eumb
Senior Member
- Apr 2, 2012
- 149
- 70
Jana baada ya kusikia taarifa za kukamatwa kwa jambazi eti aliyekwenda kutubu kwa Mch Gwajima kuwa ndiye mhusika wa kumteka na kumtesa Dr Ulimboka, niliamua kurudi JF nakutafuata ile thread iliyo na video clip ya Dr Ulimboka Ushuhuda wa Dr. Stephen Ulimboka - YouTube akijeleza jinsi tukio zima lilivyotokea. Nimesikiliza na naomba kila mtu asikilize tena kwa makini halafu tujiulize maswali. Kwa upande wangu nina haya yafuatayo;
1. Dr ameeleza jinsi alivyokuwa anawasiliana mara kwa mara na mtu aliyefanikisha yeye kufika Leaders Club usiku ule. Tena anasema mawasiliano yao yalianza wakati wa mgomo wa kwanza, je kweli polisi wanaweza kutuambia mtu huyo kwa kujaribu kufuatilia kwenye mitandano ya mawasiliano hawajaweza kumpata? Kwa jinsi ilivyokuwa ni lazima yeye ndio aliunganisha watekaji.
2. Dr anakumbuka watu waliomteka na hata wakati wa kumtesa hawakuwa kumi na mbili, tena walimuamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, sasa hilo jambazi la Kenya limepata wapi figure ya 12?
3. Dr anasema walipomtesa walikuwa wanamwambia unatusumbua sana wakati tulishasaini makubaliano, je makubaliano yapi? Unafikiri ni ya wagonjwa na madaktari? Hapa, je watanzania tuliwahi kufanya nao makubaliano? Hapa, makubaliano pekee ninayoyakumbuka ni kati ya Madaktari na serikali, correct me if i'm wrong!
4. Haingii akili eti Jambazi linataja idadi ya waliokwenda kumteka na kumtesa lakini hawakumbuki kwa sura!! Jambazi mzoefu kutoka nje ya nchi aliyekodiwa kwa special task hawezi kuwakumbuka waliompa ajira? Kwa kazi kama hizo lazima kuna makubaliano fulani ya awali sometimes part payment na watu waliomuunganisha kuja kufanya kitendo kama hicho, kweli hata hao hawakumbuki?