Tumuunge mkono Waziri Ndumbaro kwenye uzalendo wa kuvaa jezi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,316
12,614
Simba na Yanga zimeanzishwa miaka ya 1930's, lakini hazijawahi kushinda mataji makubwa ya Afrika kwenye mpira. Baadhi ya sababu za kushindwa kushinda mataji ni pamoja na kuhujumiana zenyewe kwa zenyewe zinapokutana timu za kigeni. Huu ni utamaduni/utani wa jadi ni mbaya sawa na utamaduni wa kujisaidia vichakani, kukeketa wanawake, kujufungulia majumbani kwa wakunga wa jadi, au kuowaoza mabinti wadogo.

Ni kweli Simba na yanga wana utani wa jadi lakini utani ambao hauzisaidii timu zetu haufai kuendelezwa, ukome kama vile mashabiki walivyokoma kunyonya matiti ya mama zao.

Timu zetu ni lazima zizuie hasara za goli la ugenini linatokana na timu zetu kuruhusu kufungwa nyumbani kwa kumuongezea nguvu mchezaji wa 12 (mashabiki) kwenye viwanja vywa nyumbani (home advantage). Mtanzania yeyoyote anaeshangilia, kupokea na kuvaa jezi ya timu ngeni anapunguza nguvu za mchezaji wa 12 wa timu yetu ya tanzania; hana nia safi.

Kuna wachambuzi uchura wanatumia nafasi ya kupewa nafasi kwenye chombo cha habari cha mtu kupingana na serikali kuhusu swala la uzalendo kwenye michezo, eti hawaoni uhusiano kati ya mtu kuvaa jezi ya timu ngeni na matokeo ya timu yetu ya tanzania.


View: https://www.youtube.com/watch?v=3dhqS4wt4N0

Turuhusi waandishi wenye degree pekee kwenda hewani kuzungumza na public. Hawana akili kabisa.
 
Back
Top Bottom