ExpertBroker
JF-Expert Member
- Jun 1, 2009
- 454
- 107
Kuna dada tuko naye ofisini, alizaa na jamaa yapata miaka mitano iliyopita! Wakati mtoto ana miezi 4 jamaa akaoa mwanamke mwingine bila kumwambia mzazi mwenzie wa awali! Huyu dada alipata fununu kwamba kuna vikao vinaendelea lakini jamaa akadai ni vikao vya ndugu yake! OK, hiyo si ishu kwani jamaa ana uhuru wa kuoa mwanamke anayemtaka.
Ishu kubwa hapa kwa huyu dada ni kwamba jamaa hataki kabisa kumsaidia mtoto wake kwa maana ya matumizi na school fees, toka mtoto yupo kindagarten na sasa yupo darasa la kwanza! Jamaa hataki kabisa kujihusisha na masuala ya huyu mtoto wake wa nje kwa kuhofia mke wa ndoa atajua! Kinachomuuma huyu dada ni kwamba yeye binafsi ana matatizo na hawezi kumudu kuendelea kumlea mtoto peke yake wakati baba yake yupo hapa jijini Dar na ana kipato, Kinachouma zaidi ni kwamba jamaa hajawahi kumwambia huyu dada kama kaoa? Je, achukue hatua gani?