Tuna washauri wangapi wa kimataifa kwenye uchumi? Mwenye kujua anijuze tafadhali

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,344
Kama swali linavyo uliza hapo juu.

Ningependa kufahamishwa taifa letu lina washauri wangapi wa kimataifa katika uchumi na kutoka nchi gani?

Mwenye kujua anijuze tafadhari.
 
Washauri wapo. Kuna Mzee mmoja aliyekufa juzi juzi hapo ana Degree 7. Ila nilishangaa et ni Afisa tu.. hata Umeneja hana.
 
Hata walete maprofesa wa uchumi kutoka mbinguni, Tanzania haiwezi kuendelea bila ya katiba mpya, dira ya maendeleo na misingi imara na endelevu.

Ukishajenga msingi. Unaweka dira. Huu upuuzi wa Rais katoa hela za kujenga shule, sijui katoa hela kujenga hospital ufe.

Tunataka kusikia serikali unajenga miundombinu ili hata Rais mwingine akija awe serikali na sio mtu na wazimu wake.

katiba nzuri na dira ya maendeleo inampa mipaka raisi asijione kajenga yeye, ili kuzuia mwingine mwenye kupenda sifa na ubinafisi kubomoa mifumo ya wwaliomtangulia.
 
Mambo ya uchumi ni magumu hata usa na ulaya yanawasumbua. Huu Tanzania ili uwe mtu wa uchumi inabidi uwe uchawa na phd za mchongo,bila kusahau kuvaa tai na skafu yenye bendera ya nchi 🤣🤣🤣
 
Degree 7 za makaratasi hazina msaada kwa taifa, kama hata mtu mwenyewe hatujawahi msikia
 
Kama swali linavyo uliza hapo juu.

Ningependa kufahamishwa taifa letu lina washauri wangapi wa kimataifa katika uchumi na kutoka nchi gani?

Mwenye kujua anijuze tafadhari.
= tafadhali

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Tuna wachumi waliobobea, ilibidi tuwatumie wao vilivyo.

Tuna Professor Lipumba, Tuna Professor Assad, Tuna Dr. Mpango. Tuna Kikwete, wote hao wana uzoefu mpana sana kwenye masuala ya uchumi.

Bila ya kumsahau Zitto Kabwe.
 
Hata walete maprofesa wa uchumi kutoka mbinguni, Tanzania haiwezi kuendelea bila ya katiba mpya, dira ya maendeleo na misingi imara na endelevu.

Ukishajenga msingi. Unaweka dira. Huu upuuzi wa Rais katoa hela za kujenga shule, sijui katoa hela kujenga hospital ufe.

Tunataka kusikia serikali unajenga miundombinu ili hata Rais mwingine akija awe serikali na sio mtu na wazimu wake.

katiba nzuri na dira ya maendeleo inampa mipaka raisi asijione kajenga yeye, ili kuzuia mwingine mwenye kupenda sifa na ubinafisi kubomoa mifumo ya wwaliomtangulia.
Umemaliza
 
Back
Top Bottom