Tumieni mitandao kujiendeleza na kujenga

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
TUTUMIE MTANDAO KUJITANGAZA NA KUJENGA

NDUGU WATANZANIA POPOTE MLIPO
Napenda kuchukuwa fursa hii kuandika jambo kidogo kuhusu suala hili la mtandao , jinsi tunavyoweza kujenga mitandao yetu kuiunganisha na kuweza kuwa na picha Fulani ndani ya mitandao hiyo – picha ambayo kila anayetembelea aweze kutambua mtandao Fulani kuna watanzania , nikitaka taarifa Fulani za uhakika kuhusu Tanzania na watu wake nitembelee mtandao Fulani , nikitaka marafiki na watu wengine wa kazi walio Tanzania ntembelee mtandao Fulani
Wiki iliyopita tu tulikuwa na sherehe za wiki ya mawasiliano kauli mbiu ya wiki hiyo ilikuwa “ MKINGE MWANAO DHIDI YA MTANDAO “ kabla ya sherehe hizi tuliona jinsi baadhi ya mitandao inavyotumia fursa ya kuwasiliana na kupashana habari , kuharibu , kuchonganisha , kuchochea fujo na hata kutangaza au kusambaza habari za uwongo kuhusu Tanzania na watu wake
Mitandao hii inavyotangaza habari hizi mfano kama ni za uwongo , mtu anayefuatilia anashindwa wakati mwingine kujua ukweli ataupata wapi , hajui hata kitu hicho kinajadiliwa wapi hata kama akijua na kwenda katika mitandao hiyo mingine mingi wanachama wa kule wanatumia majina ambayo si yao kwahiyo inaleta utata kadogo katika kuwasiliana na kutafuta ukweli wa tukio au taarifa
Kuna wale watu ambao wanafanya utafiti ambao una husiana na mitandao au wanapenda kutumia mitandao , watu hawa wanapenda kufanya utafiti wao na watu ambao wanaonekana watu ambao wanatumia majina halisi ili kuweza kuleta ukweli na uwazi katika kazi zao , nashangaa kwanini wataalamu walio bobea katika fani mbali mbali wanatumia majina bandia katika kujadili mambo yanayogusa mambo yao na taifa lao hii ni aibu sana
Napenda kuwasisitizia watanzania haswa wale wanaotumia au wanaopata fursa ya kutembelea mitandao sasa waanze kutumia majina halisi ya kweli , waanze sasa kuamka na kutangaza nchi yao pamoja na mambo ya nchi hii kwa ukweli na uwazi bila kuficha chochote na hata kukosoa kwa namna ya kujenga na kuimarisha umoja , amani na upendo wote tuliokuwa nao toka zamani .
Unapoona taarifa yoyote imekosewa kuhusu Tanzania au sehemu yoyote yenye maslahi yetu kama nchi basi usisite kutoa taarifa zaidi kuhusu suala hilo ili kuweza kupambana na hali hiyo au unapoona taarifa yoyote ina utata au haijakamilika usisite kutoa taarifa mapema au kuuliza zaidi kwa faida zako na nchi yako .
Maslahi yetu lazima yawe mbele linapokuja suala la kujiendeleza na kujitangaza katika mitandao hii , nawashauri hata vijana walio katika vyuo na sehemu zingine za elimu waunde vikundi vyao vya kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa vitu mbali mbali kuhusu mitandao hii jinsi wanavyoweza kuiendeleza na kuijenga zaidi
Tupo nyuma sana ukifananisha na nchi jirani katika kuwasiliana kutoa taarifa , kuhabarishana na kuelimishana hata kuburudishana , sasa enzi hizo naomba tuzizike , tuanze na nguvu mpya sasa katika kujenga , kuburudisha , kuelimisha na kupashana habari moto moto ambazo si za chuki wala majungu kuhusu nchi yetu na watu wake .

Katika mitandao kuna vitu vingi sana ambavyo wewe kama mzalendo unaweza kushiriki kutokana na fani uliyokuwa nayo wewe , kama wewe ni mhandisi basi tumia nafasi hiyo kuimarisha fani hiyo na kuijenga zaidi kwa kuunda mitandao ya kiuhandisi kama wewe ni mshairi hivyo hivyo tufanye hivyo kwa lugha tukufu ya Kiswahili mwishowe tutafanikiwa na kuwa na mafanikio zaidi .
Kwa kuanzia unaweza kutembelea mtandao wa wanabidii : Wanabidii | Google Groups

Wanabidii imeunganishwa na zaidi ya vyombo 100 vya habari duniani na ringi zaidi ya 60 unapoandika chochote au kuchangia chochote jua kinaenda katika vyombo vya habari vingi wahariri wanapata kusoma kile ulichoandika kwa sasa tunashirikiana sana na mitandao migine ya kutafsiri lugha iweze kuutambua mtandao huu
Jisajili hapo uweze kuona faida za kuwasiliana uweze kujenga na kuelimisha jamii yao popote .
Kama utashindwa kujisajili upokee taarifa wasiliana na oldmoshi@gmail.com utaunganishwa mara moja
Wanabidii ni mwanzo tu mengine mengi na wazuri yanakuja ya kujenga picha ya taifa letu katika mitandao ya kimataifa .
 
... nashangaa kwanini wataalamu walio bobea katika fani mbali mbali wanatumia majina bandia katika kujadili mambo yanayogusa mambo yao na taifa lao hii ni aibu sana
Napenda kuwasisitizia watanzania haswa wale wanaotumia au wanaopata fursa ya kutembelea mitandao sasa waanze kutumia majina halisi ya kweli
Ni jambo zuri, ila wakati mwingine hata serikali yetu imetufundisha hivyo. Kwa mfano, polisi inatoa namba za simu za kufichua au kuripoti uhalifu, na unaambiwa kwamba unapotoa taarifa si lazima utaje jina lako, tutajifunza nini? Lakini kwa upande mwingine mtu anaweza akawa na nia nzuri tu kujadili mambo yenye maslahi kwa taifa, ila kwa kuhofia usalama wake (maybe jambo hilo litaharibu maslahi ya watu wenye nguvu kifedha etc), inabidi aripoti tu kwa kuficha jina lake halisi, na ninadhani huyu atakuwa amefanya vizuri kuliko aliyenyamaza.
 
Sounds like Marketing the Mtandao flani....!

Somebody in here(JF) said that its around 2% of

Tanzanians who are accessed by the Electricity Power...

and hence the computers!

So, a lot is to be done so as to make this Marketing worth

it, pal...!

Labda ndo maana 'mwenye nchi' anaongea na

jamaa wa Google etc ili tusogeesogee..ha ...ha...haaa!

Kaaaz kwelikweli...
 
Back
Top Bottom