Tunajifunza nini kwa Kifo cha Mtoto wa Nabii Bushiri Aka Major 1?

Kwani ukiwa mtumishi wa Mungu ndio hufi au haufiwi? Kufa tumeandikiwa kila binadamu, fumbo tu ni lini utafikwa. Pamoja na hayo yote hatupaswi kuacha kuomba maana ukiomba unajibiwa kwa namna Mungu anavyoona inafaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nafsi itaonja mauti , haibagui iwe ya mtoto wa dk 1 au kijana wa miaka 30 au mzee miaka 100, uwe ni mtumishi wa Mungu unayeongoza maelfu ya watu, uwe mchumia tumbo, uwe mshirikina, ili mradi una nafsi iko siku itaachana na mwili wako.

Pia, Mungu hutenda alitakalo na analoona ni jema kwa mtu ili aendelee kutukuzwa na kuheshimiwa na kuabudiwa. Ndio maana wanadamu tunamwomba hatumshinikizi, hatumshurutishi, hatumwelekezi na wala hatumpangii maana hatuna uwezo huo na ndio maana siku zote tunaambiwa tumwombe Mungu na unapoomba jambo unaweza ukapewa kama ulivyoomba, au ukapewa lakini si kama ulivyoomba, au ukapewa lakini si kwa wakati huo huo ulioomba au unaweza usipewe kabisa, hayo yote ni maamuzi yake Mungu.
 
...kasome tena...
Ayubu, Daudi, Mwanamke aliyempokea Elisha, mama Naomi mkwewe Ruthu, Yuda mtoto wa Yakobo... Kukutajia wachache.
Hivyo unataka kusema bashiri anajaribiwa kama ayubu teh teh nakujibu Yakobo hakufiwa na mwanawe, Ibrahim hivyo hivyo, yusuph n.k kuhusu yuda watoto wake walikuwa SABABU walimkosea Mungu na hawakutubu biblia imeeleza waziwazi(walimkosea Mungu akawaua) huyo mmoja baada yakurithi mke wa kaka yake alikuwa anamwaga shahawa nje. Kwa kosa hilo Mungu akamuua
 
Inashangaza wanaojadili hii mada wote ni wapagani na wachawi. Basi wanajifarijiana kwa uzinzi na uchawi wao.
 
ukristo umepoteza kabisa mwelekeo na maana zama hizi ambapo watumishi wengi wamejikita kwenye kuhubiri faida tu ya mapesa,majumba na magari na sio ucha mungu na unyenyekevu kama miaka ya tisini na elfu mbili mwanzoni tulivyoona wakati ulokole unashika kasi!!!wakati huu wa sarakasi hizi akili ya ziada inahitajika sana tu!!!
Mtu akishaokoka na kuacha dhambi utaendelea kumhubiria kila ibada aache dhambi?
 
Kwa huyu inawezekana ni pigo kutoka kwa Mungu kwasababu ni Kanjanja.

WALAKINI, Kwa watumishi sahihi wa Mungu hilo linaitwa ''JARIBU''

Mwl. Christopher Mwakasege alipata taarifa kuwa kijana wake amefariki, wakati yeye akiwa katikakati ya Ibada jukwaani katika mkutano mkubwa. Mwl. Mwakasege hakuacha ibada ila aliendelea kuwaombea wengine na mpaka ibada ilipoisha akafunga mkutano na kuondoka kuelekea hospitalini au Mochwari.

Alipokuja kuhojiwa kuwa alijisikiaje baada ya kupata taarifa akasema ni mipango ya Mungu na shetani alitaka kumjaribu kwa kumpima kama ataacha kufanya kazi aliyoagizwa na Mungu muda ule au lah, akasema lile ni Jaribu

Btw, kila Binadamu ana jaribu lake chini ya jua.
thank you
 
Kufa ni lazima kwa mwanadamu, kila nafsi itaonja mauti, halafu kuwa mtumishi wa Mungu hakukufanyi kwamba usipatwe na majaribu, mimi simtetei lakini asipewe nafasi ya kuchukua utukufu wa Mungu kwa either miujiza n.k, biblia ipo wazi kabisa Yesu aliwaambia wanafunzi wake mtu hataishi kwa mkate ikiwemo miujiza bali mtu ataishi kwa neno litokalo kinywani mwa Mungu, Lazaro alifufuliwa na Yesu leo hii yuko wapi? miujiza ni kama chambo cha kuwavuta watu kwa Yesu, lakini watu wasiitegemee.
 
Back
Top Bottom