNASOMA JINSI YA KUWA WAJINGA.
:A S embarassed:
 
Ni Kazi nzuri ila vinavyoongelewa sijui kama vinafanyiwa kazi na hao Wasanii wa CCM wakiongozwa na msanii wao mkuu M/kiti wa CCm na mshika pembe wake pinda kwani ni jambo la kushangaza sana kwa yeye Pinda kuona posho ni halali na kwa wabunge na kuwa haramu kwa Madaktari na watumishi wengine.

Huyo Pinda akafundishwe upya sijui kama ni mtanzania anayetujua hali tuliyonayo watanzania. Possibly anajali familia yake zaidi kuliko watanzania eti akishasaini hela za wizi kwenye umeme anajiita mtoto wa mkulima ebu awaulize watoto wa wakulima hapa tanzania kama na wao ni waizi wa kusaini posho na raia wakiwa gizani kama yeye.

Kero yangu kuu ni kupandishwa madaraja walimu kilichofanywa ni mfumo wa devide and rule. Kuna wengine wamepandishwa na na wengine hawakupandishwa madaraja na wakati wanasitahili kabisa kupandishwa Kwani wana umri wa zaidi ya miaka matano kazini. hiyo ifikishwe kwani kuna sample kutoka halimashauri kadhaa.
 
Wazo hili ni zuri sana. Endapo kero zilizoorodheshwa hapa zitafikishwa mahali pake bila kujali Serikali inazifanyia kazi au la, wabunge watakuwa wamefanya sehemu yao. Wachangiaji ni wengi hivyo nimeshindwa kusoma uzi mzima lakini nimeona na hili langu niliweke hapa, kama nitakuwa nimelirudia naomba nisamehewe bure.

Ukiingia katika wavuti ya Baraza la mitihani la Taifa (NECTA) (http://www.necta.go.tz nenda http://www.necta.go.tz/matangazo/vyeti_vilivyopotea.pdf) utaona orodha ndefu ya Watanzania walioomba 'statement of results' na kutumwa kwa mamlaka husika. Baraza hilo limekuwa likitoa 'statement of results' za Watanzania waliopoteza, kuibiwa, kuhabirikiwa na vyeti vya kidato cha Nne na Sita. Bila aibu baraza hili limekuwa likituma 'statements' hizo kwa mamlaka zinazohitaji matokeo mfano waajiri, vyuo vikuu n.k. na kusahau kuwa Watanzania hao wamesoma na wanahitaji elimu yao itambuliwe kupitia vyeti vya baraza hilo.

Vyuo vikuu vimekuwa vikitoa vyeti mbadala pale inapothibitika kuwa vyeti vimepotea, vimeungua ama vimeharibika kwa njia yoyote ile. Iweje baraza la mitihani la taifa lishindwe kufanya hivyo katika karne hii ya Sayansi na Teknolojia?

Naomba mbunge shupavu aiulize serikali kupitia Wizara ya Elimu kwa nini Baraza la Mitihani la Taifa halitoi vyeti vingine na lini litaanza kutoa vyeti hivyo kwa Watanzania waliopatwa na mikasa mbalimbali kuhusu vyeti vyao. Serikali ibanwe hadi Baraza lianze kutoa vyeti kwa Watanzania hao kwa vile ni haki yao.
 
napenda kujua hatima ya wabunge waliovuliwa uanachama na vyama vyao. Tunaambiwa, kisheria mbung akishavuliwa uanachama ndo kavuliwa na ubunge pia, sasa hawa vipi? mgombea binafsi ruksa? wao kuhudhuria vikao vya bunge sio kuvunja sheria na mwongozo wa katiba? nawasilisha hoja.
 
