The Listener
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 993
- 213
Pamoja na yote yaliyotokea Sasa naona Ndo tushampata Rais wetu wa JMT. Kazi imebaki kwetu watanzania kuhakikisha kuwa tunajipatia maendeleo. Hapa nitajikita katika ofisi za umma. Kwa kuwa Mh. Rais Magufuli amejipambanua na falsafa ya hapa kazi tu, ni vema akapewa msaada toka Kwa wananchi wake.
Taasisi nyingi za umma zimekuwa ni 'kapu la kuchota' Kwa watumishi wengi wa Serikali ikimaanisha wamekuwa wakijineemesha Kwa manufaa Yao wenyewe.
Kwa kuanza namuomba sana Mh. Rais Anza na watumishi wenye dhamana kubwa Kwa baadhi ya taasisi za umma. Hapa nitatoa mfano dhahiri. Niliwahi kufanya kazi katika moja ya taasisi za masuala ya ulinzi nchini miaka ya 2000 hadi 2009. Moja Kati ya Vitu Vya kifisadi nilivyoshuhudia ilikuwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Kulikuwa na gari alilokuwa akilitumia bosi na kulikuwa na gari jingine la Serikali lililokuwa likimuhudumia Mke wa bosi na shughuli za nyumbani lakini Kwa gharama za ofisi. Nilijiuliza sana ni ofisi ngapi za umma zinafanya hivi na gharama kiasi gani zinatumika ambazo zingetumika kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo
OMBI: Mh. Rais please piga marufuku suala hili. Yapo maeneo mengine mengi ambayo Mheshimiwa Rais Mimi Kama mwananchi mwema mwenye kupenda maendeleo ya nchi yangu nitaendelea kukuelezea sehemu zenye mianya unayotakiwa kuiziba Kwa manufaa ya nchi na umma Kwa ujumla