Tunaendelea,kumbe tukiamua tunaweza,kusini tumeonesha mfano huo leo hii na dunia imeona

mafisadi waliangalie sana hili,yan wasipokuwa makini tutaona roho hivi hivi kwa mali aliyotupa mola,binadam siku hizi hawaogopi mungu,wao kila ikitokea rasilimali tuh huigeuza yao na kusahau ya kwamba mungu pia aliweeka kwa manufaa yetu sote viumbe wake,bila huruma wao wanachukua ten percent wanakimbilia kuficha uswiss,sasa ili iweje??vizazi vinavyokuja vitarajie nini katika ardhi hii??
Wamekuwa watu wa hovyo kabisa.
 
patamu hapo.....je, watapeleka umati wote huo mabwepande kuwang'oa meno?

jeuri hiyo waitoe wapi??
Vichwa vinawawaka moto huko waliko,wameamuru tbccm isiseme chochote juu ya aibu ya huku,ila haijalish ujumbe watanzania na dunia wanaupata kisawa sawa.
 
JK ameona bora akimbilie Paris kuomba mbinu za kuwashawishi wanamtwara ila naona hali imekuwa tete, hawa jamaa wapo siliasi
 
watanzania wamechelewa sana kudai haki zao za msingi,nafikiri ufike wakati tudai maji,elimu,hospitali bora,miundombinu nk
 
hapa hakitoki kitu na tukimaliza hili tunaanza kudai reli yetu aliyoiba mzee mchonga
 
watu wameghairi moja kwa moja,
dhulma imepitiliza mipaka kwa kweli.
Kaka Mkubwa sio tu kwamba Dhuluma imepitiliza,hapana!!! Ila Wadanganyika wa jana (1961-2005),ni Kizazi cha Analog!! Na kizazi cha leo(2005-2015) ni DIGITAL!! so wanachoshindwa kutofautisha,kina Nape, Mwigulu,na Mzee Mangula, ni hapo...!Fikiri mtu kama Waziri "Muhongo",na Mkuu wa Mkoa "Simba Kalia" Matamko walio yatoa,mwanzoni kabisa Wanakusini walipoanza kuonyesha Hisia zao! Yalikua ni Matamko ya Kejeli,Vitisho na Dharau.Naamini kwamba Wanakusini ni watu waelewa,na kwamba Wanachokihitaji,ni kuelezwa kwamba ni kwanini,Gesi isafirishwe kwenda Dar,na kama itasafirishwa Wao,watanufaikaje? Sasa Viongozi tulio nao ni MAJUHA KALULU,wanaofanya kila kitu ni Siasa. Muhongo na Simba Kalia, vyeo walivyo navyo nani asiejua kua ni Asante SALMA.,hawakuchaguliwa na wananchi ndio maana wanaweza Kuwatukana jinsi watakavyo!!! Shame on Them..ufike wakati sasa wananchi tuseme Enough is Enough!! Ile Dhana ya kudanganywa kwamba Gesi ni Keki ya Taifa na wakati ni Keki ya Watawala, na Wake, watoto,na Vimada wao,,!!! Tuipuuze!!! Shime Watanzania "Tushikamane" na kamwe,tusikubali kuyumbishwa wala kugawanywa na MAFISADI (CCM ) kwa tofauti ya Itikadi ya VYAMA au Dini,kwani Hawa jamaa ni WALAINI sana,tukiamua hawana nyimbo. We Fikiri watu wanaotegemewa,kuokoa Meli ya MV Ccm,inayokaribia Kuzama eti ni NAPE na MWIGULU.angalao kidogo Nape,some time huwa na Aibu lakini kwa. MZINZI MWIGULU,ambae siamini kama zinamtosha unategemea hapo Jahazi litaokolewa? GESI KWANZA VYAMA BAADAE!!!!!! Hili Game ndio kwanza limeanza sijui kama watamudu hii kasi ya Watanzania waliokua Gizani,na sasa Wamengamuka.Poleni Ccm.
 
Sawa endelea kunipuuza lakini nakuambia ukweli ueleweki unachosimamia naona unaitisha serikali huku umejificha nyuma ya Laptop.
mkuu naona ur mindset is still stuck on analog ages.unadharau harakati na hoja za msingi zinatolewa via social media!!.hizo laptop/desktop/ mobile devices ndio zilipelekea kuangushwa kwa mababa wa u-dictetor duniani (muamar gaddaffi,ben ali,hosn mubarak).ulitaka THE BIG SHOW atumie mbinu kama walizotumia wazee wetu zamani walipokuwa wanapigana na mkoloni.?pitia hapa.http://www.nbcnews.com/technology/technolog/how-internet-brought-down-dictator-125222 ujifunze faida na madhara ya mitanadao ya kijamii na uache kudharau hoja zinazo kufikia toka ktk laptop.
 