Walimu tanzania wana shida nyingi sana,mshahara wao ni mdogo,hawana marapurupu kama watumishi wa umma wengine,toka kitambo wizara husika na shule za sekondari washaweka zawadi kwa walimu wanaofaulisha kidato cha sita kwa kiwango cha 'a' kwa somo hivyo mwalimu husika hupewa laki tano.lakini zawadi hizi zimeshindwa simamiwa ipasavyo kuanzia wizarani mpaka wakuu wa shule,ama kweli jk alisema mbaya wa mwalimu ni mwalimu mwenzake,pesa hizo huliwa wahasibu tamisemi,au wakuu wa shule huwapa wanaojipendekeza kwao badala ya wahusika ama wahusika huzipata baada ya msuguano mkubwa,yote haya ya nini,mpangalio mzima hufisha morali ya wahusika katika hili,
 
Kero yangu kubwa ni serikali kukosa sauti kabisa katika masuala ya uwekezaji
utakuta mwekezaji anaenda kijijini anahadaa wananchi na kujipatia ardhi hatimaye anapewa hati kisha anateklekeza ardhi na hachukuliwi hatua yoyote. Mfano mzuri uko pale Mavuji Kilwa ambako kampuni ya Bioshape ya Uholanzi wametelekeza karibu hekta 36,000 na pale Kisarawe ambako vijiji 11 ardhi ya ukubwa wa hekta 9,000 imechukuliwa na Sun Biofuel ya Uingereza kulima mijatropha. Kwanini pale wawekezaji wanaposhindwa kutimiza masharti kama ya kulipa fidia, mishahara, mikataba na wenyeji hawachukuliwi hatua?
 
Natumaini Kufa kwa mpambanaji Rejia sio mwisho wa kazi nzuri aliyoianzisha... Naamini wapo makamanda ambao mtaendeleza mapambano na kutupatia majibu ya kero zetu.... Swali langu ni hili;

Ni kwanini wafanyakazi wanaoajiriwa serekalini toka taasisi binafsi na wafanyakazi hao kuhamua kuendelea kuchangia mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF (kwakuwa sheria inaruhusu), wanaendelea kukatwa asilimia 10 ya mshahara wao kama mchango badala ya asilimia 5 kama wanavyokatwa waajiriwa wengine wa serekali wanaochangia mifuko ya PPF na PSPF?

Kwakuwa serekali imeweka utaratibu wa kumchangia mwajiriwa wake asilimia 15 je si kuwaadhibu wanaohamua kuendelea na mifuko ambayo tayari wameshaanza kuichangia ili kukwepa athari za kuanza upya kwenye mifuko ya serekali jambo ambalo linaweza kuwakosesha pension baadaye kwa kutotimiza idadi ya michango inayotakiwa kwakuwa huenda wasitimize miaka inayotakiwa endapo wataanza upya kuchangia?? Je huu sio ubaguzi wa wazi kwa wafanyakazi?

 
Vile vile wabunge waambiwe wananchi wa Dodoma wanalalamika kuwa wakiwa huko wanawamalizia supu ya vichwa vya mbuzi. Hili linawauma sana wananchi wakazi wa Dodoma waliozoea kunywa supu hiyo.
 
Kuna tatizo chuo kikuu ardhi kuna wanafunzi waliomaliza mwaka 2007 na TUKALAZIMISHWA kuingizwa kwenye chuo cha KIKUU ARDHI wakati registration na mitihani ya mwisho tumefanya chini ya UCLAS (university of dar essalaam) tumeenda mahakamani na kesi tumeshinda tatizo linakuja ni Ardhi university kutoa taarifa zetu kwenda UNIVERSITY OF DAR ES SALAA tulikofanyia udahili linachukua mUda mrefu sana; hadi sasa hivi huwezi amini watu hatuna vyeti wameamua kutukomoa.

Tunasikitika sana mama yetu Regia alisema atatusaidia ila ndio hivyo tena ametangulia mbele ya haki kwa kweli tunaumia sana.
 
kero kubwa kwa wanafunzi tuliomaliza kidato cha nne mwaka jana ni kwamba tumecheleweshewa matokeo yetu,embu iojini wizara husika ni nini hasa linatatiza hili
 
Ungozi wa mkoa wa rukwa kwa kupitia halmashauri zake mpaka dakika hii bado zimewakopa wafanyakazi kwa kuto kuwalipa mshahara hususani sekta ya waalimu. Kimsingi kuto kumpa mtu mshahara na kukaa kimya pasipo taarifa yoyote nikumwingiza mtumishi katika wakati mgumu hususan kumuathiri kisaikolojia.naomba kuwauliza wahusika mjengoni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom