Tumshauri Kijana mahusiano yamemvuruga sana kaathirika kisaikolojia

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,293
Wakuu,

Kijiwen nnakopata riziki kwa mbele kdg kuna kijiwe Cha bao na draft huwa wanapaki bodaboda, Nikiwa Sina kazi huwa napenda kukaa pale Kupiga story na kubadilishana mawazo na vijana.

Kuna dada mmoja ni single mother yuko kwny 25s huwa anatembeza uji wa lishe, mi mwnyw Ni mteja wake na namfahamu kua kazaa na boda mmojawapo pale kijiweni.

Mwaka Jana mwanzoni hivi niko kijiweni na uyo boda na wengineo, jamaa mmoja akaulizia yule dada wa uji skuhz haonekani. Ana hamu na uji wake ataupataje.

Wadau wakasema sahv anamimba kubwa TU anaweza jifungua MDA wowote hawez kuja kijiweni. Ikanibd kumtania yule boda nnaejua alizaa nae kua "mwamba naona umeamua kuongeza familia,utaki masihara kabisa kutimiza agizo la mungu"

Jamaa akasema ile sio mimba yangu Ni ya uyu boda mwenzangu,kammyooshea kidole boda mwenzie pembeni.Basi nikampa pongezi, jamaa kashukuru,akasema ndio anajiandaa kuitwa baba kwa mara ya kwanza,sahv kampumzisha ili ajiandae kujifungua.

Nikauliza harusi lini Sasa, tuandae michango kabisa, boda akasema yeye haoi Ila anafurahia Sana kuitwa baba, watalea tu mtoto na mpk sahv anatoa matunzo yote ya mimba vzur kule kule binti anakoishi mwnyw.

Nikauliza kwann asiishi nae na hajaoa bado?, akasema ile mimba iliingia bahat mbaya tu, yule sio mwanamke wa ndoto zake, atamhudumia uko uko aliko. Anae mwanamke mwngn wa malengo yake anaesomea unesi.
Basi nikaheshimu maamuz yake. Ikaisha hivyo.

Mwezi JUNE nikaskia yule binti kajifungua salama mtoto wa kiume, nilipoonana na yule boda nikampa mkono wa pongezi maana kwangu pia keshanipa Kama Mara 2 hivi kwa wife alipojifungua. Jamaa kashkuru sn na maisha yakaendelea.

Nmekuja kuonana na yule boda Tena Juzi juzi mwaka huu pale kijiweni, nikamchukua anipeleka mahali njiani namuuliza jamaa vipi mda mrefu sn huonekani kijiweni, yule mwanao na mama ake vp wanaendeleaje?.

Akanambia Bro mambo ya mahusiano Ni Changamoto Sana, tukifika ntakusimulia vizuri. tumefika saiti ameanza nisimulia kua Binti yule baada ya kujifungua,aliamua kwenda kwa wazazi wake kisarawe kuugulia uko na Yeye akawa anapeleka huduma zote muhimu uko kila baada ya siku 2 au 3.

Sasa baada ya afya ya binti kutengamaa, Wazazi wake wakamrudisha town na kumleta Moja kwa moja nyumban kwake akilazimishwa aishi nae pale pale kwa lazima kwasababu kamzalia mtoto.

Akaona ni kama vile anaozeshwa kwa lazima, akamtoa binti na wanae wawili kwa nguvu na kuwatupia kila kilicho chao nje na akafunga chumba chake.

Baadae binti na wazazi wake wakampeleka polisi ustawi wa jamii kua kamshambulia na kumjeruhi mkewe,kamdhalilisha na kumtelekeza nje na damu yake mtoto mchanga wa miez 2.

Boda alipoitwa polisi akasema Hana lengo la kumuoa, makubaliano Yao tangu mwanzo walee TU mtoto yeye atatoa huduma zote muhimu, huyu binti ana kwake kapanga, arudi akakae uko uko ili walee tu mtoto.

Polisi wakatishia kumuweka ndani kwa kosa la kumshambulia mwili na kumdhalilisha mwanamke na kusema kua wasipoyamaliza nje na ile familia. Hii kesi itaenda mpk mahakamani na atafungwa jela.

Ikabidi boda awe mpole kwa mwanamke na wazazi wake ili asiwekwe ndani, Kisha baada ya kutoka polisi wakarudi na yule binti nyumbani kwenye chumba walichopanga. Hawaongeleshani zaidi ya siku 3, akitoka kaacha ela ya matumizi, akirud kila mtu kivyake.

Baadae akili ikamuijia kua Hapa ni Kama anaozeshwa kwa lazima, afu na mwezi unaofata mpenz wake wa malengo chuoni anarud likizo, akimkuta yule mwanamke pale nyumban ataharibu mahusiano yake.

Basi akaamua kupanga chumba kingine, sehem nyngn na kuhamia kule rasmi, chumba kile kamwachia yule binti na mwanae ndani na kila kitu.
Alibeba nguo zake TU.

Ikawa anapeleka matumizi TU anaondoka zake,hakai Wala halali pale.Baada ya wiki hakai pale, Tena mwanamke na wazazi wake wakaenda polisi kua boda kaitelekeza ile familia. Boda kaitwa polisi hakuenda, akafatwa kijiweni na kukamatwa Kisha kuwekwa ndani, kosa Ni kuitelekeza familia.

Kajitetea Sana polisi hawakumwelewa, wakasema ayamalize na Ile familia wao hawana tatizo. Ikabidi ajishushe kua anarud nyumbani rasmi, basi akatolewa ndani baada ya kukaa karibu masaa 10. Akarud nyumban kishingo upande.

Alivorud nyumban Moyo wake ukawa mzito sn kukaa Tena na yule mwanamke,ukzingatia hasira za kupelekwa polisi na kuwekwa ndani. Ikabd jamaa atoroke tena na kwenda kwao mbeya na kubadili laini ya Simu, akawa hapatikani kila sehemu, uko mbeya alikaa kwa miez 2 Bila mawasiliano yyt yule mwanamke.

Aliporudi majirani wakamwambia yule binti kasomba kila kitu ndani na kahama pale kapeleka kwenye chumba chake. Basi boda akaelekea kwa binti kumjulia Hali mwanae na kupeleka matumizi.

Kufika kwa binti akakutana na sura ya mwanaume mtu mzima Kama mwarabu amekalia Kochi lake kanyoosha miguu, ikabd amsalimia kistaarabu yule mzee. Kisha akajifanya Kama anaulizia binti alipo. Kajibiwa kaenda sokoni. Kaaga na kuondoka. Kumtafuta kwny Simu, katukanwa matusi mengi kua yeye alimkataa mtoto.

Huyo mtoto sio wake Tena,
Keshapewa baba mwngn na ndo
Uyo aliemkuta kwake na kwa taarifa yake uyo ndo baba wa halisi wa mtoto,mwanzoni alikosea na jina keshabadilishwa tayari kwaiyo aondoke Apo haraka akaendelee na maisha yake.

Ikabidi awatafte wazazi wa binti,
Nao wakasema hivo hivo kua jamaa keshaenda kuonekana nakalipa faini ya uchafuzi na kakamilisha mila bado ndoa TU. Ikabd awe mpole na kuondoka kuendelea na shughuli zake.
Basi nikampa pole,story yake inasikitisha,kashukuru na kanirudisha,kila mtu kashika 50 zake.

Sasa leo asbh saa 2 hivi Niko kijiweni,
Yule binti nikamuona kwa mbaali anapita na mtoto mgongoni anauza uji wake kama kawaida, ikabd nimuite ili anipe uji wa buku pia nimpongeze kwa kujifungua.

Baada ya kunimiminia uji na kumpa mkono wa pongezi, Kwa furaha akanipa mtoto wake ili nimbebe kidg, kweli nikambeba kwa bashasha zote na kumsifu kua mwanae ana afya njema. Siku zote hatuletei uji,kumbe uji wote anampa mwanae akue vizuri.
Akasema huwa anapita Sana Sema hanikuti dukani,anawauzia sana vijana wangu.

Mimi akili yote iko Kumuangalia mtoto kwa makini,Nikagundua mtoto Ni mweupe sana na shombe shombe tupu Hadi nywele. Wakati boda mwnyw Ni black pure Tena ile ya kinyakyusa mbeya,nae binti Ni pure black, Sijui kabila gani yule.

Akilini nikakumbuka ile story ya boda kua alimkuta jamaa mtu mzima Kama mwarabu nyumbn kwa binti. Nikimuangalia mtoto namuona kabisa Ni shombe shombe wa kiarabu huyu,Hadi nywele.

Akilini Nikajua kweli Hapa
BODA ALIPIGWA KITU KIZITO Kichwan
Kwa macho ya kawaida, huyu MTOTO SIO DAMU YAKE KABISA.

Mchana namuona boda,
Namwambia aisee nmemuona yule binti wa uji,mtoto Mbona shombe shombe kabisa yule. Akasema nae alishaona na kijiweni wote wanajua.

Sema anajutia Sana gharama na muda aliotumia kuilea ile mimba na mtoto asie wake Kipind chote kile.
Ameingia matatizo makubwa kwasababu ya yule mwanamke. Anajuta hata kuwatambulisha Hadi watu kua anategemea mtoto. Maana hata binti yule anapopita kijiwen na yule mtoto mgongoni anaona Kama fedhea TU.

Boda anasema hawaamini Tena wanawake, aliathirika kisaikolojia Hadi binti wa chuo nae akaamua waachane TU akae peke ake. Haamini Tena katika upendo,watoto na mahusiano.

Sahivi kaamua awe mtu wa kununua na Kuhit&run, hafikirii kuwekeza chochote kwny mahusiano.
Ikitokea binti kapata mimba yake Ni mpaka mtoto azaliwe ndo atatoa taarifa kwa Watu au huduma yyt, na hafikirii Tena mahusiano serious Wala kuoà.

Nmemsikiliza kwa makini,
Sema kwasababu nilikua na ubize flan, nikamwambia ntakutafta baadae tuongee nikushaur vizur. Kasema poa.

Sasa NAOMBEN MNIPE MADINI,
NIMSHAUR VIPI uyu jamaa Maana nmeguswa Sana na suala lake.

Na akiendelea kuwaza hivi,
Sidhan Kama atakua na mwisho mzur uko aelekeapo ukzingatia namuona ni kijana mpambanaji sana aliekua positive sn kifikra.

NAWASILISHA
 
Halafu anatoka mbeya ya wap? Mbona anatuaibisha watu wa mbeya sasa chakufanya ni hivi Kama alichukua chupi ya huyo mwanamke aende kumroga ashike adabu...
 
Wakuu,
Kijiwen nnakopata riziki kwa mbele kdg kuna kijiwe Cha bao na draft huwa wanapaki bodaboda, Nikiwa Sina kazi huwa napenda kukaa pale Kupiga story na kubadilishana mawazo na vijana.

Kuna dada mmoja ni single mother yuko kwny 25s huwa anatembeza uji wa lishe, mi mwnyw Ni mteja wake na namfahamu kua kazaa na boda mmojawapo pale kijiweni.

Mwaka Jana mwanzoni hivi niko kijiweni na uyo boda na wengineo, jamaa mmoja akaulizia yule dada wa uji skuhz haonekani. Ana hamu na uji wake ataupataje.

Wadau wakasema sahv anamimba kubwa TU anaweza jifungua MDA wowote hawez kuja kijiweni. Ikanibd kumtania yule

NAWASILISHA
kupanga ni kuchagua, acha afate vile moyo wake unapenda kwasas
 
Halafu anatoka mbeya ya wap? Mbona anatuaibisha watu wa mbeya sasa chakufanya ni hivi Kama alichukua chupi ya huyo mwanamke aende kumroga ashike adabu...
Sijawahi muuliza mkuu
 
Wakuu,
Kijiwen nnakopata riziki kwa mbele kdg kuna kijiwe Cha bao na draft huwa wanapaki bodaboda, Nikiwa Sina kazi huwa napenda kukaa pale Kupiga story na kubadilishana mawazo na vijana.



NAWASILISHA
Hatari sana, arudishe vitu vya jamaa yetu,
 
Bro, Single Mama Wanavunja Sana Moyo Aisee, Mwambie Asonge Mbele.. Problems are a part of life, facing them is an art of life....... Nina uhakika katika hilo hatokuwa kama alivyo tena, amejifunza jambo
 
Bro, Single Mama Wanavunja Sana Moyo Aisee, Mwambie Asonge Mbele.. Problems are a part of life, facing them is an art of life....... Nina uhakika katika hilo hatokuwa kama alivyo tena, amejifunza jambo
Jamaa kavurugika sana,
Nataka nimuweke sawa arudi kuamini ktkt mahusiano
 
Back
Top Bottom