Pongezi kwenu wanamtwara!! yatupasa nasi wa kanda zingine tuwaunge mkono kwa kuendeleza mapambano ya kizalendo ya kulinda raslimali za nchi yetu kwa maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida.
 
653d4j.jpg
1234ggi.jpg
 
Kwa maelezo yako inaonyesha huu ulikuwa mkutano wa CUF kujiimalisha kusini siyo Watu wa kusini kudai manufaa ya gesi ambayo Mora amewapatia. Move hii mnaifanya kijingajinga sana. Sijui kwa kukosa elimu au nini.

Watu ambao siyo Magreater thinker watakusapoti lakini kama mimi naona hili swala litawashinda. Mimi huwa sisapoti kila kitu hata kama nakipenda. Ninapenda wanamtwara wapewe haki zao lakini sijapenda namna mlivyofanya move hii hata akama waliokuwa wakihutubia wangekuwa chadema. Achaneni na mwaswala ya vyama. Fanyeni hili swala kiharakati zaidi. Fikirieni kutokea kichwani si kwingineko. Jifunzeni kutoka mahali pengine wanavyofanya kupigania haki kwa maswala ambayo hayahusu chama.

Eti unasema mlimuelekeza ya kusema. Kwa nini hamkusema nyinyi wenyewe na wanaharakati wenu wa gesi? Eti tumewapa wapeleke bungeni? Kwani huyo mbunge wa Lindi ni mwakilishi wenu? Au Sakaya ni nani kusini?

Baada ya mwakilishi wenu kusingizia safari wakati akijua anachokiogopa ni kuhudhuria ule mkutano na kusema maneno ambayo yangeweka hatma yake ya siasa ndani ya CCM mahali pabaya ( Naamini hiyo ndiyo sababu ya msingi. Kwani huko Dar alienda kufanya nini ilihali akijua kuna mkutano muhimu jimboni?). Mngefanya vyema mngeandaa hoja zenu kisha kukodi magari na kuandamana mpaka wizara usika. Mkitoka hapo ikuru mkitoka hapo Bungeni. Kwa kuwa kuna wananchi wengi wanawaunga mkono mngeona jinsi maandamano hayo yatakavyonoka na kuitingisha serikali ya Nkwere.

Wana kusini msipopambana kwa kutafuta namna bora ya kutetea haki zenu bila kuogopa hakuna atakayesimama kuwatetea. Nawasihi pambaneni. Piganieni haki yenu. Vita hii siyo ndogo. Lakini hakuna serikali duniani iliyewahi kupambana na nguvu ya umma ikashinda. Mabomu hayatawamaliza. Risasi hazitawamaliza. Mungu atalinda viumbe vyake! Kuna watu hawafi kwa uchawi, wala risasi na wala mabomu. Wanakufa kwa wakati wa Mungu tu. Ndiyo maana huwezi ona vita inayomaliza Askari wote! Nyinyi mtashinda. Sisi tupo nyuma yenu tukiwatia Moyo mkuu.

Good analysis...!!
 
Kama kweli kwa hali hii hakuna atakae guswa na kutafakari jinsi ya kuthamini matakwa ya wananchi huko mbeleni sijui nini kitatokea.Ila hakika hali inatisha wananchi wamehamasika sana hawataki tena umaskini.
 
mkuu naona ur mindset is still stuck on analog ages.unadharau harakati na hoja za msingi zinatolewa via social media!!.hizo laptop/desktop/ mobile devices ndio zilipelekea kuangushwa kwa mababa wa u-dictetor duniani (muamar gaddaffi,ben ali,hosn mubarak).ulitaka the big show atumie mbinu kama walizotumia wazee wetu zamani walipokuwa wanapigana na mkoloni.?pitia hapa.How the Internet brought down a dictator - Technology on NBCNews.com ujifunze faida na madhara ya mitanadao ya kijamii na uache kudharau hoja zinazo kufikia toka ktk laptop.

mkuu huyo ndugo ni mvivu sana wa kufikiri,cha kushangaza hata lugha ya picha anashindwa kuielewa yani,anashangaza sana.
 
pongezi kwenu wanamtwara!! Yatupasa nasi wa kanda zingine tuwaunge mkono kwa kuendeleza mapambano ya kizalendo ya kulinda raslimali za nchi yetu kwa maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida.
tupo pamoja mkuu,,

mapambano dhidi ya mafisadi bado yanaendelea.
 
Back
Top Bottom